SoC02 Mzazi mlee mtoto kwa upendo kwa manufaa ya mtoto ya baadaye

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 9, 2022
Posts
3
Reaction score
3
Habarini ndugu watanzania wenzangu Mimi Ni binti wa miaka 25 kwa sasa Ni mama wawatoto wa 4 na hapo niliolewa na miaka 14 chanzo ninaandika kuuchungu mkubwa sana Tena sana.

Nilizaliwa wilaya ya hai mkoa wa Kilimanjaro na bw/bi festo na nimtoto wa pili katika familia ya watoto8 kiukweli familia ilikuwa duni ilihali baba alikuwepo Tena mwenye nguvu alitumia ubaba vibaya kwa kutumia bangi na alikuwa mkali kupita kiasi alikuwa mkorofi asiye pendwa na watu alikuwa mwizi alikuwa wakufuwngwA jela kila miaka huku akituacha na mama kiasi kwamba tulianza kufanya kazi tukiwa bado wadogo nakumbuka baba alifungwa uku akimuacha mama na mtoto wa siku moja.

Aliukumiwa miaka mitano jela uku tukibaki na mama pekee tulelewa na mama na upande wa Bibi wapimsaidia mama na baada ya miaka mitatu baba alitoka jela lakini Mambo hayakuwa kama tulivyotarajia alikuwa niyuleyule hakubadilika kabisa alikuwa nimpigaji kupita kiasi.

Dada yangu wakwanza alikuwa anasoma secondary lkn kutokana nakupigwa aliamua kuacha shule na kukimbia na alipo rejea qlikuja na mimba na HIV juu haikutosha kumbadilisha baba labda ajifunze apo alikuwa ana shika vibarua yani mashamba anajivunia anawatoto anachukua ela kulima tuna Lima sisi Tena unakuta unatoka asubuhi atakula ujala mpk jioni tulikuwa tukilima nusu eka Mimi na mdogo wangu ambaye Ni marehemu kwa sasa kwa siku mbili tuna maliza.

Maisha yaliendelea hivyohivyo mpk nikafika secondary nilipangiwa shule ya mbali sana akajitokeza msamaria mwema akanisaidia baiskeli ya kwendea lkn hiyo siku niliyo enda kuchukua baiskeli baba alinipiga na kuniambia kwa Nini nipokee na mwishowe alikuwa anitumia nikitaka kwenda shule niifate shamba asubuhi ndio niende shule Hali iliendelea ata wakati wa siku za shule alikuwa.

akitupeleka shamba au akisema tumfuate shamba hatukua hata namuda wakucheza na watoto wenzetu tulikomaa na kuwa na makovu kwa kupigwa sana Kuna siku ilikuwa juma mosi akasema tumfuate shamba lkn sisi tulikuwa tunanguo chafu tukaongea na mama tukamwambia sisi atuta enda shamba tutabaki nyumbani tufue mamaa akasema haya basi tukibaki tukifua maana kila siku shamba au shulempk juma pili muda wa kufua nimdogo lkn hiyo siku siwezi kuisahau baba alirudi jioni nakutuita jamani jaman nakumbuka alianzwa mdogo wangu Mimi nikiwa nasubiri kupigwa alimpiga teke alijigonga kwenye ukuta mama alikuwa pembeni alipiga kelele kwa kusikia kile kishindo na mdogo wangu alikimbia kwenda kwa Bibi mzaa mama maana siyo mbali kwa kugongezwa kule alipo fika anaulizwa shida Nini alijibu mama yangu anauliwa ikiwa Ni yeye alikuwa anapigwa.

Sitosahau hiyo siku mama alipiga yowe watu walijaa na kuna mama wakichaga alikuwa akimsemesha baba kwa kichaga nakumwambia watoto ni azina lkn alikimbia kuona watu wamejaa basi ile siku ukapita sijui waliongeaje na mama maisha yakaendelea nikashindwa kukaa nyumbani nilikuwa Nina akili shule ya msingi matokeo nilifaulia daraja B na hapo kuwa tulikuwa tunapitia magumu nilikuwa na shirikishwa kwenye maazimisho ya mtoto wa afrika kusoma risala.

