Mzee Augustine Mahiga ndiye alikuwa "role model" wangu. Roho inaniuma sana sikuweza kuhudhuria msiba wake. Siku moja ninatamani kuja kuwa kama yeye

Mzee Augustine Mahiga ndiye alikuwa "role model" wangu. Roho inaniuma sana sikuweza kuhudhuria msiba wake. Siku moja ninatamani kuja kuwa kama yeye

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

images (69).jpg


Ndugu zangu Watanzania;

Kama kuna matukio yaliouchoma moyo wangu ndani ya mwaka huu wa 2020 basi ni kifo cha huyu mzee Augustine Philip Mahiga. Huyu baba sikubahatika kuonana naye ana kwa ana lakini ndiye aliyekuwa "role model" wangu katika kupenda masuala ya kidiplomasia na siasa za kimataifa.

images (68).jpg


Siku moja ninatamani kuja kuwa mwanadiplomasia makini na mwanasiasa mstaarabu kama yeye. The guy was sincerely humble and kind, mwanasiasa muungwana na mstaarabu kweli kweli.

Roho inaniuma sana sikuweza kuhudhuria msiba pamoja na mazishi yake kutokana na changamoto ninazozipitia sasa katika maisha yangu lakini ipo siku nikienda Iringa nitapita katika kaburini lake walau nisimame dakika tano niangalie pahala alipolala huyu shujaa wangu.

images (70).jpg


USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO NA UIPENDE TANZANIA KAMA MZEE AUGUSTINE MAHIGA.
 
Apumzike kwa amani.

Ila angekuwa mwanasiasa wa kwenda bungeni, sijui angekuwaje!
 
Marehemu Dr. Augustine Mahiga kweli alikuwa mwana diplomasia mahili wa kutukuka na mtu mwenye busara ; alikubali hata kufanya kazi chini ya watu ambao walikuwa hawana hata nusu ya akili zake!!!
Mahiri si mahili
 
Huyu mzee sijui maccm yalimfanya nini.

Yaani kabla hata msiba haujaisha li meko limeshateua lijitu lake
 
Back
Top Bottom