Tatizo wazazi wengi wampeitia huko ndio maana wanaamini ndio njia sahihi lakini ukweli ni kwamba kama nyumbani kuna uwezo wa kulipa ada ya chuo ni heri mtu aende chuoni, huko 5 na 6 ni kwa wale wasio na uwezo wa kwenda chuoni ama walae wanaotaka kuwa walimu wa advance
Kwenda chuo kuna faida ambazo mtu wa form 6 hawezi kuja kuzipata,
mimi nilisoma form 6 naingia chuoni kusome degree nakutana na wale waliosoma diploma tayari wapo wenye kazi tayari wanajisomesha, yaani wanaongeza elimu ya degree ili wapandishwe madaraja sio kuanza kutafuta ajira kama sisi
Waliowahi kuanza chuo mapema wana uwanja wa ajira mkubwa, wao wanaweza kuomba kazi za diploma na degree lakini wale wa form 6 wanaomba kazi za degree tu, kazi za diploma nafasi 10 zinatangazwa unakuta wanaoomba ni 500 lakini kazi za degree nafasi 10 wanaoomba ni elf 10,
Kitu kingine ni kwamba wanaoenda kusomea diploma wana cv inayovutia kiuzoefu kuzidi aliesoma form 6, ni kwamba wao wamesomea taaluma kwa muda mrefu zaidi tangu wamemaliza form 4, wana vyeti vya kitaaluma vingi (certificate + diploma + degree) na pia wana wamefanya kazi kwa vitendo maofisini zaidi kuliko yule wa form 6 anaeanza kusomea taaluma kwa mara ya kwanza baada ya form 6.
Urahisi wa Kubadili kozi, Mtu wa diploma anaweza kubadili kozi baada ya kupata muda wa kutafakari kwa kina akiwa chuoni kozi anayoona itamfaa, Mfano anaanza kusomea certificate ya mwaka moja designing lakini huko chuoni anakuja kuona kuna kozi nyingine nzuri zaidi, akiingia diploma anabaili kozi na huko anaweza kuona kuna kozi flani anaweza kupata connection ajira, akiingia degree anabadili, wale wa form 6 hawana urahisi katika hili, wengi inabidi warudie upya kusomea degree.
Kuzoea maisha ya chuo mapema, Nakumbuka nikiwa chuoni baada ya kumaliza form 6 watu wengi ule mwaka wa kwanza walikuwa hawafanyi vizuri kwenye masomo kwajili ya ugeni wa vitu vingi kuanzia uhuru wa maisha ya chuoni, style ya kusoma, kuandaa assignments, presentations, n.k. muda huo wenzetu waliosoma diploma washavizoea, Ni kweli kwamba waliokuwa wanakimbiza ni wale vipanga wa form 6 lakini pia waliokuwa wanafeli sana ni hao hao wa form 6, wale wa diploma walikuwa average na ni kwasababu kipindi hicho wengi walikuwa wana divison 4 form 4, lakini siku hizi hata wenye division 1 na 2 wanaenda naamini hali imebadilika.
Unataka kusomea designing ya nini