Mzee anaendesha RAV4 huku kavaa Helmet za pikipiki

Umenikumbusha kwetu miaka ya nyuma kuna mzee mmoja alikuwa na Baiskeli aina ya Swala yeye kama anaendesha baskeli basi alikuwa akifika darajani anashuka mpaka ahakikishe amevuka daraja ndio aipande tena!

Duniani kuna vijimambo
Na kwetu kulikua na mzee baiskeli yake ya kubebea mizigo tu hapandi na haikua na pedals,dah wazee wamepita wapumzike kwa amani
 
Huenda mawazo yake anafikiria anaendesha pikipiki. Ila ni kituko cha aina yake, sawa na mama mmoja aliendelea kubeba mzigo wake kichwani akiwa kwenye gari ili asilipie mzigo. Mama ndie kabeba mzigo na sio gari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwetu kulikua na mzee baiskeli yake ya kubebea mizigo tu hapandi na haikua na pedals,dah wazee wamepita wapumzike kwa amani
Hivi vitu vipo ukisikia kwa mtu unaeza sema labda mtu ameamua kufurahisha no vipo kweli
 
Kuna mzee kanunua pkpk ila hutakuja kusikia kujifunza kuendesha ila tokea ujana wake kila akiona toleo jipya analo ila kuendesha ni mwiko juzi kat kanunua gari mambo ni hayo hayo
 
Dunia ina watu watata

Maajabu tumepishana na mzee ana RAV4 anaendesha kavaa Helmet zile za bodaboda kichwani nimeambiwa ukiomba lift anakwambia kama una Helmet panda

Gari yake hata mkewe na watoto wake hawapandi sababu sharti la kuvaa Helmet limewashinda

Mwenyewe anasisitiza kuwa hata abiria kwenye mabasi wawe wanavaa Helmet just in case ajali ikitokea vichwa vyao vitakuwa salama

Ganja bana
 
picha?
 
Mmempeleka Milembe kwa uchuguzi?
 
halafu anakuja kufa na ukimwi anyway avae condom pia
 
Mimi ningekua naangusha kicheko kila nikimuona😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom