Mzazi kumlazimisha mtoto wake kwenda kanisani ni sawa?

Nlisoma nikajua vingi, havikunisaidia kitu
 
sishauri kwa kufuata dini ila logic tu ya kawaida. usipoteze nguvu nyingi kupambana na mzazi kwenda kanisani. hiyo nguvu ipeleke kwenye kutafuta kazi ili upate means za kuanza kujitegemea mapema. nina dada yangu kwetu tupo wasichana tupu yeye naye alivyofika umri wa chuo akawa hapendi kwenda kanisani ila hakuwa atheist alitaka tu kwenda lutheran. tumeishi mda wote anatii ya wazazi ila kaja kupambana baada ya kumaliza chuo katafuta kazi akaanza kusave hela zake. siku kaomba kikao na wazazi akasema mimi naomba kwa sasa nihame nataka nianze maisha ya kujitegemea hapo anaongea hivyo ni mtu ambaye anatoa support pale nyumbani kwenye issue za pesa. wazazi walisikitika kiasi ila wakamwachilia akaenda. ni miaka 6 sasa tangu ameondoka anaishi kwake alikuja kuolewa hukohuko alikoenda ana familia. sie tuliobaki tukaja kuondoka nyumbani baada ya kuolewa. kwa hiyo mdogo wangu we pambana tu kiuchumi ujitegemee mapema until then....
 
Dah, hadi huruma[emoji26]
 
Asante, tatizo anataka tuwe wote ibadani.
 
Thanks
 
ishu sio mimi kuamini au kutoamini, huo ni uamuzi wangu binafsi kwasababu nimeshazidi 18 na nina uwezo wa kupambanua.

ishu ipo kwenye uhuru wa kuabudu. Kwanini tulazimishane?
Unazungumzia uhuru wakati wewe bado ni KULA BURE,KULALA BURE?Hama hapo nyumbani, jitegemee halafu fata msimamo wako.Tegemezi hana uhuru
 
Kabla ya huku mlihudhuria wapi?
Pengime hapa ndipo tatizo lilipo,amejikuta tu anahamishwa Makanisa kila kukicha na Mama yake.Ile foundation ya mwanzo kabisa imeshavurugwa.Sina uhakika kama Kanisa la Mwamposa lilikuwepo 20 yrs ago.
 
Sometimes muwe mnafatilia mambo kwanza b4 hamjafanya maamuz, je umesoma maandiko vizuri na ku correlate na maisha ya kila siku. Kama kweli Mungu asingekuepo wa2 wangeshapuuza zamani God is real na kama huamini endelea kupuuza, destruction is on your corner
 
Wewe dini yako inaruhusu kulazimisha mtu kuiamini?
Haujanielewa.You have an independent mind,contrally to what others believe.Good.Hautaweza kuishi huru kama Bado uko chin ya himaya ya mama.HAMA,JITEGEMEE.OTHERWISE,FUATA ANACHOTAKA MAMA MPAKA HAPO UTAKAPOJITEGEA.Nyumbani kwenu no himaya ya mama,si yako.Na Kila mtu ana haki kuweka Sheria na taratibu kwenye himaya yake.Hili ni swala la logic ndogo tu.Nashangaa kwanini hautaki kuielewa na unashikiria hiyo sentesi ya mama kulazimisha uamini anachoamini.Hata hivyo ni maisha Yako na huyo no mama Yako ,amua unachoona kitafaa.
 
Nlisoma nikajua vingi, havikunisaidia kitu
Eti "nikajua vingi". WakanaMungu bhana. Hujajua kitu kuhusu Uislam bado.

Halafu ndio utakuta mtu kama wewe anasema nimesoma dini zote hakuna kitu sijui. Jamani.

Nyinyi watu ni wajinga halafu mna kibri mno.
 
Mfundishe mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata pale atakapo kua mzee..Mama yuko sahihi
 
Ujue wacha Mungu wengi kwa kawaida na hasa wazazi hupenda kuona nyumnba nzima mkienda Kanisani kiusali, hivyo kama kuna mtu ndani ya nyumba hiyohiyo haendi kusali hujiona kama vile wanaishi na shetani na hivyo ndio maana Mama yako anaumia na kukwazika unapoonekana kutopenda kusali!
Pia kumbuka mzazi atabaki mzazi mpaka kufa kwako hivyo hata kama umejiona umeshaelimika usiwe mbishi kwake au kuwa mtu wa kupingana naye, utajibebea laana zisizo za lazima!
Kwavile bado upo chini yake kama jinsi alivokukumbusha basi endelea kumtii vinginevyo utamkatisha tamaa hata kukupambania katika mambo mbalimbali ili ufanikiwe kimaisha, usikute tangu uko chuo huwa anafunga kufanya sala na maombi kwa ajili hivyo ukimuonyesha kitu cha namna hiyo hakika utakuwa unamuumiza sana!
Bora nenda kanisani hata kwa kumfurahisha yeye tu ila usikaidi completely!
 
I respect your opinion
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…