Mzee anategemea kupokea kiinua mgongo, lakini simwelewi elewi kabisa

Mkuu nimepiga hesabu hapa, approximately ni 340Milions.

Mimi kwa wazo lako nakuunga mkono 100%, yalishatukuta kwenye familia yetu mwaka 2004 pindi mzee anastaafu, yeye alikuwa ni askari. Nakumbuka baada ya mzee kurejea home alisema atanunua gari (bus), ataboresha mazingira ya nyumbani, na pia nakumbuka alisema ataleta mashine za kusaga na kukoboa.

Aisee huwezi amini, hakufanya jambo hata moja, alikuwa akienda club analala hukohuko anarudi asubuhi, alikuwa na michepuko afadhali ile ya suleimani inahesabika. Yaani hata mazingira ya hapa home tumeyarekebisha sisi watoto huku ukubwani.

Siyo kwamba unampangia matumizi laah hasha fedha kama hizo ni vyema nyie kama familia mkanufaika nazo.

If you think you're a good person, go home and love your family, hao ndio watakuuguza uzeeni.
 
Kuna mtu tena mtumishi wa umma alimpeleka baba yake ustawi wa jamii, eti alitumia hela ya kustaafu kula na mchepuko, na wao Kama wanafamilia hawajanufauka, nilishangaa sana!!!!
 
Nilizani utasema kuna mwanamke mchepuko ametega mingo ya kumkwapilia mzee wako pension yake Kwa hiyo unaomba ushauri jinsi ya kumnusuru babio na kuibiwa pension yako kumbe sio?!

Kumbe ni wewe unapigia hesabu hela ya mzee wako?!

Muongoze vizuri bila hila moyoni mwako.
 
Kwanza niwasalimu ndugu zanguni wapendwa. Kiukweli naona kuna mambo kadhaa nahitaji ushauri wenu.

Mzee anastaafu mwezi ujao tu. So nimeona ni wakati muafaka nami kupanga bajeti. Kwa mzee salary aliyokuwa anapokea ni kama mil 7 kwa mwezi. Pia ana miradi yake kadhaa so maisha hayasumbui.

Je, mnadhani hapo kiinua mgongo anaweza akapewa tsh ngapi? Ili nijue kabisa bajeti inakuaje.

Mimi natamani kununua gari moja kati ya Toyota Vanguard au Rav 4 inayofanana nayo. Nataka nijue from Japan niandae Tsh ngapi ili mzee akipokea tu nimwambie anipatie huo mshiko. Hapa town bila gari ngumu sana kupata watoto warembo.

Nataka na simu moja Samsung ya kukunja. Hapo sasa moyo wangu utakuwa umetulia nasubiria tu sasa agawe urithi maana kuna nyumba 3 mzee alijenga kapangisha.

Mimi nashukuru kupata mzee ambaye aliwekeza. Sina tena haja ya kujenga.maana umri wake umeenda na pia ana sukari. So nategemea akistahafu tu nimwambie agawe kila mtu afe na chake.

Sasa juzi nlikuwa nimeenda home nmetoka kwa sister nikaona nibadilishe mazingira. (Mimi pa kuishi si tatizo na weza lala kwa sister au home nikiona huku wananighasi)

So nikamuuliza mzee anategemea kupata pensheni tsh ngapi? Hakujibu kitu. Kitendo ambacho kilinikwaza sana. Nikaacha na chakula nikaenda room. Nikawaza huyu mzee ana akili kweli? Anadhani tusipopanga bajeti hiyo pesa si itapotea tu? Na anaweza ishia kwenda oa mke mwingine au akapata mchepuko.

Kesho yake hata sikutaka kuonana naye maana nilikuwa na hasira sana.nakumbuka alikuja hadi mlangoni akawa ananiita.sikuitika.

Sasa mnishauri je niende kuuliza ofisini kwao? Je, nimuulize tena? Je kati ya gari hizo ni ipi the best?na katika nyumba zake nichague ya Goba, Mbezi au Kigamboni? Maana nataka niende kabisa kumwambia mpangaji akae kwa kujiadhali akichafua au kuharibu nyumba kitawaka.

Naombeni maoni yenu. Of course mimi nina degree nilisoma SAUT human resource na kumaliza 2010. Bado sijapata ajira ila nimeona si issue naweza simamia miradi ya sister au mzee.
Chagua nyumba ya kigamboni maana barabara za kwenda kule zinapendeza sana ukiwa unapita na magari makali kama unayopanga kununua
 
Kuna mtu tena mtumishi wa umma alimpeleka baba yake ustawi wa jamii, eti alitumia hela ya kustaafu kula na mchepuko, na wao Kama wanafamilia hawajanufauka, nilishangaa sana!!!!
Hii ni Sawa.

Na wakiweza kuzuia ni nzuri sana maana mchuma janga hula na wakwao.

Yaani arubuniwe aibiwe pension yake halafu aje kuwa tegemezi kwa watoto kila wakati kuwaomba hela za matumizi?

Hapana wakati angeweza kutumia hela yake kidogo bila kuwa mzigo kwa watoto.
 
Hii dunia unaweza ukadhani umeshaona yote kumbe wap
 
Ndo madhara ya kauli mbiu ya Jf. Where we dare to talk openly...
 
Hii ni Sawa.

Na wakiweza kuzuia ni nzuri sana maana mchuma janga hula na wakwao.

Yani arubuniwe aibiwe pension yake halafu aje kuwa tegemezi kwa watoto kila wakati kuwaomba hela za matumizi?

Hapana wakati angeweza kutumia hela yake kidogo bila kuwa mzigo kwa watoto.
Hivi babu wa miaka 61 na kibinti Cha miaka 25, nani anamrubuni mwenzake?
 
Pesa za babaako wewe unazipangia bajeti? Tafuta kazi upate za kwako usije ukaumia Bure kwa pesa ambayo haikuhusu
Itakuwa wa Kinondoni mvaa vibukta...
anapenda kutanua pesa za wengine na ipo siku watamtanua kwa tama zake,
 
Kwanza niwasalimu ndugu zanguni wapendwa. Kiukweli naona kuna mambo kadhaa nahitaji ushauri wenu.

Mzee anastaafu mwezi ujao tu. So nimeona ni wakati muafaka nami kupanga bajeti. Kwa mzee salary aliyokuwa anapokea ni kama mil 7 kwa mwezi. Pia ana miradi yake kadhaa so maisha hayasumbui.

Je, mnadhani hapo kiinua mgongo anaweza akapewa tsh ngapi? Ili nijue kabisa bajeti inakuaje.

Mimi natamani kununua gari moja kati ya Toyota Vanguard au Rav 4 inayofanana nayo. Nataka nijue from Japan niandae Tsh ngapi ili mzee akipokea tu nimwambie anipatie huo mshiko. Hapa town bila gari ngumu sana kupata watoto warembo.

Nataka na simu moja Samsung ya kukunja. Hapo sasa moyo wangu utakuwa umetulia nasubiria tu sasa agawe urithi maana kuna nyumba 3 mzee alijenga kapangisha.

Mimi nashukuru kupata mzee ambaye aliwekeza. Sina tena haja ya kujenga.maana umri wake umeenda na pia ana sukari. So nategemea akistahafu tu nimwambie agawe kila mtu afe na chake.

Sasa juzi nlikuwa nimeenda home nmetoka kwa sister nikaona nibadilishe mazingira. (Mimi pa kuishi si tatizo na weza lala kwa sister au home nikiona huku wananighasi)

So nikamuuliza mzee anategemea kupata pensheni tsh ngapi? Hakujibu kitu. Kitendo ambacho kilinikwaza sana. Nikaacha na chakula nikaenda room. Nikawaza huyu mzee ana akili kweli? Anadhani tusipopanga bajeti hiyo pesa si itapotea tu? Na anaweza ishia kwenda oa mke mwingine au akapata mchepuko.

Kesho yake hata sikutaka kuonana naye maana nilikuwa na hasira sana.nakumbuka alikuja hadi mlangoni akawa ananiita.sikuitika.

Sasa mnishauri je niende kuuliza ofisini kwao? Je, nimuulize tena? Je kati ya gari hizo ni ipi the best?na katika nyumba zake nichague ya Goba, Mbezi au Kigamboni? Maana nataka niende kabisa kumwambia mpangaji akae kwa kujiadhali akichafua au kuharibu nyumba kitawaka.

Naombeni maoni yenu. Of course mimi nina degree nilisoma SAUT human resource na kumaliza 2010. Bado sijapata ajira ila nimeona si issue naweza simamia miradi ya sister au mzee.
Hahaaa..kweli bhana hongera..ukiona mzee anazingua kukujibu mchape makofi atoe majibu haraka ebo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom