Mzee Butiku ana lipi la kushauri kuhusu Uchumi?

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Hili halisemwi sana ila ndo ukweli wenyewe!

Moja ya sababu zilizofanya Mwl. Nyerere aamue kung' atuka mwaka 1985 ni kutokana na kufeli kwa Sera zake za kiuchumi hasa za kijamaa. Ilifika kipindi watanzania walianza kuvaa nguo zenye viraka na hata ununuzi wa bidhaa madukani ulifanyika kwa foleni. Kuwa na Sukari ilikuwa anasa na watu walifikia hadi kufua nguo zao kwa majani ya mpapai.

Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1981 lilimshtua sana Nyerere ambae washauri wake wakuu walikuwa ndugu yake Mzee Butiku.

Ukiniuliza mimi moja ya sababu za umaskini wa Watanzania ni ujinga ulioletwa na Sera za Kijamaa ambazo watu wanaozipigia debe mmoja wapo ni huyu Mzee Butiku.

Kama kwa Sera hizo za Kijamaa nchi yetu ni maskini hivi basi waache wenzao wenye akili mbadala waamue.

Ni muda sasa wa nchi kufanya maamuzi na kujikita kwenye kazi kuliko maneno maneno.

Rais Samia chapa kazi, tumechelewa sana kwa akili za kijinga!
 
Umekuwa vizuri pale mwanzoni ni kweli umaskini wa Tanzania umesababishwa na sera mbovu ya kiuchumi ya kijamaa. Ujamaa umedumaza hata akili zetu. Lakini hapa mwishoni umerudi kwenye yale makosa ya Taifa letu; kuwasifia na kuwaunga mkono watu dhaifu.

Nyerere alifanya makosa mengi ikiwepo kutaka watu wote walingane kwa kila kitu, hata Mungu hakuumba hivyo. Aliwafanya watu waogope utajiri kwa kuwabana matajiri, kuwazuia wasiwe viongozi na kuwaita wezi. Ndio maana hadi leo tunaongozwa na watu dhaifu tukifikiri ni fadhila.

Kuna mengi sana ya kubadilisha nchi hii ili tuendelee ikiwa ni pamoja na sera mbaya, katiba mbovu na mfumo CCM.
 
Unakuta hao wazee wanapigania sera za kijamaa huku watoto na wajukuu zao wapo USA na Canada
 
Kisa Mzee Butiku amesema ule mkataba wa hovyo wa bandari uangaliwe upya ndio umeanza ujinga wako, kuvaa viraka huku ukiwa ndani ya mipaka ya nchi yako, ukiwa unathaminiwa utu wako, kwangu ni muhimu kuliko kuwaruhusu waarabu waje kujitawala ndani ya mipaka yetu.
 
Kuna shida gani nikikuita mjinga?
Kisa Mzee Butiku amesema ule mkataba wa hovyo wa bandari uangaliwe upya ndio umeanza ujinga wako, kuvaa viraka huku ukiwa ndani ya mipaka ya nchi yako, ukiwa unathaminiwa utu wako, kwangu ni muhimu kuliko kuwaruhusu waarabu waje kujitawala ndani ya mipaka yetu.
 
Hili halisemwi sana ila ndo ukweli wenyewe!

Moja ya sababu zilizofanya Mwl. Nyerere aamue kung' atuka mwaka 1985 ni kutokana na kufeli kwa Sera zake za kiuchumi hasa za kijamaa. Ilifika kipindi watanzania walianza kuvaa nguo zenye viraka na hata ununuzi wa bidhaa madukani ulifanyika kwa foleni. Kuwa na Sukari ilikuwa anasa na watu walifikia hadi kufua nguo zao kwa majani ya mpapai.

Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1981 lilimshtua sana Nyerere ambae washauri wake wakuu walikuwa ndugu yake Mzee Butiku.

Ukiniuliza mimi moja ya sababu za umaskini wa Watanzania ni ujinga ulioletwa na Sera za Kijamaa ambazo watu wanaozipigia debe mmoja wapo ni huyu Mzee Butiku.

Kama kwa Sera hizo za Kijamaa nchi yetu ni maskini hivi basi waache wenzao wenye akili mbadala waamue.

Ni muda sasa wa nchi kufanya maamuzi na kujikita kwenye kazi kuliko maneno maneno.

Rais Samia chapa kazi, tumechelewa sana kwa akili za kijinga!
kweli vijana wengi tanzania akili ni kisoda na wavivu wa kusoma, mitandao imewaathiri sana, wengi wanasimuliwa vitu bila hata tafiti hata kidogo, haya mambo yameandikwa kwenye maandishi, haitaji hata kwenda shule sana ili ujue hii, mpaka sasa ujui nchi yao ni mlengo gani wa kijamaa au ya kibepari?, kwani lini nchi iliacha siasa ya ujamaa? kasome katiba ya nchi yako ili ujue nchi yako ina siasa za nchi mlengo gani.

have a respect na nyererre, angetaka kuuza rasilimali za nchi hata bandari wanayauza ndugu zako msingeikuta leo, angetaka kufanya hivyo hata ngorongoro angeshauza, madini angeshauza, mlima kilimanjaro angeshauza, aliwapenda watanzania kama familia na hakupenda kujilimbikizia mali wala hakuwa mlafi wa mdaraka kama viongozi wetu wa leo.. mpe heshima yake anayostahili,
 
Kuna kitu gani hapa nchini kimeuzwa? Unajua hata maana ya kuuzwa?
 
Inasikitisha Sana...yaani mwaka 2023 mtu anamsikiliza Butiku ..,Shivji ..
Ukiuliza unaambiwa hawa wazalendo....as if uzalendo ndo qualifications za kujipa utaalam WA uchumi na uwekezaji.....

Kuwa na uchungu na nchi ni jambo moja na kuwa na majibu ya uchumi ni jambo lingine...
Wote tuna uchungu na wazazi wetu ..
Lakini wakiumwa tunaenda wasikiliza madaktari hospitali...daktari Hana uchungu na mzazi wako ..anaweza kuwa hata amekunywa kidogo lakini ndo "Mtaalam"..wa kusikilizwa
 
wasomi hawapingwi kwa mipasho mkuu kwa kuhamisha goli, jibu hoja zao ndio ueleweke,
 
Inasikitisha Sana...yaani mwaka 2023 mtu anamsikiliza Butiku ..,Shivji ..
Ukiuliza unaambiwa hawa wazalendo....as if uzalendo ndo qualifications za kujipa utaalam WA uchumi na uwekezaji.....

Kuwa na uchungu na nchi ni jambo moja na kuwa na majibu ya uchumi ni jambo lingine...
Wote tuna uchungu na wazazi wetu ..
Lakini wakiumwa tunaenda wasikiliza madaktari hospitali...daktari Hana uchungu na mzazi wako ..anaweza kuwa hata amekunywa kidogo lakini ndo "Mtaalam"..wa kusikilizwa
Hawa watu ndo chanzo cha nchi kuwa masikini hivi! Alafu leo wanataka kuturudisha kule kule
 
Umekuwa vizuri pale mwanzoni ni kweli umaskini wa Tanzania umesababishwa na sera mbovu ya kiuchumi ya kijamaa. Ujamaa umedumaza hata akili zetu. Lakini hapa mwishoni umerudi kwenye yale makosa ya Taifa letu; kuwasifia na kuwaunga mkono watu dhaifu.

Nyerere alifanya makosa mengi ikiwepo kutaka watu wote walingane kwa kila kitu, hata Mungu hakuumba hivyo. Aliwafanya watu waogope utajiri kwa kuwabana matajiri, kuwazuia wasiwe viongozi na kuwaita wezi. Ndio maana hadi leo tunaongozwa na watu dhaifu tukifikiri ni fadhila.

Kuna mengi sana ya kubadilisha nchi hii ili tuendelee ikiwa ni pamoja na sera mbaya, katiba mbovu na mfumo CCM.
Uzuri Butiku anaheshimika kuzidi kikwete na amesikilizwa TZ nzima
 
Hili halisemwi sana ila ndo ukweli wenyewe!

Moja ya sababu zilizofanya Mwl. Nyerere aamue kung' atuka mwaka 1985 ni kutokana na kufeli kwa Sera zake za kiuchumi hasa za kijamaa. Ilifika kipindi watanzania walianza kuvaa nguo zenye viraka na hata ununuzi wa bidhaa madukani ulifanyika kwa foleni. Kuwa na Sukari ilikuwa anasa na watu walifikia hadi kufua nguo zao kwa majani ya mpapai.

Jaribio la Mapinduzi la mwaka 1981 lilimshtua sana Nyerere ambae washauri wake wakuu walikuwa ndugu yake Mzee Butiku.

Ukiniuliza mimi moja ya sababu za umaskini wa Watanzania ni ujinga ulioletwa na Sera za Kijamaa ambazo watu wanaozipigia debe mmoja wapo ni huyu Mzee Butiku.

Kama kwa Sera hizo za Kijamaa nchi yetu ni maskini hivi basi waache wenzao wenye akili mbadala waamue.

Ni muda sasa wa nchi kufanya maamuzi na kujikita kwenye kazi kuliko maneno maneno.

Rais Samia chapa kazi, tumechelewa sana kwa akili za kijinga!
Na Nyerere alikuwa hivyo hivyo.
Baada ya nchi kumshinda hakupenda kuona Mwinyi akifanya tofauti na sera zake, so akaishia kuwa anamshambulia tu sirini na hadharani
 
Kisa Mzee Butiku amesema ule mkataba wa hovyo wa bandari uangaliwe upya ndio umeanza ujinga wako, kuvaa viraka huku ukiwa ndani ya mipaka ya nchi yako, ukiwa unathaminiwa utu wako, kwangu ni muhimu kuliko kuwaruhusu waarabu waje kujitawala ndani ya mipaka yetu.
Duh!
Kwa hiyo kwako wewe unaona afadhali tu turudi enzi za kuvaa kaniki, uhaba wa bidhaa muhimu na tuvae tu nguo za viraka.
Kweli bandari imekuvuruga. Sijui ndo unaanza kuiona juzi hiyo bandari basi hulali kutwa kucha we unawaza bandari tu
 
Acha ujinga mtoa mada sera ya kijamaa haikuwa tatizo ila tatzo ni ujinga wa watendaj ikapelekea mismanagement of resource,pili ubepari ulishika hatamu kwa nchi ndogo kama tanzania ni ngumu kupingana nao,kinawasumbua suala la bandari ni itikadi ya vyama 2.,CHADEMA akiingia madarakan atafany kama alivyofanya samia kubinafsisha hakuna hasara au uuzwaji wa bandari muhm kuweka sera nzur madhubut ya kodi.ukiona wanapga kelele ujue wanamaslah yao ila vizur kubinafsha ili serikal ifanye mambo ya maana zaid,pesa wanakula wakurugenz 2
 
Kuna kitu gani hapa nchini kimeuzwa? Unajua hata maana ya kuuzwa?
Nyerere ndo aliyeanzisha mambo hii ya kusema eti nchi imeuzwa.
Tumeanza kusikia nchi kuuzwa tokea miaka ya 1990s lkn mpk leo wanarudia tu. Sijui wanatafsiri vp nchi kuuzwa au ndo wamekariri tu
 
Back
Top Bottom