Mzazi Mwenzangu kamtelekeza mtoto wangu

Mzazi Mwenzangu kamtelekeza mtoto wangu

Mzee Kimamingo

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2024
Posts
1,861
Reaction score
4,462
Habarini wana Jamvi.

Mwaka 2022 nikiwa site za barabara huko Malinyi ndani ndani mkoani morogoro ilitokea Nikazaa na Binti mmoja wa kisukuma (Alikuwa na Mzigo balaa) ili hali nina mke na mtoto ilikuwa ni ajali kazini.

Nahudumia mtoto ina Bima hii mbovu mbovu ya NHIF nimemkatia ila katikati apa nikawa simpati kumbe bana katoroka na mtoto kamuacha kwa bibi yake Yeye kaenda kuolewa kusikojulikana.

Leo Asubuhi Mtendaji wa kile kijiji kanitumia msg kwakuwa alikuwa Mshkaji wangu nanukuu "Eng mtoto wako anaishi kama Chokoraa muda mwingi anashinda mtaani akiranda randa fanya juu chini umchukue" kiukwel roho imeniuma na Home wife hajui huu msala naumalizaje.

Waliopitia hii Changamoto mlitokaje?
 
inauma,,ila naamini adi umeoa huyo mwanamke uliona anafaa kwa asilimia kubwa,, mwambie tu ukweli then angalia mapokeo yake omba msamaha,,kisha beba mtoto wako peleka nyumbani.
Oya ataaribu. Kwa sasa tuongelee kwanz kusolve tatizo la dogo.
 
apo mwanaume anaeenda kuoa mwanamke aliyeweza kutelekeza mtoto wake mwenyewe hajiulizi kwel!!??,, watoto sio wa kutelekeza aseee nenda kale nae utachokula wewe.
Kwani walioana? Si amesema aliteleza na sasa ameteleza mpka kwa kiumbe kisicho na hatia!
 
Back
Top Bottom