Mzani wa ubaya ndani ya CHADEMA umeelemea upande wa Lissu!

Mzani wa ubaya ndani ya CHADEMA umeelemea upande wa Lissu!

Lisu aliona ndani ya CDM hakuna tena anayeaminika

Sasa ameamua kusimama pekee yake na anakwenda kushinda

Naimani Lisu ni mmoja ya watu wanaojua mengi sana ya nchi hii kuliko yoyote ...
Hata mimi ananizidi kilaza Lisu?
 
Kinachoitwa pesa za Abdul na Lissu ni pesa zake za matibabu anazoidai Serikali, Abdul alikuwa anatumika kujaribu kusaidia kufanikisha zitoke.

Lissu alishapoteza imani na Mbowe muda mrefu akawa anajaribu kutengeneza mtandao wake dhidi ya Mbowe lakini haukufanikiwa sana, alijaribu kusingizia amehongwa magari na serikali.

Lissu akiwa makamu mwenyekiti alianza kubagua viongozi wa chama chake na kukigawa chama, alimpigia kampeni Msigwa dhidi ya Sugu na akajaribu bila mafanikio kutaka kumpigia kampeni Wenje dhidi ya wagombea wengine.

Lissu hajawahi kutoa kauli yoyote hasi dhidi ya Msigwa au kumtetea Mbowe kwa lolote pamoja na kashfa zote ambazo Msigwa amekuwa akimtolea Mbowe, hii sio kawaida.

Lissu alikuwa amepewa kwenye majukumu yake ya makamu mwenyekiti lakini pia amekuwa akijifanyia mambo ya ki chama kama mtu binafsi, yeye anavyoona inafaa tu bila kuzingatia mawazo ya wengine, maazimio, umoja na misimamo ya chama.
Mkuu, CHADEMA wamejitanabahisha kama chama chenye msimamo mkali dhidi ya ufisadi na kukosekana kwa maadili ndani ya serikali na makada wake kama Lissu, Wenje, Lema na wengineo wakiwa firebrands (vichomi) kabisa katika kupambana na serikali kuhusu tuhuma mbalimbali za kifisadi.

Kwa mazingira hayo, kitendo cha kada muhimu Wenje kuwa na "dili" na huyo Abduli bila kuchukuliwa hatua yoyote tena akikubaliwa kugombea umakamu mwenyekiti wa chama, ni kielelezo tosha kuwa kutakuwa na MATATIZO MAKUBWA SANA ndani ya CHADEMA. Kama Wenje ni "mtu wa Mbowe" huu ni msiba.

Nashindwa kupata picha. Wenje aliwezaje kumfuata Abduli na kisha kumpeleka kwa Lissu eti "amsaidie" kupata malipo yake (ya halali) serikalini?!! Alitoa wapi huo ujasiri? Lissu ninayemfahamu ni bora azikose hizo hela kuliko kuweka dili na mafisadi wanaohujumu taifa wakati huu. Mtikila alipokea hela za Rostam na kufifia. Sioni Lissu akiruhusu hali hiyo.

Mkuu, kwa andiko lako hili umeshusha hadhi uongozi mzima wa CHADEMA!

Unakubali tukubaliane kuwa CHADEMA si chama makini cha upinzania tena bali A BIG POLITICAL HOAX?
 
Mkuu kwanza nakubali kitendo kilichoelezewa na wenje hakina picha nzuri sana kwa jamii inayolilia usawa, ilitakiwa upatikanaji wa haki usiwe kwa kujuana na kona kona nyingi hivi(hata hivyo uhalisia ni kwamba tuko mbali sana na mfumo huo wa kupata haki/stahiki). Jambo ambalo mimi haliniingii akilini huu ulikuwa ni ufisadi au hongo ya kimfumo ndani ya CHADEMA.

Kitu ambacho nakiona kwa CHADEMA kuna kuchokeshwa au kuchoshwa (fatigue) na jinsi wamefanya siasa za harakati kwa muda mrefu bila mafanikio au kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa raia kwa aina hiyo ya siasa, hapo ndipo yakaja mambo ya maridhiano na hata kutumia njia zile wengine wanazozitumia kupata haki zao ikiwemo hiyo ya kumuangukia Rais.

Mkuu fikiria umedhulimiwa kiwanja, umepigwa dana dana kuipata haki yako idara ya ardhi na kesi mahakamani imekuwa mzunguko usioisha, halafu kuna Makonda ambaye huyakubali mambo yake mengi na unajua sio msafi lakini unajua ukimueleza kwa sababu zake za kisiasa atakusaidia kutatua shida yako na utapata haki yako, utafanyaje?!
 
Mkuu uko sawa lisu alipata madhara sana baada ya lile shambulio hali imepelekea ubongo kuwa na matatizo. Leo anasema hivi kesho vile yaani kwa ufupi jamaa hajielewi. Mbowe asikubali kuachia hicho kitu ni hatari sana.
 
Wewe ndiye hujui, kisheria Rais sio mgawa haki nchi hii wala hatakiwi kushawishi maamuzi fulani ya utoaji haki yafanyike kwa sababu eti yeye ni Rais. Mahakama ndio chombo cha mwisho cha utoaji haki, kama Lissu alinyimwa pesa zake na bunge au na serikali angeenda Mahakamani na uamuzi wa mahakama ndio ulipaswa kuwa final.

Ni mfumo dhaifu tu wa haki ndio unaotoa mwanya wa wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri na Rais kufanya maamuzi ya kugawa haki mfano katika kesi za ardhi, kodi, mirathi n.k ila sio utaratibu sahihi wala sheria
Kwa mahakama zetu hizi ambazo kila wakati zinakuwa remoted by ule mhimili uliojichimbia chini zaidi sijui kama angeweza kupata haki yake.
 
Back
Top Bottom