Mhafidhina07
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 3,340
- 4,659
Mtoto ni baraka kutoka kwa muumbaji wa hii dunia, ni furaha ya wazazi pamoja jamii kwa ujumla uwepo wa mtoto inaonekana ni nuru na baraka kwa kuwa ni kiliwazo kwa wazazi na inatarajiwa kuongezeka kwa maarifa na nguvu katika familia, jamii au taifa kwa ujumla.
Katika jamii za kale kuna tamaduni ya kupewa utambulisho wa mtoto/jina ambalo litaweza kumtofautisha na watu wengine, utambulisho mara nyingi hubeba maana na nadharia nyingi kwa mtoaji mfano Historia ya afrika au familia ilikuwa inapatikana katika majina ya watu kuna watu wanaitwa Masumbuko, Kesi, Mwinyi na Kinjitikile n.k yote ni kuilinda kumbukumbu ya wakati huo mzazi alikuwa nayo.
Wapo waliotumia majina ya mitume Mfano Musa, David, Paulo, Ibrahimu na wengine ili kukipa kizazi chake sifa ya utukufu kwa mtoto huyo.
Ila kwa sasa sijajua kwamba labda kuna maendeleo makubwa hivyo hakuna ulazima wa kuhifadhi historia tutatumia kompyuta tu au ndiyo utandawazi kumekuwa na majina mengi ya ukopaji na wazazi wanatoa majina kwa raha ya kuyatamka au kuna nini cha zaidi?