mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Tatizo lako Mkuu jambo lolote baya likitokea hapa nchini, wewe huliusisha na CDM, BAVICHA ama Tundu Lissu. Na pia lolote zuri likitokea huliambatanisha na CCM ama Mh. Magufuli. Na hapo unakuwa ndiyo hitimisho kwako.Hii imekuja baada ya chadema kugeuka chama cha kushangilia mabaya yote yanayoitokea nchi, mfano kukamatwa kwa ndege, kunyimwa misaada na korosho kukosa soko.View attachment 1189315
Si mbaya kuwa "biased' ama kuwa na "prejudices" lkn ni lazima ujipe muda kuchimba zaidi "facts" na kuzimwaga hapa jamvini kwa uelewa zaidi. Sasa, wewe ukiokota kipande cha habari popote pale ulipopata huishia tu kusema wanafuria mabaya.
Nahisi kijiwe chako ama maskani yako ni unakutaba masela na wahuni waliodatishwa na maisha ya Uswazi, na wewe ndiye ambaye unsonekana pekee kipanga mwenye nondo kichwani. Kwa hiyo masela wakiku "challenge" unawamaindi kutokana na msimamo wako wa kiitikadi na unawahisi kuwa ni CDM.
Sasa,kama hicho ndicho chanzo chako kikuu cha habari si lazima kuja kila mara na kuzitupia huku. Kuleta swaga huku ni kulishushia jukwaa hili heshima. Ndiyo! CDM kuna mambo hayapo vyema, na yenye kuhitaji kurekebishwa. Jenga hoja, njoo na "references & factual statements". Mbona tutakupa shavu tu? Ebu jitafakari Mkuu. Samahani sana lakini.