Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Kwanza niwasalimu ndugu zanguni wapendwa. Kiukweli naona kuna mambo kadhaa nahitaji ushauri wenu.
Mzee anastaafu mwezi ujao tu. So nimeona ni wakati muafaka nami kupanga bajeti. Kwa mzee salary aliyokuwa anapokea ni kama mil 7 kwa mwezi. Pia ana miradi yake kadhaa so maisha hayasumbui.
Je, mnadhani hapo kiinua mgongo anaweza akapewa tsh ngapi? Ili nijue kabisa bajeti inakuaje.
Mimi natamani kununua gari moja kati ya Toyota Vanguard au Rav 4 inayofanana nayo. Nataka nijue from Japan niandae Tsh ngapi ili mzee akipokea tu nimwambie anipatie huo mshiko. Hapa town bila gari ngumu sana kupata watoto warembo.
Nataka na simu moja Samsung ya kukunja. Hapo sasa moyo wangu utakuwa umetulia nasubiria tu sasa agawe urithi maana kuna nyumba 3 mzee alijenga kapangisha.
Mimi nashukuru kupata mzee ambaye aliwekeza. Sina tena haja ya kujenga.maana umri wake umeenda na pia ana sukari. So nategemea akistahafu tu nimwambie agawe kila mtu afe na chake.
Sasa juzi nlikuwa nimeenda home nmetoka kwa sister nikaona nibadilishe mazingira. (Mimi pa kuishi si tatizo na weza lala kwa sister au home nikiona huku wananighasi)
So nikamuuliza mzee anategemea kupata pensheni tsh ngapi? Hakujibu kitu. Kitendo ambacho kilinikwaza sana. Nikaacha na chakula nikaenda room. Nikawaza huyu mzee ana akili kweli? Anadhani tusipopanga bajeti hiyo pesa si itapotea tu? Na anaweza ishia kwenda oa mke mwingine au akapata mchepuko.
Kesho yake hata sikutaka kuonana naye maana nilikuwa na hasira sana.nakumbuka alikuja hadi mlangoni akawa ananiita.sikuitika.
Sasa mnishauri je niende kuuliza ofisini kwao? Je, nimuulize tena? Je kati ya gari hizo ni ipi the best?na katika nyumba zake nichague ya Goba, Mbezi au Kigamboni? Maana nataka niende kabisa kumwambia mpangaji akae kwa kujiadhali akichafua au kuharibu nyumba kitawaka.
Naombeni maoni yenu. Of course mimi nina degree nilisoma SAUT human resource na kumaliza 2010. Bado sijapata ajira ila nimeona si issue naweza simamia miradi ya sister au mzee.