Mzazi, mjengee mtoto wako mazingira ili aweze kukuheshimu

Mzazi, mjengee mtoto wako mazingira ili aweze kukuheshimu

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
23
Reaction score
59
Kwa WAZAZI NA WALEZI. Imekuwa ni kawaida kusikia wazazi na walezi wakilalamikia tabia ya watoto wao kukosa heshima. Wengi wanaona watoto wao wana jukumu la kuwaheshimu tu bila kuangalia upande wa pili yaan wajibu wa wazazi.

Natamani kukushirikisha haya ili kesho na kesho kutwa usiwe mzazi Lialia na ukaishia kutishia kutoa laana ambayo haitadhuru mtoto wako! Fuatana nami

Kutoka 20:12 " Waheshimu baba yako na mama yako, Siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana"

Pia Mathayo 15:4 "Kwa kuwa Mungu alisema; mheshimu baba yako na mama yako"

Waefeso 6:2 Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo ya Kwanza Yenye ahadi: Upate heri, Ukae siku nyingi katika dunia."

#Nukuu hizo tatu hapo juu, zinaonesha na kusisitiza umuhimu na ulazima wa watoto kuwa na heshima kwa wazazi wao.

Ilisemwa hivyo ktk agano la kale, Yesu pia alikazia na mitume walisisitiza!

Lakini suala la mtoto kumweshimu baba na mama yake wakati mwingine Ni mtambuka!

ANGALIA HAPA!

Neno "Waheshimu" katika tafsiri ya kiingereza (KJV) Limeandikwa "Honour" hii honour Ni zaidi ya heshima hii ya kiswahili. "Honour" ili ilete Maana haswa kusudiwa inajukuisha mambo matatu yaan Heshima (respect) kujivunia (Proud of) na kuamini ( trust) .

Kwa hiyo Ni muhimu kuwa na hizo dhana tatu zinazokamilisha neno "Waheshimu" yaan Kuheshimu, kujivunia na kuamini!

UKWELI ULIVYO

Nikiwa na kiu, usongo, hamu na ari ya kujua hali halisi ilivyo, niliandaa "Hojaji" yaan Questioneer Iliyolenga kujua kama watoto/Vijana wanawaheshimu wazazi wao kwa Kiwango Cha dhana hizo tatu.

MAJIBU NILIYOPATA

Asilimia kubwa ya Vijana Wenye UFAHAMU walisema wanadhani wanawaheshimu wazazi wao kwa Maana ile moja ya "Respect" Lakini upande wa kujivunia na kuamini ilikuwa story nyingine! Hata hivyo wapo wachache Sana walisema wanajivunia na kuwaamini Sana wazazi wao!

Waefeso 6:4 "Nanyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu: bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana"

Kumbe wapo wazazi wachokozi! Wazazi hawa huwapa jaribu watoto wao la kushindwa kuitimiza kikamilifu amri hiyo ya Mungu! Wanajitahidi Sana kuwaheshimu lakini suala la kujivunia na kuamini linakuwa gumu.

Mzazi Mchokozi? Ndivyo wapo wazazi wachokozi!
Hawa wanawafelisha sana watoto wao.

Watoto wanashindwa kuwaenzi, kujivunia na kuwaamini!

Mzazi bora anayo nafasi ya kumrahisishia mtoto wake kuitimiza kikamilifu amri hiyo!

#Mzazi usikubali kumpa mzigo mzito mtoto wako wa kulazimika KUKUHESHIMU kwa kujikaza kaza huku moyoni anaomboleza life style yako.

#Mzazi jiulize kwa maneno na matendo yako kwa watoto na jamii, Kuna uwezekano wa wao kujivunia maisha yako?

#Kwa kuwa huwajibiki kwa lolote kwa watoto na familia yako unadhani wasipojivunia uwepo wako Mungu atawaadhibu?

#Una sifa za kuwa baba/mama wa kuheshimiwa, kujivunia na kuaminiwa?

Mungu aliwahimiza watoto kuwa na heshima kwa wazazi, akitegemea kuwa wazazi hao watakuwa vilevile na viwango vya juu vya uadilidu, uwajibikaji na upendo. Kwani hayo yanachochea na kuchangia pakubwa ktk kuinua kiwango Cha heshima ya watoto kwa wazazi wao!

Usidai tu kuheshimiwa, Una wajibu wa kuifanya hiyo heshima uitamaniyo kuwa halisi kwa kuwa Mzazi bora!

KUNA WATOTO wanatamani sana kuwaheshimu wazazi kwa Kiwango kinachotakiwa, lakini Hawakupata bahati ya kuwa na wazazi wa aina hiyo! I'm sorry for that!

Wazazi Vijana amkeni. Wasaidieni watoto wenu kuitimiza amri hii muhimu ya Mungu.

Ukweli utatuweka huru

Tafakari na kuchukua hatua!

#ShetanianaogopaMtuanayejuakitu.
 
Back
Top Bottom