kiredio Jr
JF-Expert Member
- Jul 8, 2024
- 989
- 1,843
- Thread starter
-
- #41
Nitamchukua tu, ni swala la mudaBasi mbebe mwanao uje kumsomesha Dar. Kule kijijini atakabidhiwa mikoba ya kichawi πππ
Hata wazazi wa mzazi mwenzangu wanatamani mjukuu wao asome shule nzuri, tatzo ni mama yake....Ndio watoe huko wapangie sehemu na umsomeshe mtoto wako kwa uhuru ila kumchukua mtoto wa miaka 3 kutoka kwa mama yake bila sababu za msingi hata sheria zinagoma tena kwa mazingira ya siku hizi haya..
Alafu muulize mama yako kama na yeye angefanyiwa hivyo angekubali kukutoa wewe ukiwa na miaka 3?
Za kuambiwa changanya na zako.
Makosa yanaanzia hapo. Hutaki aishi na baba mwingine kwanini hukumwoa huyo mwanamke na kama ulimwoa kwanini umevunja ndoa. Simply unachotaka kufanya ni kujimwambafai kuwa wewe ni kidume ila ina madhara kwa mtoto.Walikuja dar, wakaishi Vizuri na familia yangu, mtoto alikuwa na furaha sana, hata sasa mama yake anasema anasumbu sana anamtaka baba yake, kiufupi alizoea maisha ya huku na kuwa huru zaidi.
Sitaki au sitopenda akiishi na Baba mwingine
Nilipanga kumuona hata wazazi wake niliwaambia hilo, lakini alifanya mambo ya ajabu ambayo hata ingekuwa ni wewe usingekubali kuoa mwanamke wa aina hiyo.Makosa yanaanzia hapo. Hutaki aishi na baba mwingine kwanini hukumwoa huyo mwanamke na kama ulimwoa kwanini umevunja ndoa. Simply unachotaka kufanya ni kujimwambafai kuwa wewe ni kidume ila ina madhara kwa mtoto.
Unanijua vzr? Au unaota kwamba unanijua?mbabaishaj hyo hana hata hiyo ada π namjua vzr π π€£
Sababu yoyote ile ya kumfanya mzazi mwenzako kuwa jeuri wakati huu, ujeuri huo kukuathiri wewe leo kosa ni lako.Hujuia yamefikaje hapo, hujui nini sababu ya mzazi mwenzangu kuwa na jeuri wakati huu...
Hakuna kuyakayaga wala nini, maisha yanaendelea kama kawaida
Sio kulialia tu, hata nikitaka kupiga mayowe uhuru huo ninao, nimeandika kama wengine wanavyo andika...Kama maisha yanaendelea kama kawaida, kwa nini unakuja kulialia hapa?
Unaikosea Sana serikali yako mkuuMimi naamini serikali hakuna elimu bora.
Naikosea kwa kukiri kwamba Elimu yao magumashi, wao wanatukosea mangapi? Tukisema tunakosewa nani anatutetea?Unaikosea Sana serikali yako mkuu
Jazba ni sehemu ya binadamu, tunakasirika pia tunafurahi, tunahuzunika pia tunafarijika.Umeandika kwa jazba Sana mkuuπ€
Nani amesema hawezi kulea?Mnazaa hovyo kama simbilisi halafu kulea hamuwezi, shenztype.
Kwanini unamiini kuwa akija Dar tu ndio atasoma shule bora?. Mfano hata kama kijijini hakuna shule hiyo bora, kwanini usimlipie aende akasome kwa ndugu yake yeyote mkoa wowote hata hapa Dar kama ana ndugu, halafu wewe umlipie hiyo shule bora?Hatuna tena mahusiano, kila mtu anafanya mambo yake lakini bado huduma natoa, na shule ni jukumu langu ila kama akikataa atamsomesha yeye.
Sasa hiyo ni shida mkuu? Hakuna ndugu yake anayeweza kukaa na mtoto, mimi pia sio kama nataka kukaa naye, ila akae na Bibi yake then asome shule nzuri.Wewe inaonekana pia una shida, unataka kumchukua mtoto kwa gia ya kumsomesha shule bora.
Mimi ndyo nalipaMlipa School fee ndo anaamua, Nani analipa?
Mimi ndyo nalipa
Kauli yangu ni kwamba wakimpeleka shule wanayotaka wao, gharama zitakuwa juu yao.We ndo una amua, ukiendekeza ujinga Kama huu utakuja teseka sana baadae, toa kauli, cha maana aiumizi mtu, kataa mijadala!
KAma una malengo ya mtoto uyo asome shule nzuri (Bus la njano) basi tuma ada ataftiwe za huko sio mpka aje DarHabarini ndugu
Mimi na mzazi mwenzangu bado hatuna ndoa, ila tumebahatika kupata mtoto mmoja, kwa sasa wamerudi mkoani baada ya kuja na kukaa nyumbani kwetu kwa lengo la kumleta mtoto familia yangu imtambue.
Baada ya mtoto kufikisha miaka mitatu na nusu, nikamwambia mama yake itabidi mtoto aanze shule, na natamani mwanangu arudi Dar asome shule nzuri na ya kisasa.
Mzazi mwenzangu anadai hawezi kuruhusu hilo, ni afadhali mtoto abaki kijijini asome shule za kawaida (serikali). Nikamwambia utamsomesha wewe huko, mimi nilitaka aje Dar asome shule nzuri na tofauti na hapo sitahusika na maswala ya shule endapo atasoma tofauti na nilivyotaka.
Nadhani labda bado anachuki au kinyongo dhidi ya familia yangu, lakini hajui Elimu bora ina faida kwa mtoto na maisha yake ya baadaye, sio mimi wala yeye.
Je ni sahihi nikikataa kutoa huduma za shule endapo atasoma kijijini? Kwani lengo langu lilikuwa aje asome Dar, akae na Bibi yake (Mama yangu) na yupo tayari kwa hilo.
pia soma: Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara