Mzee anategemea kupokea kiinua mgongo, lakini simwelewi elewi kabisa

We utakuwa masikini wa kutupwa ila hapa unaleta changamsha kijiwe tu🤣🤣🤣
 
Kuwa na mtoto Kama wewe Ni hasara,ungekuwa mwanangu ningekupeleka kyela nikabadilishane kwa gunia la mpunga tu walah!
 
Leo wale wategemezi wa wazazi hadi wakiwa na umri wa 40+ wamejificha wapi
 
Mimi nakushauri, hii hadithi ukaisimulie kule facebook, itapendeza zaidi
 
Hapo ukute mzee alimwombea mwanawe awe kama christiano ronaldo, na mwanawe alimwombea mzee awe kama baresa.
Patamu hapoo!
 
Atapokea kama 200m hivi.
Nyumba chukua ya mbezi beach
Kweli? Maana hili linanifikirisha ingawa bado nahisi kama zinaweza zidi hapo. Mzee asije akatukata panga hizo pesa...
 

Nilianza kusoma kwa umakini nilipofika kwenye point ya kununua gari na kupata warembo nikaacha.

Uzi wa kijinga tu huu.
Wanawake hawajawahi mtajirisha mtu zaidi ya kumfirisi.

Piga mbususu kwa akili sana unaweza ugua ukakosa hata panadol
 
Nimejikuta nacheka,,,yaan wewe ungekuwa mwanangu tayari ningeenda kukuweka polisi ukae hata miaka 5 ukitoka akili zikusimame. Dunia ya leo bado kuna mtoto anawaza urithi wa mzazi wake aiseee. Tuzae tu kwa kweli.
Namshukuru mzazi wetu wakati tunasoma alisema wazi kabisa hakuna atauekuja kupata urithi wowote kwake zaidi ya elimu anayotupa tena alikuwa anasema akiwa serious kabisa. Hali ile ilitufanya sote tusome kwa bidiiii na kwa machungu. Leo hii sote tunamaisha yetu. Na dingi bado hajastaafu. Anatarajia kustaafu baada ya miaka 3 mbele lkn hakuna hata mmoja anayewaza hata huo urithi wake. Na tulipopata kazi wote alitumbia tusihangaike na yeye iwe kumuhudumia wala kumuwazia. Tunamtumiaga hela tu pale tunapojisikia.

Kwa sheria za Tz huwezi kudai urithi kwa mzazi ilihali yupo hai,,labda awape tu kwa mapenzi yake. Na kumdai mzazi urithi ilihali hajafa ni kujitakia tu laana isiyokuwa na maana.
 
We chizi kweli,
 
Sio fair kutolea macho pesa ya mzaz wako tena mstaafu

Umesema mzee wako alikua anapokea 7mil mtu kama huyu sidhan kama anaweza kuwa na mtt mwenye mawazo kama ya kwako maana alikua na uwezo wa kumpeleka shule nzuri na ni mara chache kuwa na akili za kuandika kitu kama ulichoandika hapa🙂

Fikiria wewe umekuwa mzee unasikia watt wako wanakupigia hesabu kama hizi
 
Hizi thread nyingine ukisoma unaona kama mtu katunga hadithi kuwachota akili aone mnajibu nini tu.

Kama social experiment tu.

Lakini pia inawezekana kuna watu u wana akili za hivi.
Kwa hizi jamii zetu haya mambo yapo sana tu, hata kama wanaiita 'chai ', lakini bado ina uhalisia mno kwenye jamii yetu.
 
Wanangu ambao mmeajiriwa au mmejiajiri kujenga mwisho nyumba moja tu tena unamuandika bi mkubwa zilizobaki kula maisha ukisikiliza ile kesi ya arusha ya mzee said na mwanae Abdallah unaona kabisa watoto wa kizazi kijacho watakuwa wanauwa wazazi wao kwa tamaa za mali bila kusahau yule wa kcmc aliyeuliwa na mwanawe wa kike tuleni maisha wanangu.
 
Hizi thread nyingine ukisoma unaona kama mtu katunga hadithi kuwachota akili aone mnajibu nini tu.

Kama social experiment tu.

Lakini pia inawezekana kuna watu u wana akili za hivi.
Na ndicho alichofanya huyu jamaa,
Sio mara ya kwanza kashakuja na mada hizi mara nyingi tu hapa.
 
Tafuta zako acha mzee aongeze mke wa pili
 
Nakushauri tafuta mume upewe gari, nyumba na hiyo simu uitakayo.
Muache mzee afurahie pesa na maisha yake.
Hutaki mzee apate mchepuko,ww unaweza kumtoa genye zake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…