Mzazi mwenzangu hataki mtoto apate Elimu nzuri, nadhani hajui elimu ni kwa faida ya mtoto sio mimi wala yeye

Kugharamika sio tatizo, ila Urithi wa Elimu ni bora kuliko urithi wa nyumba na magari.
Sisi masikini ndio tunaosema urithi wa elimu ni bora zaidi; ila viongozi na matajri wanawarithisha mali na vyeo.
 
Mhamishe mama na mtoto....umri wa mtoto ni wa kukaa na mama mzazi
Umri wa mtoto ni wakuanza shule, na mimi kama Baba hilo ni jukumu langu, na pendekezo langu ni Nursery.
 
Tunapo wambia kuzaa na kuacha ni shida kubea huwa hamuelewi.

Kijana unajiona una hela unapiga huku. na huko unazaa hovyo unatelekeza unajifanya unampenda mtoto
 
Kweli kabisa serikalini hakuna elimu bora. Kama ipo basi tungewaona watoto wa Mawaziri wakisoma shule hizo. Tusijizime data kuhusu ubovu wa elimu katika shule za msingi za Serikali.
Huo ni ukweli ambao wengi hawataki kuusikia, Elimu bora ni gharama.
 
Tunapo wambia kuzaa na kuacha ni shida kubea huwa hamuelewi.

Kijana unajiona una hela unapiga huku. na huko unazaa hovyo unatelekeza unajifanya unampenda mtoto
Hakuna aliye tekelezwa, kama ni huyo Mama mtoto, basi alijitelekeza mwenyewe kwa matakwa yake.
 
Hakuna aliye tekelezwa, kama ni huyo Mama mtoto, basi alijitelekeza mwenyewe kwa matakwa yake.
Sawa......lakini ulipozaa naye alikuwa Pisi kali ila sasa hivi??

Mkuu sio kwamba nakusakama hapana. Nataka na vijana wengine wasirudie makosa tuloyofanya mimi na wewe. I hope you take it postive.
 
Nadhani baba wa mtoto yuko sahihi sana na ana maono ya mbali sana, lakini pia hata na wewe sio kwamba una maoni mabaya, nawe pia uko sahihi tu.

kupanga ni kuchagua. Mnaweza kukubaliana shule ya msingi akasoma huko kijijini na sekondari au chuo akasoma mjini. Japo elimu na shule nzuri ziko mahali kote Tanzania..

hivi sasa elimu imeimarika sana kuanzia vijijini huko ndrani ndrani kabisaa. watoto wanasoma vizuri na wanafaulu vizuri sana.

hakuna sababu hata moja ya kupambana kwenye hilo, akishaandikishwa shule tu inatosha na sehemu ya gharama za kumuhudumia mtoto inabebwa na serikali na sehemu nyingine kidogo hakuna mlezi au mzazi ana weza kushindwa kumuhudumia.

Ni muhimu sana kama wazazi kuepuka kumuadhibu mtoto kulingana na tofauti zenu. Kila moja awajibike kwa nafasi yake kadiri ya Neema na Baraka za Mungu, kijana asome kwa uhakika na amani na hapo mtakua mmemtendea haki kijana wenu.

Vinginevyo,
niwapongeze sana kwa namna ambavyo mmeonyesha umuhimu wa elimu kwa mtoto wenu licha ya kutofautiana mawazo na mtazamo ya kwamba akasome wapi..🐒

God bless you wazazi
 
Mimi mtoto wangu sijui atakuwa tajiri au maskini, lakini naogopa baade akinilaumu kwamba nimeshindwa kumpa Elimu bora.
Kabla ya kumpa elimu ya gharama kubwa, hakikisha kwa upande wako umeshajikomboa kiuchumi. Yaani unavitegea uchumi vinavyoeleweka.​
 
Sawa......lakini ulipozaa naye alikuwa Pisi kali ila sasa hivi??

Mkuu sio kwamba nakusakama hapana. Nataka na vijana wengine wasirudie makosa tuloyofanya mimi na wewe. I hope you take it postive.
Mkuu matendo ya huyu binti ndyo sababu ya kutengana naye, sio kama nilimtelekeza bila sababu.
 
Nitambomoa mimi au mama yake? Akimpeleka kwa Baba mwingine ndyo atajenga au kubomoa?

Mimi nataka nimuokoe mtoto, aishi vizuri na kwa amani, asome vizuri na kwa usahihi.
Sio wewe wala sio mama yake. Kisaikolojia mtoto akiwa mdogo inashauriwa akae na mzazi wa kike. Nenda ustawi wa jamii uombe ushauri
 
Umesema vyema mkuu, kweli elimu bora ni muhimu kwa malengo ya baadaye, na naamini hatuwezi fikia pabaya kama wazazi, tutapata suluhisho juu ya hili, na mwisho mtoto lazima asome shule nzuri.
 
Kabla ya kumpa elimu ya gharama kubwa, hakikisha kwa upande wako umeshajikomboa kiuchumi. Yaani unavitegea uchumi vinavyoeleweka.​
Mpaka nimeweka nia ya kumpeleka shule, means najua gharama nitazikabili vipi.
 
Sio wewe wala sio mama yake. Kisaikolojia mtoto akiwa mdogo inashauriwa akae na mzazi wa kike. Nenda ustawi wa jamii uombe ushauri
Nafahamu hilo, lakini naamini busara binafsi za pande zote mbili zinaweza kutoa suluhisho katika hili.
 
Oya wee, we unazingua, aliekwambia elimu nzuri inapatikanai Daslam ni nani???? Mtoto huyo bado mdogo anahitaji uwepo WA mama, Sasa kwanini umlete akae na bibi wakati mama Yuko hai???? Embu toa pesa mtoto akasome, elimu nzuri elimu nzuri, elimu nzuri Iko Kila pahala ni vile tu watoa elimu wanavyoitoa. Funguka weqe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…