Mzazi ananilazimisha kwenda kidato cha Tano

Kuna kazi bila kupitia kidato Cha 5 sawa na kuvaa suruali juu yake ukavaa boksa.
 
Ungekuwa unaenda chuo kusomea kozi za skills za kueleweka. Kama ufundi magari, umeme,. Unesi , ufundi electronics,, Ningekusapoti.

Ila mambo ya kwenda chuo kusomea designing naona haupo serious na maisha.

Ni bora uende advance
Kwa hiyo mkuu umeona nursing ni skills based kuliko designing ???.....

Pia hajasema design ya nini, ni interior design au clothing design..

Kama ni clothing design, bado inalipa Ila anatakiwa kuwa highly talented ili watu wamuone. Ukifuatillia nguo mfano za maharusi na mtu akiwa na jina. Usishangae suti au shela moja ni mshahara wa nurse wa miezi miwilli

Plus kumsagia kunguni kwa umri wake sidhani kama ni sawa maana hana experience wala maturity ya kufanya maamuzi. Tumshauri kwa lugha atakayoielewa kwa umri wake
 
Kwa hiyo unamshauri aende chuo akasome "designer"?

Kabla ya kumpa huu ushauri ulikua unajua anaenda kusoma nini huko chuoni?
 
Kama unajua hana maturity kwanini asisikilize anachoambiwa na wazazi wake?

Pia umenishangaza sana umetoa ushauri mreeefu kumbe hata hiyo "design" anayotaka kwenda kusomea huko chuo huijui. Ungekua na akili kama ungetaka kujua hiyo "design" ilikua ni kitu gani kabla ya kutoa ushauri!
 
Umeandika ga
UMeandika gazeti reeeefu kumbe hata hujui hiyo design ni ya kitu gani?
 
Faida za kwenda advanced???
Shida yenu nyie vitoto mkikaa kwenye magroup yenu na baada ya kuangalia movi za wazungu mnakaa mnashauriana ujinga bila kujua mnaishi tanzania na sio ulaya!

Sasa tuambie

1. Wewe na wazazi wako nani anaijua hii dunia?

2. Je hiyo "design" unayotaka kwenda kusomea huko chuo inahusu nini?

3. Kama kweli hiyo div2 uliipata kwa juhudi zako kwanini unaogopa kwenda form5?
 
Mosi, si kila ushauri unaangalia maturity Ila life experiences, professional capacity, exposure na flexibility ya mzazi kuweza kuangalia ni nini mtoto anataka, capacity yake na uhalisia wa soko la ajira au kujiajiri. Ndio maana si kila mzazi anaweza kufanya career guidance kwa hiyo kama wewe unaamini hivyo. Mimi naamini tofauti

Pili, nimetoa ushauri kwa assumption yenye general advice inayoweza kumsaidia yeye muhusika lakini pia kwa comment ya niliyemquote. Ni technique tu

By the way kutumia character assassination kwenye discussion is not my style, so ukiniona sina akili ni sawa pia maana naheshimu uhuru wako wa kuwa na opinion. Upo sawa kabisa
 
Mitoto ya siku hizi bhana! Huko mashuleni wao kwa wao wanajazana ujinga tuu; eti anataka kusoma designing............ 👉
Mtoto aliyehitimu mwaka jana ina maana alizaliwa 2005/6. Pata picha. 😁
Bila shaka ulibunda kidato cha nne na inakuumiza hadi uzeeni
 
Mafanikio huja kwa kupenda unachofanya, ukifuata maneno ya mzazi sidhani kama utasoma kwa bidii, nafsi yako imekwisha kataa.
Inategemea msingi wa hicho kitu unachopenda ni upi, mfano mtotot amekaa na watoto wenzake wakashauriana tukasome ualimu na wewe mzazi unajua kabisa ualimu kwenye nchi hii huyu dogo atateseka je utaacha tu mtoto akasome ualimu kisa amekwambia anapenda ualimu?

