Mzazi wangu hajaridhika na mchumba wangu, hajasema lakini nimeona ishara

Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Kama humtaki mke wako nenda kalale na mama yako, kua mwanaume kama baba yako naacha kushikiwa akili na mama yako
 
Naelewa majukumu yote ni yangu katika kufanya maamuzi, lakini still bado nahitaji kujifunza na kupata ushauri kuhusu mambo haya kwani mimi bado ni kijana ambaye sina experience na mambo ya Ndoa
Kama huna experience na mambo ya ndoa kwanini hukumuuliza mama yako kuhusu kumkojolea huyo binti ndani. hebu acha kutuaibisha wanaume
 
Wewe ndyo unajiaibisha kwa kutukana na kukebehi wazazi wa wenzio
 
Habarini ndugu

Baada ya kupata mtoto, ilibidi mzazi mwenzangu aje nyumbani kwetu kumleta mtoto Bibi yake amuone kwani alikuwa na shauku ya kumuona mjukuu wake.

Walikaa kwa kipindi cha miezi kadhaa, na walikaa kwa furaha na amani. Mama yangu alifurahi kwani mwanzo aliona na kusifia tabia nzuri na kujituma kwa binti yule.

Kadri siku zilivyokuwa zinasonga, nikahisi kuna jambo halipo sawa, kila nikiongea na Mama kuhusu mipango ya baadae alikuwa haonyeshi dalili za kubashiri ndoa yangu na binti yule. Nikajua tu hajaridhika nae.

Lakini naamini Mzazi wangu ananijua vizuri na anajua ni kipi kitanifaa na kuendana na mimi, nahisi kuna vitu amegundua kwa binti yule kwa muda aliokaa nae.

Mimi sina tatizo na mawazo na ushauri wa Mzazi wangu, lakini najiuliza je ni sahihi kuendelea kumuaminisha binti huyu kwamba nitamuoa ilihali najua Mzazi wangu hajaridhika nae?

Najiuliza nimwambie mapema kwamba haitowezekana kufunga ndoa hapo badae? Naogopa kumpa maumivu na kumfanya akose amani.......

Ni uamuzi gani wa busara napaswa kufanya wadau? Naombeni ushauri wenu bila kebehi na masihara..

Asanteni.....
Kama ulimuamulia mama yako kuolewa au kuzalishwa na baba yako, basi haina shida, mruhusu mama yako akuchagulie mke.
 
Hilo swali sidhani kama lina mantiki yoyote, kwani wewe hujui nini kinafanya watu wazae?
Hili swali linamaana kubwa sema umechukulia wepesi labda kwasababu tunatofautiana kwenye upeo we ni jibu alafu nitapata mwanga ujue kwanini nimekuuliza
 
Hizo ni koo mbili tofauti. Simba huwa hatuna matatizo hayo, tunaoana simba kwa simba au na marafiki wa koo za simba.

Nje ya hapo hata kuzaa nae hatuwezi, ni kifo wote kasoro simba tu.

Na simba utatengwa kwa muda mrefu, wansema ni mpaka harufu za kishenzi zikutoke. Hapo ni mpaka ukagfanyiwe matambiko na kuoshwa kimila za kisimba. Unafanyiwa nyungu na singi za nguvu kwa siku 40 bila kuwacha hata siku moja, ukiwacha siku moja inaanza tena upya. Ukiwacha mara tatu, na wewe unauliwa.
 
Hili swali linamaana kubwa sema umechukulia wepesi labda kwasababu tunatofautiana kwenye upeo we ni jibu alafu nitapata mwanga ujue kwanini nimekuuliza
Kilichofanya nizae nae siwezi kusema ni kitu gani, ila tulikutana na baada ya hapo nikapewa taarifa za ujauzito, nikazipokea na mambo mengine kuendelea
 
Back
Top Bottom