Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Wakuu, nimewaza sana kuhusu malezi ya watoto leo. Wazazi tunapaswa kujua mabadiliko ya tabia za watoto yanategemea zaidi ukaribu walionao kwa Mzazi au Mlezi wao na kwa kiasi gani Wazazi wanazungumza kuhusu makuzi, fursa, hatari zilizo mbele yao na jinsi ya kuzikabili au kuziepuka.
Watoto wengi wanajikuta kwenye mazingira hatari ya kudhurika Kiakili, Kisaikoloji au Kimwili kwasababu hawana watu wa kuzungumza nao mambo yao kutokana na baadhi ya Wazazi kutokuwa na utaratibu wa kuwasikiliza Watoto.
Kama unatamani au kutarajia makubwa kwa Mwanao, basi ukiwa kama mzazi kuwa na utaratibu wa kuzungumza na kuwapa nafasi Watoto kusema vitu wanavyofikiria, wanavyokutana navyo kila siku Shuleni, maeneo ya michezo na makazi yao. Pia, jua aina na tabia za watu wanaoshinda nao ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
Samaki Mkunje Angali Mbichi....