Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Mie bhana napenda kufanya kitu kwa uhuru na maamuzi yangu, sitaki mambo ya kuridhisha watu. Siwezi
Shida hapa kwetu ukiishi uhalisia wako lazima wakuone mara kibru mara dharau ilihali unaishi ukipendacho .

Sikatai wazazi wanatuzaa na pia wanatulea ila wana muda wa kuwa washauri tu sio kuwa mlazimishaji kwa kofia ya mzazi.

Nilipata kadada masikini kakanipenda sana basi mtoto wa mjini si nipo village nikawa nakavusha nakaleta maeneo .

Duh kumbe wanakijiji wamenilia timing basi wakaja kufosi siku moja nikaoe kwa lazima ati namuharibia maisha .

Nikasema sawa shida ikaanza kwa mama mzazi kumpigia simu bintiye mara mbona jana sijakuona kanisani ? Mara ooh kwahiyo sasa hivi umeamua kuvaa kama wauza bar?

Mwisho mdada wa watu akawa dillema anisikilize mimi au wazazi ila wazazi wakanishinda maana alikuwa sehemu za kwao .

Na mimi nikapata chance ya kusema sasa silipi mahari na binti yenu njoo mumchukue maana sasa ni kama bado mnaishi naye hamtaki amtii mme wake bwana MENEMENE TEKERI NA PERESI

Wakaja kumchukua binti yao na mim nikawa huru na maisha yangu .

Sasa nakaona kamekonda kameolewa na jamaa anaranda mbao ni baunsa sana hivyo anakanyonya mpaka kamekonda kamebaki kichwa tu.[emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzazi yuko sawa kama unakaa nyumbani kwake tii mamlaka ya mwenye nyumba kama huwezi hama [emoji35]
 
Kwani ni lazima? Hata nikienda kumfurahisha anione nimeenda.
Je vipi kiimani? Mungu anaonaje?
Maana naenda tu kuchati huku moyo ukisononeka muda wangu unavyopotea
Mzazi wako ndio Mungu wako aliyekuumba msikilize .. nenda kanisani kijana
 
Inategemea na utamaduni wenu.
Mimi hapa nikienda kujitegemea naonekana muhuni, naonekana nafanya hivyo ili nipate uhuru wa wanaume.
Na sio kwamba sina kazi. Ninafanya kazi ila sina ajira.
kwani usitumie same logical framework ie critical thinking uliotumia kuwa aetheist pia kuhama kwenu bila kujali watu watakuonaje ama kukufikiriaje. Sababu ni maisha yako binafsi hakuna anayeyamiliki isipokuwa wewe. Uko just addicted na vya bure vya nyumbani una hofu kuanza maisha yako ya kujitegemea.
 
Reactions: Cyb
Siwezi kuishi nje ya uhalisia wangu.
 
Kma vp toka kma unaenda kanisani halafu njoo kwangu then mengine yatakuja
 
Nimezaliwa familia ya Dini(ukristo) ule wenyewe.. Baba Mchungaji Mama Mwinjilist (unaweza pata picha)

hakunaga shkamoo kwetu ni mwendo wa (bwana asifiwe kwa sana)

ila pamoja na kulelewa maisha hayo tangu utoto,someshwa seminary tangu Kindergaten sikuwahi Penda kwenda kanisani.

Yani sipendi nachukia mno lakini nilikua naenda ili kuonyesha utiifu kwa wazazi,na kweli naenda kwa kujivuta ila nikirudi nakua na amani flani.

Kipindi kama ulichopo wewe kilinikuta nikawa staki sikia kanisani kabisa, sisi home kanisani sio mpaka Jumapili tu (kama ilivyo kwako).

Lakini nilichokua nafanya nilikua natoka Home napita kona ya kwanza ya pili ya tatu Yuleee,Harakatini zangu!

Mida ya kutoka ikifika najirudsha home,nani ameniona siri ni yangu na moyo wangu.

Umesema ni mtu mkubwa wewe,sasa unagombanaje na mzazi kwa case nyepesi ivyo? unapungukiwa nn ukiwa unamridhisha utoke uende (then usiende unaenda mishe zako) kisha unarudi home mida ikifika?

Ninataka kusema nini unajua? Usigombane na mama mpe anachotaka aone.. Mrithishe (kwani hujui danganyia toto na wewe)

Usimkasirishe mama,nenda nae sawa... (sio lazima kwenda kweli kanisani) ila hakikisha unatoka home kila jumapili useme unaenda kansani.

NOTE:

Ukienda kanisani kuna ka raha unakapata japo ni jambo linahitaji uridhie kweli na moyo wako.

Binafsi hata mimi wanangu ntawaforce kwenda kanisani, Ukiwa mkubwa utaona na utajua umuhimu kwann mama alikua akikusisitiza kwenda kanisani. Sasa hivi huwezi elewa ila Sitoacha Mshukuru Mungu kwa kunipitisha kwa WAZAZI alioamua wawe baba na mama yangu.

Una MAMA mzuri sana,utagundua uzuri wake ukikua mkubwa.
 
Yaan namshangaa sanaaa huyu Taikon, nilikua namuona akili kubwa, ila ktk huu uzi ndo kajivua nguo zaid
Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa bali wapumbavu wanaikataa hekima.
"Sio kwamba ulimuona ana akili kubwa", Ni ukweli ana akili kubwa na mimi nimepata kujua sababu ya akili kubwa nayo ni kumjua Mungu aliyetuumba sisi.
Mungu niwa ajabu maana ametuumba na kutupa nafasi ya kuchagua hata ukiamua kutokukubali kwamba yupo yeye hajili maana amekupa uwezo huo. Zaidi ni ww mwenyewe kuangamia maana hutaweza kujitambua nje yake
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Doh shukran kwa kuniita bro ngoja nisome hapa nione nini kinaendelea.
 
Watu wenye ukafiri wa hali ya juu zaidi ni wale waliokanusha vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka mbinguni.
 
Hata unajua unacho kizungumza? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acha mambo ya ushauri wa kwenda kanisani. Nakushauri uhame kwa wazazi ukapambane mwenyewe. Hata saidia fundi kwa mama lishe.
 
mzazi huwa hakosei hata siku moja
Sio kweli, ndio maana wazungu mtoto akifikisha 18 tu yupo huru kuishi anavyotaka ila Africa bara la giza dadadek

Mchana husemezana na mchana
Usiku huutolea maarifa usiku wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…