Kwenye mabunge ya watoto na nilikuwa Nina ndoto zakuwa mwanasheria lkn yote yakawa Kama maji tu nilipo amua kutoroka na kuja mji wa Dar es Salam.

Kiukweli nilipitia magumu wazazi hususani ma baba mujue majukumu yenu hapo ndipo nilipo aribikiwa na kila kitu.

Basi nilikuja dar huku nikiwa Sina ndugu yeyote ninaye mjua nakumbuka nilishuka pale ubungo saa moja huku Nina njaa sijala toka asubh nilikaa kwenye bango ukunikiwa nasubiri uruma ya mungu tu watu walikuwa wakipita huku nakule wenye kupokelewa walipokelewa lkn kwangu ilikuwa mbaya mpaka.

Saa nne ndipo alikuja Dada mmoja akaniuliza unandugu una msubiri nikamjibu Sina ajaniambia umekuja kufanyaje huku nikamwambia kutafuta maisha alicheka na akaniambia inabidi nikupeleke polisi urudi kwenu ulipo toka wewe bado mdogo apo Nina miaka 14.

Nilikuomba sana asinipeleke polisi nikajaribu kumuambia alihalisi akanielewa mpk akatoa na machozi basi akanichukua tukaenda alikuwa mama ntilie wapale stend alikuwa akiishi tegeta tukaenda mpk kwakwe basi nilikaa kwake Kama mwezi huku nikimsaidia kazi ndipo siku akaja rafiki take akaniona akasema namtaka huyu mtoto akafanye kazi kwangu basi wakaongea akaniambia jioni jiandae utaondoka siwezi kukaa na wewe sana nimekupatia kazi kwakua nilikuwa Sina maamuzi ya utuuzima me nikakubali kwenda bila ya kujua Ni kazi gani basi nikaja kuchukulia na huyo Dada nikapelekwa kwenye baa moja iko bunju shule ilikuwa inaitwa Obama nikapelekwa Kama muudumu niliyo kutana nayo jmn 😓 jmn inauma kila nikikumbuka naumia sitaki ya mkute binti mwingine Tena yule Dada alikuwa ana patana na wanaume ananiambia nilale nao hukupesa anachukua yeye kiukweli nilipoteza usichana wangu pale bila chochote ndio nilipo Anza kumbuka nyumbani Tena Safari ya kudai kurudi nyumbn ikafika hapo nilifanya kazi kama mwezi nikapewa elfu hamsini nikaamua kurudi nyumbn Tena kwa zumuni nikasome lkn Mambo hayakuwa Kama nilivo tarajia nikirudi nyumbn mama alilia sana baba nae alikuwa niwakunilaumu nikaongea na mama.

Nikamwambia nataka kurudi shule mama alinipeleka mpk kwa mwalimu mkuu akamwambia Janet anataka kurudi apo niliacha Kama mwezi mwalimu alikubali nirudi Tena shule lkn shida ilikuja pale ambapo baba alikuwa akinisema Malaya wewe umerudi kufanya Nini.

