Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Pole,Imani yetu Kwa mama zetu ni kubwa sana na Kwa heshima tuliyowapa Huwa tuna Imani kuwa wapo sahihi Kwa Kila watuambiacho bila kukumbuka kuwa nao ni binadamu pia,wana mapungufu Yao.
Sahihi kabisa, nao wana mapungufu yao lakini hawawezi kuruhusu kuona watoto wao wanapotea au kuingia katika matatizo
 
Sijamaanisha upuuzie ndo maana nikasema maisha ni ya kwako.

Mapenzi hayanaga mwalimu.
Kweli hayana mwalimu, sijahitaji kufundishwa au kuelekezwa namna ya kuwa na mwenza, ila nahitaji kujua ni sababu gani mpaka mzazi wangu abadili mtizamo wake juu ya binti huyu
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Unafurahisha kijana,mama ndio anayeoa na kuishi huyo mwanamke au wewe,chagua mwanamke unae weza kuishi nae wewe sio mama yako,mama walichaguana na baba yako.Utapishana na gari la mshahara kwa kutaka kuridhisha watu.Hata mm nilipotaka kuoa mama alipinga mambo ya kabila ila mm ndio naoa sio mama mpaka sasa tuna miaka kumi ya furaha na amani tele na watoto watatu na sijawahi kujuta kumuona mke wangu hata nikirudia ujana nitamtafuta yeye tena nani marafiki sn na mama.
 
Samahani ila ndio ukweli halisi.

Wewe ni mama boy una mtoto unatarajia kuoa na kuwa na familia ila bado upo attached/umejishikiza kwa mama yako mzazi sababu amekuzaa.

Umefanya ujinga na umeruhusu mama yako amchoke mzazi mwenzako. Sikiliza ndugu, mama yako anampimia binti wa watu kwa kipimo ambacho sicho!!

By the way, huo ni utamu wako na amekuzawadia mtoto huhitaji kupata validation kutoka kwa mama yako.

Funga ndoa, oa na chukua mke wako na mtoto wako mkaishi kivyenu achana na mama yako ni chakula cha baba yako tu asivuke mipaka.

Sorry kama nimetumia lugha Kali mimi ni mubaba wa kunyoosha.
Katika makosa usijefanya ni kuishi na familia ambayo mama mwenye nyumba anakuchukia
 
Unafurahisha kijana,mama ndio anayeoa na kuishi huyo mwanamke au wewe,chagua mwanamke unae weza kuishi nae wewe sio mama yako,mama walichaguana na baba yako.
Mama yangu hajanichagulia ila mimi ndyo nilichagua, kwa sasa nimeona hana imani naye na nataka nijue sababu ni nini, bado sijafanya maamuzi na still bado nina nia ya kuishi na mzazi mwenzangu.
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
 
Mda wa kutumia akili zako hiz. Mzazi kamaliza yake. Achana ana habar za wazazi mtu anabadilika. Alafu shika maneno yangu haya. KUISHI NDANI YA NDOA NI KUREKEBISHANA KILA MTU MBOVU MNAREKEBISHANA HATA KUFA KWENU KIPI SAHIHI NA KIPO SIO SAHIHI. HAMNA ALIYE PERFECT.
 
Sina mpango wa ndoa kwa sasa, ila lazima nipate maoni kutoka kwa mzazi wangu
 
Muacheni mtto wa watu, hata ukimuoa wewe na mamako mtamtesa sana!
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Nimegundua mzazi wangu hana imani naye tena na sijui ni kwanini, nitamuuliza anipe sababu za kubadili mawazo yake ya awali.

Naombeni ushauri wenu juu ya hili bila kejeli na maneno mabaya
Asanteni.....
Wewe bado ni mvulana, siku ukiwa mwanaume utaongozwa na kichwa chako na sio mawazo ya mtu.
 
Back
Top Bottom