Nawaambieni ukweri ndugu zangu, tuiombee sana nchi yetu. Tuombe amani iendelee kutawala. Haijawahi kutokea rais kutoa zawadi ya pikipiki zenye jina lake kabla hata ya wakati wa kampeni.
Haijawahi kutokea rais kuwasafirisha wananchi nje ya nchi kwa lengo la 'kula bata'.. Haijawahi kutokea rais kukabidhi rasilimali za taifa kwa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji. Yapo mengi ambayo hayawahi kutokea lakini leo yanatokea. Na yanazua maswali mengi.
Tuliombee sana Taifa letu hasa nchi ya Tanganyika! Mwenyezi Mungu aliponye hili taifa