Serikali ipo serious sana. Shida nyie mnaleta siasa zenu uchwara
Tuliokuwa na akili awamu ya kwanza walisema hivyo hivyo, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya pili, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya tatu, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya nne, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya tano, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya sita, "serikali ipo serious sana".
Lakini cha kustaajabisha, miaka 60 baada ya uhuru na miaka 60 baada ya "serikali iliyo serious sana" kuamua kusomesha raia wake ili wawe na uwezo na ujuzi waje kushika nafasi za kiuongozi kwenye taasisi,mashirika,viwanda na idara, eti bado tunatafuta watu wa kutoka nnje waje kuendesha taasisi zetu!!
Hizo awamu tangu ya kwanza zilifanya nini kuwaandaa raia wake kuja kuendesha nchi na taasisi zake kama leo hii hatuna uwezo wa kuendesha wenyewe!!??
Maana yake ni kwamba hata chama tawala kinapaswa kuendeshwa na watu kutoka nnje maana wameshindwa hata kuandaa raia wa kuendesha nchi yao.
Failure kubwa sana kwa wananchi, serikali, chama tawala na taasisi zote za kuandaa watendaji na viongozi.