Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Mama kama mama akikaa na mkwe zaidi a mwezi ni kosa lazima atatoa kasoro usizo ziona wewe kwa hiyo maamuzi yapo kwako na wewe kuona hizo kasoro au kuzifumbia macho mambo yakawa mbele kwa mbele
Nitamuuliza ni kasoro gani ameziona na kisha nitafanya maamuzi
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Maoni ya wazazi ni muhimu katika hilo. Ila tambua ya kwamba wewe ndie unae kwenda kuishi nae na sio mzazi wako. Jiridhishe na moyo wako kwamba kweli unampenda na utaenda kujenga naye familia, hiyo inatosha kabisa.
 
Huyo binti ungemleta kwa mama kabla hujazaa nae ungekua umefanya la maana sana. Ona sasa unaenda kuongeza idadi ya singo mazaz na watoto wasio na malezi.
Mzazi wangu ndyo alitaka aje ili amuone mjukuu wake
 
Mzingatie mtoto na huyo binti kama umeamua kumpiga chini....piga chini mapema ajue kama ataenda dar au abaki Kijijini
Kwa sasa yupo dar, kwao ni kijijini, ila nataka niongee na Bimkubwa then nifanye maamuzi ya mwisho
 
Lakini pamoja na hayo wewe kwanza umebesha mimba amezaa ndo unaenda kutambulisha kwenu sasa huyo ni mchumba au mkeo bado ndoa tu 😂😂😂😂😂
Amekuja hom kwa lengo la kumleta mtoto bibi yake amuone na si vinginevyo
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Ongea na mama uso kwa uso. Mwambie nia yako kwa huyo mzazi mwenzio, then msikilize anamaoni gani baada ya kukaa nae kwa muda huo. Hakuna mkamilifu, labda usio kabisa
 
Kwa hiyo ukampeleka mdada wa watu miezi akae na mama Yako agundue Nini? Unaoa wewe au mama Yako, akili Yako haitoshi mpaka utumie ya mama Yako, hebu tutolee utoto wa mama hapa be a man, ni Nini unataka eti nimegundua mama kaona Kuna kitu hakipo sawa muone kwanza hovyoooo
 
Unaoa kwaajili ya mama ako au kwaajili yko?
 
Naomba uniruhusu nikukebehi kidogo tu mkuu hivi hivi sitaridhika naweza kukosa usingizi nikikuacha mkuu
 
tutolee utoto wa mama hapa be a man, ni Nini unataka eti nimegundua mama kaona Kuna kitu hakipo sawa muone kwanza hovyoooo
Sasa maneno yote hayo ya kejeli ya nini? Kama umekuja kwa lengo la kutoa ushauri fanya hivyo sio kuporomosha unnecessary drama
 
Amekuja hom kwa lengo la kumleta mtoto bibi yake amuone na si vinginevyo
Mimi naona kama wewe ndio humtaki huyo binti baada ya kuwa umemzalisha. Hapa unachofanya ni kutafuta kisingizio cha kumpiga chini.
 
tutolee utoto wa mama hapa be a man, ni Nini unataka eti nimegundua mama kaona Kuna kitu hakipo sawa muone kwanza hovyoooo
Sasa maneno yote hayo ya kejeli ya nini? Kama umekuja kwa lengo la kutoa ushauri fanya hivyo sio kuporomosha unnecessary drama
 
Kwa sababu unamuolea mamako, endelea kutafuta mpaka upate atakayemuelewa.
 
Back
Top Bottom