Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kinachoitwa pesa za Abdul na Lissu ni pesa zake za matibabu anazoidai Serikali, Abdul alikuwa anatumika kujaribu kusaidia kufanikisha zitoke. Hata hivyo ni jambo la kusikitisha katika nchi yetu mambo yanabidi kupelekwa hivi wakati mwingine ili mtu apate haki yake tu, ila huo ndio uhalisia.
Lissu alishapoteza imani na Mbowe muda mrefu akawa anajaribu kutengeneza mtandao wake dhidi ya Mbowe lakini haukufanikiwa sana, alijaribu kusingizia amehongwa magari na serikali.
Lissu akiwa makamu mwenyekiti alianza kubagua viongozi wa chama chake na kukigawa chama, alimpigia kampeni Msigwa dhidi ya Sugu na akajaribu bila mafanikio kutaka kumpigia kampeni Wenje dhidi ya wagombea wengine.
Lissu hajawahi kutoa kauli yoyote hasi dhidi ya Msigwa au kumtetea Mbowe kwa lolote pamoja na kashfa zote ambazo Msigwa amekuwa akimtolea Mbowe, hii sio kawaida.
Lissu alikuwa amepewa kwenye majukumu yake ya makamu mwenyekiti lakini pia amekuwa akijifanyia mambo ya ki chama kama mtu binafsi, yeye anavyoona inafaa tu bila kuzingatia mawazo ya wengine, maazimio, umoja na misimamo ya chama.