TANZIA Mzee David Cleopa Msuya afariki Dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Mzena

TANZIA Mzee David Cleopa Msuya afariki Dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Mzena

Rais Samia Suluhu ametangaza kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya ambaye amefariki leo Mei 7, 2025 alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena


Aliekaa kwenye kiti mwendo ni CLEOPA DAVID MSUYA
=> Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Tanzania 1994-1995
=> Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1980 -1983
=> Waziri wa Wizara tofauti kama wizara ya Fedha na wizara ya viwanda
=> Katibu Mkuu wa Wizara tofauti tofauti
=> Mtia nia ya kuwania urais kupitia Chama cha Mapinduzi Mwaka 1995 alikuwa kwenye wale makada watatu Yeye, B.M Mkapa na JK

Natamani kupata wasifu wake kamili,elimu aliyosoma,mke aliyemuoa,watoto aliozaa maana haijaandikwa kwa ukamilifu
 
Mzee Msuya tayari mwaka 1965 alikuwa kamishna wizara ya fedha!!,

Hiyo ni kwa mujibu wa ankal wangu.

Mungu akupe nini tena wafanya kazi na wazungu wakoloni jikoni hazina!

Anyway, Job na familia poleni sana.

RIP.
December 1964 C.D Msuya alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara serikali ya Tanzania.

Picha hii hapa.

Msuya ni wa nne kutoka kushoto nyuma.

RIP

IMG-20250404-WA0062.jpg
 
December 1964 C.D Msuya alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara serikali ya Tanzania.

Picha hii hapa.

Msuya ni wa nne kutoka kushoto nyuma.

RIP

View attachment 3330927
Hongera kwa kutupa picha ya kumbukumbu ya wasomi na wazalendo kipindi hicho, bila shaka mmoja wa family Yako alikuwa ni msomi na Tena akihudumu nyumba nyeupe
 
Hongera kwa kutupa picha ya kumbukumbu ya wasomi na wazalendo kipindi hicho, bila shaka mmoja wa family Yako alikuwa ni msomi na Tena akihudumu nyumba nyeupe
Mmoja yupo kwenye picha hapo.

Hizi ni picha zilizotunzwa katika maktaba ya familia.
 
December 1964 C.D Msuya alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara serikali ya Tanzania.

Picha hii hapa.

Msuya ni wa nne kutoka kushoto nyuma.

RIP

View attachment 3330927
Hawa pamoja na wengine akina marehemu Armon Nsekela ndo walokuwa chachu ya maendeleo ya Tanzania.

Mkuu shukran sana kwa kumbukumbu.

Hawa walikuwa ndo katika makundi ya wasomi wa kwanzakwanza enzi hizo pamoja na wengine walokuwa wamepikwa khasa mashuleni, lugha fasaha ya kiingereza na kutojivuna sana.

Marehemu Mzee Joseph Namata alikuja kushika ukatibu mkuu kiongozi kutoka kwa mzee Dunstan Omary na kafuata mzee Dickson Nkembo alikekaa mwaka 1967 hadi 1974.
 
Back
Top Bottom