Nilienda Malaya nikirudi Malaya kiukweli niliondoka Tena pale nyumbn nikarudi dar palepale kwakua nilikuwa nimesha pata marafiki nilikuwa na rafiki yangu anaitwa mage akaniambia njoo jeni kunakazi ya kuuza bar morogoro nakumbuka yule bosi alitum nauli tukaenda kuuza bar kule morogoro nilikaa Kama miezi miwili akili hainipi nataka nirudi Tena nikasome nilipo pokea mshahara nikaondoka nikarudi Tena nyumbn lkn Mambo yalikuwa niyaleyale
Nikaamua. Kuolewa Sasa nikapata mume mwenye watoto wawili jmn jmn mradi niondokane na shida za baba jmn ndio nilipo anzisha Safari ya kupata watoto wanne sasa Nina miaka 25 ninandoto zile zile zakusoma na kwakua muda umeenda nimeamua kusoma masomo ya sayansi kwa njiaa ya QT lkn nikwa ufupi sana changamoto za ndoa zilikuwa nyingi sana ilihali niliolewa na umri mdogo niliweza kuzivumilia na sasa Ni mwaka mwa kumi na moja Sasa japo kuwa nikipata mtu aliye nizidi umri pia yeye Kuna Mambo alinipitisha ya kuumiza sna kwakua niliwahi kufanya mambo yale ya kiutuuzima nilisumbuliwa sna na uzazi nilikaa miaka mitatu ndipo nikapata ujauzito nikiwa na miaka 17

Rai yangu kwa Wazazi walezi kwa ujumla mtoto niazina ya baadae Tena anakuja kukusaidia wewe mwenyew pale utakapo kuwa umri umeenda au umezeeka lkn kwa vipigo kuwakwamisha kielimu Tena Sasa ivi unakuta baba mzazi ana mbaka mwanae wa kumzaa jmn mtoto Ni faids kunawatu wanaishi kupitia watoto wao kuwajengea na kila kitu niwatoto wao.

Natamani katika Safari yangu ya kusoma na Mimi niwezeshe wasichana Kama Mimi wenye uhitaji Kama Mimi najua wengi wanandoto zao zilizokatishwa Kama Mimi na Wana taka kuziendeleza naimani munaweza rudini mashuleni Kama akili baro zipo ata kwa njiaa ya QT.

Serikali
Sirikali ninaiyomba iiangalie wilaya ya hai Tena kwa uchunguzi wa kimyakmy mabinti wengi hawasomi kutokana na sababu Kama zangu wanawake wanakimbia nyumba zao na kuwaacha watoto na baba zao huku watoto hao wakiishia kuzalishwa na umri mdogo naomba sana ninaushaidi wa watoto watatu wapo na mwingine ameenda kufanya kazi za ndani na mtoto mdogo wa miezi miwili huku yeye akiwa na miak16 tu

Serikali ninaombi la pili ifungue kwa upana shule za QT nyingi nchini ili wenye uhitaji Kama wangu wasome kwa gharama nafuu na pia wafungue walau vyuo vya ufundi japo wakushona kwenye wilaya yetu mafunzo yawe Ni bure ilikusaodia mabinti wa wilaya ya hai.

Kwa sasa nimerudi shule ninasoma QT Niko chanika taliani na baada ya miaka kumi maendeleo yangu nimazuri japo kuwa nimama Sasa Ila kinacho nisumbua ni ada ninaomba Kira zenu jmn kwa atakae Soma ukurasa wangu na pia hapa nyumbn Niko na watoto wakike wanne wa wifi yangu ambao story yangu na yao hazijapishana na wao pia niwahanga wa malezi.

Mungu awabariki sana

Q

ll
 
Upvote 2
Lengo lako la kusoma ni lipi? Kupata kazi, kutimiza kiu yako, kuiondoa ile inferiority complex.
Kujikwamua maisha sio lazima usome.
 
Niliwahi kumhurumia msichana mmoja aliyekuwa na changamoto kama zako. Nilimpeleka sekondari asome afikie ndoto zake.

Badala ya kusoma alienda kuolewa na mwanafunzi mwenzie. Hakujali gharama za chumba nilichompangia, hela ya matumizi kila alipohitaji na kila alichohitaji nilimpa.

Nilikuja kugundua anamaliza shule. Alifeli mtihani wa kidato cha nne kwa kupata zero kabisa.

Nilimfukuza kwa kumrudisha kwao akaendelee na ukahaba wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…