TANZIA Mzee David Cleopa Msuya afariki Dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Mzena

Safi
 
Hakuna ajuae yajayo.
Fedha hununua vingine lakini sio afya
 
R.I.P Priemier
 
Mwenye kujua kwa nini anatajwa makamu wa kwanza wa Rais atuambie?

..C.D.Msuya alitumikia kipindi cha chama kimoja.

..wakati huo Raisi wa Muungano akitoka Tanganyika, Raisi wa Zanzibar anakuwa Makamu wa Raisi.

..vilevile Raisi wa Muungano akitoka Zanzibar, Waziri Mkuu anakuwa Makamu wa kwanza wa Raisi, na Rais wa Zanzibar anakuwa Makamu wa pili.

..Kwa hiyo ni katika utawala wa Rais Sihaba Nzasa Ally Hassan Mwinyi ndio tulikuwa na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais.

..Mzee Joseph Warioba, Mzee Cygwiyemisi John Malecela, na Mzee Cleopa Msuya, ndio waliowahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…