Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Sasa humu umekuja kutafuta nini si umuulize huyo mama yako akuambie tatizo la huyo mwanamke ni nini.? Sisi tutajuaje?
Mimi nimeuliza je ni sahihi nikimwambia huyu binti kwamba haiwezekani kuwa na ndoa, hilo ndilo swali langu
 
Naelewa majukumu yote ni yangu katika kufanya maamuzi, lakini still bado nahitaji kujifunza na kupata ushauri kuhusu mambo haya kwani mimi bado ni kijana ambaye sina experience na mambo ya Ndoa
Jifunze kumaliza matatizo yako (hasa ya kindoa) ndani ya familia yako.

Usije ukathubutu kuoa mke kwa kigezo cha kuwa eti anapendwa na kukubalika na mama au ndugu.....hell no! Priority namba moja ni wewe na nafsi yako~kumbuka wewe ndiye utakayeishi naye "milele" kwa kiapo cha ndoa.

Usioe mwanamke kwasababu unamuonea huruma. Nafsi yako iridhie haswaaa kuwa huyu ananifaa
 
Mama boy kipeuo cha pili wewe!
Kwa hiyo mama yako unamruhusu amkwaze binti wa watu sababu hajamzaa?
Kwa hiyo akikushauri umuache binti wa watu na umemzalisha utakubali?
Mbona alishindwa kukushauri usivae kondomu au umwage nje?

Familia uliyoianzisha mwenyewe ni muhimu kuliko familia uliyotoka.
Brother, mimi bado nipo home na ni mwanafunzi pia.. hata swala la ndoa ni baadae sana, nahisi labda Mzazi wangu ameona huyu binti hawezi kuvumilia mpaka nihitimu masomo
 
Jifunze kumaliza matatizo yako (hasa ya kindoa) ndani ya familia yako.

Usije ukathubutu kuoa mke kwa kigezo cha kuwa eti anapendwa na kukubalika na mama au ndugu.....hell no! Priority namba moja ni wewe na nafsi yako~kumbuka wewe ndiye utakayeishi naye "milele" kwa kiapo cha ndoa.

Usioe mwanamke kwasababu unamuonea huruma. Nafsi yako iridhie haswaaa kuwa huyu ananifaa
Nimekuelewa Brother, lakini bado napaswa kujifunza kutoka kwa wengine, najua maamuzi ya mwisho ni yangu na mimi ndyo nitakaye amua Masika au nanyoa
 
Brother, mimi bado nipo home na ni mwanafunzi pia.. hata swala la ndoa ni baadae sana, nahisi labda Mzazi wangu ameona huyu binti hawezi kuvumilia mpaka nihitimu masomo
Kwahiyo unamaanisha huyo binti umemleta hapo nyumbani unapoishi wewe na mama yako?
 
Brother, mimi bado nipo home na ni mwanafunzi pia.. hata swala la ndoa ni baadae sana, nahisi labda Mzazi wangu ameona huyu binti hawezi kuvumilia mpaka nihitimu masomo
Mwanafunzi isiwe kichaka cha kujificha. Mbona umeweza kumtongoza demu ukamgonga na kumpa mimba na kupata nae mtoto? Kwani una miacha chini ya 18?

Achana na kujishikiza kwa mama vinginevyo kama hujawa tayari usiwazalishe mabinti wa watu hadi fikra zako ziwe pevu
 
Kwahiyo unamaanisha huyo binti umemleta hapo nyumbani unapoishi wewe na mama yako?
Binti ametokea kwao, amekuja nyumbani kwetu yaani kwa mama yangu ila mimi naishi mwenyewe geto, mbali na nyumbani
 
Mwanafunzi isiwe kichaka cha kujificha. Mbona umeweza kumtongoza demu ukamgonga na kumpa mimba na kupata nae mtoto? Kwani una miacha chini ya 18?

Achana na kujishikiza kwa mama vinginevyo kama hujawa tayari usiwazalishe mabinti wa watu hadi fikra zako ziwe pevu
Tayari nimepata mtoto na siku hazirudi nyuma, pia ni kweli mimi ni mwanafunzi wa chuo mwaka wa pili sasa
 
Binti ametokea kwao, amekuja nyumbani kwetu yaani kwa mama yangu ila mimi naishi mwenyewe geto, mbali na nyumbani
Huyo binti ungemleta kwa mama kabla hujazaa nae ungekua umefanya la maana sana. Ona sasa unaenda kuongeza idadi ya singo mazaz na watoto wasio na malezi.
 
Sio kwamba yeye ndyo afanye maamuzi, ila nataka aniambie ni sababu gani ambazo zinafanya asimkubali huyu binti
mke anaishi na wewe unaporuhusu mama yako akuchagulie mke elewa utakuwa huoi kwa ajili ya mama au jamaa zako.
 
Mimi sipo tayari kumkwaza Mama yangu, japo mimi ndyo nina maamuzi ya mwisho lakini ni lazima nisikilize ushauri wake
Mkuu, fuata anachokisema na kukushauri mama yako. Hawezi kukutakia mabaya. Ingawa ni vyema kumuuliza mama yako ikiwa hajatamka na huyohuyo atakupa njia ya kumwambia huyo mwanamke uliyezaa nae.

Usiogope kuitwa mama's boi kwenye hilo.
 
Huwezi kunijaza ujinga uliojazwa nao ukakujaa.

Yaani unaambiwa "kitanda hakizai haramu" na wewe unaingia kichwa kichwa kama vile uliwahi kuona kinazaa.

Ficheni ujinga wenu japo kidogo.
Sawa shangazi nimekusoma, lakini tayari mtoto ni wangu na hakuna haja ya kulaumu au kuitana wajinga
 
Mkuu, fuata anachokisema na kukushauri mama yako. Hawezi kukutakia mabaya. Ingawa ni vyema kumuuliza mama yako ikiwa hajatamka na huyohuyo atakupa njia ya kumwambia huyo mwanamke uliyezaa nae.

Usiogope kuitwa mama's boi kwenye hilo.
Nimekupata mkuu, kweli kabisa mzazi hawezi kunitakia mabaya au kuona nakosea na akakaa kimya. Ila nitamuuliza ni sababu zipi zimefanya awe na mawazo au maono hayo kuhusu huyo binti
 
Back
Top Bottom