Mzee Butiku ana lipi la kushauri kuhusu Uchumi?

Mtaongea maneno mengi sana ila ukweli ndio huo. Sara ya Ujamaa ilifeli big time. Tuliokuwa wadogo miaka ile hatutasahau unaenda kuweka jiwe kwenye foleni ya kununua bidhaa dukani. Nyie wa juzi tulieni tu Serikali ifanye maamuzi sahihi.
 
Nyerere ndo aliyeanzisha mambo hii ya kusema eti nchi imeuzwa.
Tumeanza kusikia nchi kuuzwa tokea miaka ya 1990s lkn mpk leo wanarudia tu. Sijui wanatafsiri vp nchi kuuzwa au ndo wamekariri tu
Ukiwauliza nchi imeuzwaje wakiweza kukujibu njoo unishtue
 
Hivi serikali ya Tanzania chini ya chama cha mapinduzi unaona ipo serious kiasi gani kwenye majukumu yake ya msingi?

Swali kama hilo wewe utajibu nini?
 
Sifa ya mtu mwenye hekima na akili nyingi ni kuwa na maono yaani visions. Nyerere alikuwa na maono na akawashauri marais wenzake wa awamu ya kwanza wa nchi zinazotuzunguka juu ya suala zima la kuachia madaraka na wenzake wakambishia.

Hawakuona kile alichokuwa amekiona tayari, Kaunda akafungwa jela na Mwalimu Nyerere akaenda kumtembelea kifungoni. Mzee Banda akafa kwa uzee, Mobutu akashindwa vita na akaenda kufia ugenini Morocco na kuzikwa na watu wasiopungua kumi!.

Anaweza kutupiwa lawama Nyerere leo hii kwa maamuzi aliyoyafanya mwaka sitini na nne lakini hakuna anayejua wakati anaamua kuchukua sera za kijamaa dunia ya wakati ule ilikuwa vipi, tukumbuke hapakuwa na utandawazi kama huu wa leo, hapakuwa na simu za mikononi za kisasa.

Napata ugumu sana kumtupia lawama Nyerere kwa kuamua kuwa mjamaa miaka ya sitini wakati hali halisi ya nchi ya wakati huo siifahamu vyema. Mwaka sitini na moja tunapata uhuru katika serikali yake wataalam wenye elimu za vyuo vikuu hawakuzidi wazalendo kumi.

Tofauti na sasa tuna maelfu kwa maelfu ya wenye shahada za vyuo vikuu wanaomaliza na kuishia kukaa nyumbani miaka miwili wakisikilizia ajira sehemu mbalimbali.
 
Wengi wanaopinga uwekezaji wa bandarini wanakuja na hoja za kijamaa na zenye uoga wa mabadiliko.

Utasikia wanasema eti waarabu wanaturudisha tena utumwani, stupid argument.

Mwarabu kawekeza kwenye bandari za Marekani, Uingereza na mataifa mengine, ina maana kote huko anarudisha watu utumwani?.

Ni mawazo ya kijamaa kuogopa kufikiria zaidi ya kile unachokifahamu kichwani mwako. Kuuwekea ubongo mipaka ni hulka za kijamaa tena ule mkongwe.
 
Butiku ameekeza ya msingi kuliko wewe hapa ya kishabiki..
 
Kwani bado Tz inaendeshwa kwa uchumi wa kijamaa ?...umewahi kusikia kuhusu azimio la Zanzibar ?
 
Nyerere ndo aliyeanzisha mambo hii ya kusema eti nchi imeuzwa.
Tumeanza kusikia nchi kuuzwa tokea miaka ya 1990s lkn mpk leo wanarudia tu. Sijui wanatafsiri vp nchi kuuzwa au ndo wamekariri tu
Watu wanalalamikia baadhi ya vipengele vya ule mkataba na sio uwekezaji.
 
haku
Kuna hoja yeyote imetolewa kwani?

watu wanapinga construction ya mkataba, wala sio mwarabu. hata mie napinga na sipingi uwekezaji napinga mkataba basi, sina argument zaidi ya mkataba, sina kabisa arguement zaidi ya mkataba unaolitweza taifa, mkataba, mkataba, mkataba full stop. zingine ni siasa,

hizo argument za waarabu ni strong points za wanaosupport ili kuwafanya weak wanaopinga, kama kweli mkataba ni mzuri, jibu arguemnt zilizowekwa as against wanaopinga mkataba, kwangu mimi ni arguemnt za wanasupport ili kufisha ukweli waaweka kibwagizo cha mwarabu kawekeza marekani, udini, uzanzibar, utanganyika, lakini shida ni nature ya mkataba wetu na hao warabu wako?, wote wanaopinga DPW hawapingi uwekezaji wa DPW, wanapinga mkataba,

mkataba, mkataba, mkataba its an issue, sio dpw
 
Serikali ipo serious sana. Shida nyie mnaleta siasa zenu uchwara
Mimi naamini kama serikali ingekuwa ipo serious sana kwenye majukumu yake ya msingi basi hata hizo siasa uchwara zisingekuwa na nafasi kubwa sana nchini. Hili suala la bandari tu jinsi hali ilivyo na ukiangalia jinsi serikali inavyolikabili unaona hawapo serious.
 
Serikali ipo serious sana. Shida nyie mnaleta siasa zenu uchwara
Tuliokuwa na akili awamu ya kwanza walisema hivyo hivyo, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya pili, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya tatu, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya nne, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya tano, "serikali ipo serious sana".
Awamu ya sita, "serikali ipo serious sana".

Lakini cha kustaajabisha, miaka 60 baada ya uhuru na miaka 60 baada ya "serikali iliyo serious sana" kuamua kusomesha raia wake ili wawe na uwezo na ujuzi waje kushika nafasi za kiuongozi kwenye taasisi,mashirika,viwanda na idara, eti bado tunatafuta watu wa kutoka nnje waje kuendesha taasisi zetu!!

Hizo awamu tangu ya kwanza zilifanya nini kuwaandaa raia wake kuja kuendesha nchi na taasisi zake kama leo hii hatuna uwezo wa kuendesha wenyewe!!??

Maana yake ni kwamba hata chama tawala kinapaswa kuendeshwa na watu kutoka nnje maana wameshindwa hata kuandaa raia wa kuendesha nchi yao.

Failure kubwa sana kwa wananchi, serikali, chama tawala na taasisi zote za kuandaa watendaji na viongozi.
 
Nyerere ndo aliyeanzisha mambo hii ya kusema eti nchi imeuzwa.
Tumeanza kusikia nchi kuuzwa tokea miaka ya 1990s lkn mpk leo wanarudia tu. Sijui wanatafsiri vp nchi kuuzwa au ndo wamekariri tu
Nyerere alikuwa mjamaa kindakindaki aliyeuchukia ubepari (japo akishirikiana nao baadhi ya maeneo mfano uwekezaji kule mwadui) na mpaka dakika za mwisho hakuamini sera zake zilishafeli.

Ila mageuzi yaliyofuata baada yake kwa shinikizo la IMF yametuletea ubepari uchwara tu, uliozaa ufisadi na ukwepaji kodi tu unaofanywa wawekezaji uchwara.
 
Kwani Tanzania ya leo nani ni tajiri zaidi ya viongozi wa CCM na serikali na washirika wao pamoja Chawa wao kama wewe.Sasa wewe una kipi cha kumfundisha Butiku kuhusu masuala ya kuendesha Siasa na Uchumi wa nchi!
 
Hakuna shida kwasababu wewe ni chawa mpumbavu.
Hawa ndiyo wanapoteza nchi kujifanya wajuaji, waasisi wa taifa wanazungumza kanatokea Kakenge kamezaliwa juzi kanajifanya kanajua kisa kamelamba asali.Hatari sana!
 
Kuna kitu gani hapa nchini kimeuzwa? Unajua hata maana ya kuuzwa?
Wewe ni mwehu unataka mpaka wakutangazie,mikataba ya Kimangungo hiyo inayowapa Wageni power kuliko Wazawa ndiyo kuuza nchi kwenyewe.
 
Kwaiyo wewe unajua Siri za nchi kuliko Butiku?Wewe hujazaliwa wenzako wapo Ikulu wanaongoza nchi,kwani hayo Mashirika na Rasilimali mnazo uza au kama mnavyopenda kusema kukodisha na kubinafsisha ni akina nani waliyaanzisha na kuyasimamia!!
Kwani walishindwa wao kuyauza Ili watajirike,mnakuja na visiasa vyenu uchwara,eti utaalamu wa Uchumi, Uchumi aliojenga nani?
Hopeless generation!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…