Na mda huo huo kwa kuangalia trend yake ya masomo na matokeo yake ya form4 unaona kabisa anauwezo wa kusoma hata MD, Engineering au phamarcy bila shida yoyote, je utamruhusu akasome huo ualimu?
 
1. How sure are you kwamba mpaka wazazi wake wanamshauri akasome form5 kwamba hawana uwezo wa kufanya "career guidance"?

2. Unaweza kuwa na wazo zuri ila hili ni jukwaa na ujue wenda huyu bado ni mtoto na ukimpa ushari wa jumla kama uliompa wenda ukampoteza kabisa! na ndio maana nikasema ingekua vyema ukatoa ushauri baada ya kujua hiyo "design" anayotaka kusomea ni nini! Wenda ungeijua ni ipi usingemshauri kama ulivyomshauri!

NB: jua kabisa mzazi anamshauri maana kwanza anamjua mwanae na anajua maisha yalivyo na yeye ndiye atakuja athirika kwa namna fulan mtoto anapomaliza masomo alafu kazi hana!
 
Ni bora kumuacha tu akasoma anachotaka, mambo yakiharibika mbeleni atakaa na kujilaumu yeye, sio kuanza kumsumbua na kumlazimisha mtoto utafikiri we ndiye unasoma.
Akivuruga huko shuleni baadae anaanza kukulaumu.

Mi huwa naona ni wazazi wa hovyo ndio hulazimisha mtoto kusoma anachoona anahisi kinafaa yeye binafsi.

Kikubwa kaa naye chini mshauri kiutu uzima na kiurafiki, mueleze faida na hasara za maamuzi anayofanya.

Kama anakwenda chuo muache aende chuo kikubwa mshauri asomee mambo yapi, mtu anasema anapenda chuo, mzazi anamlazimisha aende advance, haipendezi.

Ndio hao wazazi huchagilia watoto mke hata kama hampendi utasema ye ndiye anaingia ndoani.
 
Designing ya nini?
Tuanzie hapo maana huwa mna ndoto za kizungu sana katika nchi ambayo kutwa rasilimalu zinauzwa.
Mtakufa vibaya nyie nawahurumiaaaa
Shida ya hivi vitoto vikishapata marks nzuri vinajiona vinajua kila kitu kwenye hii dunia. Vinajiona vina akili kuliko wazazi wao.
 
Mkuu ni wapi nimesema anatakiwa kulazimishwa.

Je unadhani akienda kusoma vitu visivyo na kichwa wala miguu alafu akamaliza chuo akaja kukaa hapo nyumbani unadhani kama mzazi haitakuuma?

Au unashauri akimaliza akiwa anasoma namba mzazi auchune kisa hakufwata ushauri uliompa?

Haya turudi kwako, huyu angekua mwanao anakwambia anataka kwenda chuo akasomee "design" wewe ungemuelewa?
 
Kuliko kutoka kabisa ndani ya mawazo na interests zake, ningemshauri asome chuo kwa baadhi ya masomo yenye ajira mbeleni.

Akikataa nitamuunga mkono akasome tu. Maisha ni yake. Huwezi kua anachowaza.
Mtoto kapenda hivyo mi nimlazimishe ili iweje.
Akienda akivuruga acha aje tubanane nyumbani si mtoto wangu, nitamkataa? Au kumfukuza.
 

Nakubali unachokisema ndio maana majibu yangu huwa conditional. Sijampa mtu framework, ila nimetoa keypoints. Kuna tofauti hapo mkuu

Ni sawa umeona mtu anatoa side A, wewe ukatoa side By, haimaanishi side A ni mbaya ila unatakiwa kubalance both sides ili kumpa mtu mawazo yaliyo balanced ili aweze, kutoa maamuzi..

Upo sawa na Mimi nipo sawa kwa upande wangu. Mwenye kujua kipi ni sahihi ni ye yr atakaesoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…