Mzamiru Yassin ni jipu ndani ya Simba SC

Mzamiru Yassin ni jipu ndani ya Simba SC

Tipstipstor

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
1,528
Reaction score
3,352
Watu wengi wanamsifia kama kiungo punde ila kwa maono na maoni yangu binafsi namuona kama mchezaji wa kiwango cha chini sana kuichezea klabu kubwa kama Simba SC.

Miongoni mwa madhaifu yake ni kushindwa kupiga pasi za maana,mara nyingi amekuwa mtu wa kupoteza pasi.

Uwezo wake wa kumiliki mpira pia ni mdogo.

Madhaifu mengine ni kuwa ana maamuzi mabovu sana wakati timu inashambulia, hajui atoe pasi au apige shuti. Kitendo kinachopekea kupoteza mipira na kuigharimu timu.

Mwisho kabisa ni kuwa hajui kusukuma mpira nyavuni, kama utachunguza game nyingi za Simba, amekuwa akipata nafasi za kufunga lakini amekuwa akizipoteza.

Wito na ombi langu kwa uongozi wa simba ni kuwa wajitahidi kutafuta mbadala wa kiungo huyo punda.

Nawasilisha
 
Ndo maana nasema benchi lote la Simba livunjwe asibaki hata Matola ,maana kuna makocha wana wachezaji wao,mtu kama Matola nirahisi kugawiwa na mchezaji yeyote wa ndani ,akipewa kitu naye anamgawia Kocha mkuuu ili awe first 11.

Sisi mashabiki tunaona kila kitu,Bocco ,Mzamiru hapana tunawaona.

Ila Dilunga ,Shabalala na kidogo Kapombe sawa.

We unadhani hawa wachezaji wote hawapeani mchongo kama sisi mtaani kwenye mishemishe tunavyopeana mchongo? Mwisho wa siku mpira ni kipaji na talent ya mda mashabiki wanaona nani yuko vizuri hata mashabiki wanakupangia first 11 inayojituma na wanaostahili kwa mda huo
 
Timu yote hovyo, Bocco,Kibu, Sakho Kagere muhimu ni kuchunga timu isishuke daraja
 
matola kazi yake kubwa ni kuuza 'game plan ya Pablo' kwa tim pinzani,na kwa akili zake ndogo anafikiri anamkomoa Pablo kumbe anakomoa makolo team yoote, Mbeya City, Mtibwa na Kagera Sugar walijuaje game plan za mechi zao na simba 'a day before' ………..
 
Hivi mnadhan kuchukua ubingwa back to back 4yrs mchezo ee?

Mzamiru mnayembeza Leo ndyo aliyetufikisha robo fainal 2 CAF CHAMPION LEAGUE
na ubingwa Tanzania Mara 4 Azam 2

Tuwe na shukran jaman Kama alitupatia raha mda wote tumfariji pia. Kipind hiki kigumu wanachopitia wavhezaj wetu

Mbona Liverpool wamekaa miaka 30 bila ubingwa man u unaenda mwaka wa 10 huu arsenal mwakanwa 20 huu lakn mmevumilia

Leo mzamiru mwez TU mnamkashifu

PROJECT YA SIMBA IMEFIKA KIKOMO VIONGOZI WALIANGALIE HILI

Kuanza upya kutengeneza timu si ujinga

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Bongo hakuna ushabiki ni mataputapu tu
 
Si mnasema hata mwaka jana Yanga aliongoza ligi ila ubingwa mkabeba nyie?Hyo kauli imepotea tena?🤣🤣🤣🤣
 
Kwa mbaaaaaaaaaaaali, nauona uzi wa kutoka kwa Kolo ukiwa na maneno "...atuachie klabu yetu, anadhani netball au rede hii" Kumbe wasichojua Kolo, akitoka da' Barbara anakuja Fatema huku akiwa na cv "mzuri" kutoka Simba Queen!
 
Natabiri Simba atamaliza nafasi ya 4 kwenye ligi asipobadilika
 
Kwa mbaaaaaaaaaaaali, nauona uzi wa kutoka kwa Kolo ukiwa na maneno "...atuachie klabu yetu, anadhani netball au rede hii" Kumbe wasichojua Kolo, akitoka da' Barbara anakuja Fatema huku akiwa na cv "mzuri" kutoka Simba Queen!
Hahahaaa
 
[emoji94].... Djigui Diara aliondoka akiacha Simba ina point 24

Anarudi anakuta Simba ina point 25

Anajiuliza Ligi ilisimama au???!![emoji848][emoji848][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom