Mzee anaendesha RAV4 huku kavaa Helmet za pikipiki

Bro; Kila Shetani na mbuyu wake. WW imekuhusu nini? Mwacheni mzee wa watu atende/afanye ile kitu roho yake inapenda na moyo wake usuuzike alimradi havunji Sheria za Jamhuri..Tz. WW komaa na hali yako. Kama unacheka unapomwonavile , je, yy huwa anakuuliza unacheka nini? au anakuleta huku jamvini? Angalia usikute na yy anakucheka unapomcheka.πŸ€ͺ
 
Anaogopa kupasuka fuvu la kichwa
 
Kuna mzee mmoja yeye akifua nguo yake na kuianika kwenye kamba ikitokea kakuta nzi katua kwenye hiyo nguo yake lazima aianue na kuifua upya.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚daah huyo mzee
 

Huyo mzee namjua alinunuaga bodaboda ikaibiwa akabaki na helmet ndo maana anavaa helmet yake kupunguza hasira na kuikumbuka boda boda yake[emoji81][emoji81]
 
kipindi tunaikaribia daladala niko na babu yangu konda akaropoka akimwambia dereva.... subiri tuchukue vichwa hivyo. Nakwambia mbona alijuta kutoa hiyo kauli.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Bange ntu
 
Kuna mzee mmoja mjeda alikuwa na Korando, alitoa viti vyote akaacha kiti cha dereva tu...

Kwa sababu hakutaka kupakia abiria kwenye gari yake, hata familia yake...
Mtata mwingine huyo
 
Kuna mzee mmoja yeye akifua nguo yake na kuianika kwenye kamba ikitokea kakuta nzi katua kwenye hiyo nguo yake lazima aianue na kuifua upya.
Mzee msafiiiiiii!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…