Mzazi ananilazimisha kwenda kidato cha Tano

Inategemea msingi wa hicho kitu unachopenda ni upi, mfano mtotot amekaa na watoto wenzake wakashauriana tukasome ualimu na wewe mzazi unajua kabisa ualimu kwenye nchi hii huyu dogo atateseka je utaacha tu mtoto akasome ualimu kisa amekwambia anapenda ualimu?

Na mda huo huo kwa kuangalia trend yake ya masomo na matokeo yake ya form4 unaona kabisa anauwezo wa kusoma hata MD, Engineering au phamarcy bila shida yoyote, je utamruhusu akasome huo ualimu?
Nakazia hoja. Wazazi wana nafasi kubwa sana katika kumwongoza mtoto wao ili baadaye awe na mafanikio makubwa zaidi.
Mtoto bado ana akili finyu (akili haijafunguka) na maono (vision) yake yanahitaji mtu wa kumwongoza, kumshauri na kumpatia maelekezo sahihi.
 
Naombeni msaada wa mimi mwenyewe : ni kwamba nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nimepata division 2 ya 21 nataka kwenda chuo ila mzazi wangu ananilazimisha nifanyaje sasa ili niweze kwenda college kwasababu nataka nisome mambo ya designing
Kama anakulazimisha kwenda chuo kusomea sayansi msikilize,
Kama ana connections za kukupa baada ya kumaliza chuo msikilize
Kama ana mtaji wa kukupa baada ya kumaliza chuo msikilize
Kama ana biashara za kukuweka baada ya kumaliza chuo msikilize
Vingnevyo mpuuze tu.
 
Ungekuwa unaenda chuo kusomea kozi za skills za kueleweka. Kama ufundi magari, umeme,. Unesi , ufundi electronics,, Ningekusapoti.

Ila mambo ya kwenda chuo kusomea designing naona haupo serious na maisha.

Ni bora uende advance
Designing ya nini kwanza?
 
Tatizo wazazi wengi wampeitia huko ndio maana wanaamini ndio njia sahihi lakini ukweli ni kwamba kama nyumbani kuna uwezo wa kulipa ada ya chuo ni heri mtu aende chuoni, huko 5 na 6 ni kwa wale wasio na uwezo wa kwenda chuoni ama walae wanaotaka kuwa walimu wa advance

Kwenda chuo kuna faida ambazo mtu wa form 6 hawezi kuja kuzipata,

mimi nilisoma form 6 naingia chuoni kusome degree nakutana na wale waliosoma diploma tayari wapo wenye kazi tayari wanajisomesha, yaani wanaongeza elimu ya degree ili wapandishwe madaraja sio kuanza kutafuta ajira kama sisi

Waliowahi kuanza chuo mapema wana uwanja wa ajira mkubwa, wao wanaweza kuomba kazi za diploma na degree lakini wale wa form 6 wanaomba kazi za degree tu, kazi za diploma nafasi 10 zinatangazwa unakuta wanaoomba ni 500 lakini kazi za degree nafasi 10 wanaoomba ni elf 10,

Kitu kingine ni kwamba wanaoenda kusomea diploma wana cv inayovutia kiuzoefu kuzidi aliesoma form 6, ni kwamba wao wamesomea taaluma kwa muda mrefu zaidi tangu wamemaliza form 4, wana vyeti vya kitaaluma vingi (certificate + diploma + degree) na pia wana wamefanya kazi kwa vitendo maofisini zaidi kuliko yule wa form 6 anaeanza kusomea taaluma kwa mara ya kwanza baada ya form 6.

Urahisi wa Kubadili kozi, Mtu wa diploma anaweza kubadili kozi baada ya kupata muda wa kutafakari kwa kina akiwa chuoni kozi anayoona itamfaa, Mfano anaanza kusomea certificate ya mwaka moja designing lakini huko chuoni anakuja kuona kuna kozi nyingine nzuri zaidi, akiingia diploma anabaili kozi na huko anaweza kuona kuna kozi flani anaweza kupata connection ajira, akiingia degree anabadili, wale wa form 6 hawana urahisi katika hili, wengi inabidi warudie upya kusomea degree.

Kuzoea maisha ya chuo mapema, Nakumbuka nikiwa chuoni baada ya kumaliza form 6 watu wengi ule mwaka wa kwanza walikuwa hawafanyi vizuri kwenye masomo kwajili ya ugeni wa vitu vingi kuanzia uhuru wa maisha ya chuoni, style ya kusoma, kuandaa assignments, presentations, n.k. muda huo wenzetu waliosoma diploma washavizoea, Ni kweli kwamba waliokuwa wanakimbiza ni wale vipanga wa form 6 lakini pia waliokuwa wanafeli sana ni hao hao wa form 6, wale wa diploma walikuwa average na ni kwasababu kipindi hicho wengi walikuwa wana divison 4 form 4, lakini siku hizi hata wenye division 1 na 2 wanaenda naamini hali imebadilika.

Unataka kusomea designing ya nini
Sahihi kabisa
 
Mwenye ada ni mzazi. Usisikilize maneno ya waja na walimwengu hayatakupeleka popote. Nenda advance huku ukiifanyia research ndoto yako
 
Umesema kweli yote
 
You jad a chance to assist her to make a good choice man! Unadhani ni raha kumuona mwanao nyumbani hawezi hata kunununua vocha!
Haya mtoto ndio huyu anakwambia anataka akasome "design" wewe kama mzazi utamuelewa?
Kuliko kutoka kabisa ndani ya mawazo na interests zake, ningemshauri asome chuo kwa baadhi ya masomo yenye ajira mbeleni.

Akikataa nitamuunga mkono akasome tu. Maisha ni yake. Huwezi kua anachowaza.
Mtoto kapenda hivyo mi nimlazimishe ili iweje.
Akienda akivuruga acha aje tubanane nyumbani si mtoto wangu, nitamkataa? Au kumfukuza.
 
You jad a chance to assist her to make a good choice man! Unadhani ni raha kumuona mwanao nyumbani hawezi hata kunununua vocha!
Haya mtoto ndio huyu anakwambia anataka akasome "design" wewe kama mzazi utamuelewa?
Kwanza sijaelewa hio designing ni nini, ni fashion au nini?
Nitakaa nae chini kumsikiliza kwa nini anataka kusoma hiko anachohitaji, then nitamshauri, kama ni issue ya mavazi labda anapendezwa kujiajiri na kuanzisha baadae ofisi yake ambayo atakuwa anashona.

Kikubwa naamini sana kwenye kitu mtu anachopenda.
 
Hata mimi naamini katika kitu mtu anapenda ila kama mzazi lazima uwe na akili hasa pale unapoona mtoto hajielewi au amachagua vitu ambavyo havina future nzuri maana wengi wanafanya machaguo sio kwa kutumia utashi ila kwa kufwata mkumbo!

Bado narudi kwenye swali la msingi, wewe mwenyewe kama mzazi hujui hiyo "design" inahusu nini yet umekomaa kunshauri aende diploma yaani unamwambia akasome kitu ambacho hata wewe mwenyewe hukijui! Hii ni shida kwa kweli!
 
Nina uhakika kabisa kuna watu walikudanganya kuwa advance unapoteza muda , na hao mara nyingi ni wale waliofeli
Huwezi niambia mtu amepata div 1 au 2 tena kihalali kabisa alafu awe muoga kwenda alevo!

Kuna mawili either aliibia mtihani au anafwata mkumbo!
 
Naombeni msaada wa mimi mwenyewe : ni kwamba nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nimepata division 2 ya 21 nataka kwenda chuo ila mzazi wangu ananilazimisha nifanyaje sasa ili niweze kwenda college kwasababu nataka nisome mambo ya designing
Ushauri wangu nikiwa kama mtu mwenye experience ya miaka kadhaa kwenye industry ya graphics design na printing kwa ujumla. Baada ya ongezeko na college uchwala nyingi kuanza kufundisha wanachokiita graphics design soko la ajira hii limebadilika sana ila kuna opportunity nyingi kama utakuwa ni mtu mwenye kujiongeza. Kuhusu swala lako la kusoma sikushauri kabisa upite hiyo shortcut, kubali uende form 5 ukibarikiwa kufika chuo kasome IT au mass media. Wakati upo chuoni ndio uwe unajinoa kwenye issue za design (graphic design, motion graphics, 3D design). Usisahau kukazia kwenye somo la ujasiriamali na ikiwezekana maswala ya marketing.

N.b hii fani bado ajira zake zipo kwenye mfumo wa ujamaa zaidi.
 
Acha hizo ww. Msikilize mzazi wako na halafu uwe mtiifu kwani hicho kidato cha nne ni sawa na kusema umefuta ujinga tuu; sasa nenda kasome. :KEKBye:
Acha kumshauri hivyo mimi mwenyewe wazazi walitaka kunipeleka advance ila nilipitia kwenye mgogo wa mwanafunzi wa advance si virahisi kuajiriwa maana wazazi walitaka niajiriwe nikaona hapa ndio pakupitia so panga mistari ya kwenda nayo kwa wazazi na tafuta watu wakukusupport hasa ndugu wa karibu waliosoma wanao sifahamu faida za kwenda chuo badala ya advance
 
Naombeni msaada wa mimi mwenyewe : ni kwamba nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nimepata division 2 ya 21 nataka kwenda chuo ila mzazi wangu ananilazimisha nifanyaje sasa ili niweze kwenda college kwasababu nataka nisome mambo ya designing

Naombeni msaada wa mimi mwenyewe : ni kwamba nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na nimepata division 2 ya 21 nataka kwenda chuo ila mzazi wangu ananilazimisha nifanyaje sasa ili niweze kwenda college kwasababu nataka nisome mambo ya designing
Kama ada unaeza lipa, nenda tu. Mnatusumbua sana wazazi wenye fikra hii
 
Back
Top Bottom