Tatizo kwa Sasa ni vigumu kumjua mpinzani wa kweli... Hata yeye anaangalia kushoto na kulia,anakwama...
Kuna mtu aliyetegemea mwanasheria msomi Kama Mzee Masumbuko Lamwai angerudi CCM??
Aliyewahi kusisimua upinzani wa miaka hiyo, na kufikia kuuambia umati wa aliokuwa akiwahutubia kuwa,... "...Kuwa mfuasi wa CCM ni sawa na kumchinja baba yako,na kuila nyama yake wewe mwenyewe...!!"
Au nani angetegemea sijui Waitara Mwikwabe wa Segerea angeweza toka upinzani? Sasa ni Waziri. Au nani angetegemea huyu DC wa Tunduru, Wala usingeweza kuota kuwa angetoka upinzani.
Na masuala hayo usiyachanganye na Zitto, Zitto ni mtu tofauti sana na wanasiasa wengine wote. Yeye huwa anataka faida,umaarufu,na kila jema yeye binafsi... Yaani Yule anapenda u-mimi sana.
Ni sawa na Nyerere,alifikiria kwa miezi mingi tu anamwachia Nani urais, na awe mtu ambaye, hata Kama Yuko nje ya ikulu,ataendelea kumtii yeye.. na hata unakumbuka,aliamua kubaki kuwa mwenyekiti wa chama,ili aendelee kuwa na nguvu.
Sasa Zama hizi, ni tofauti zaidi, upinzani umebanwa,umeminyika haufai... Hakuna fikra changamfu zinazozalishwa vyuoni kutokana na utawala wa awamu ya 5 kuvibana vyama vya upinzani kufanya shughuli zake.
Zamani ukimsikia mtu haendi kupiga kura, na hana sababu ya maana, unamwangalia, unamchukulia Kama mwenye uelewa mdogo, au anayesema atakayepita yeyote ndiyo huyohuyo, tulikuwa tunamchukulia Kama punguani. Lakini Sasa,mtu anayeenda kupanga foleni , ndiyo tunamshangaa na kuhisi labda hayuko timamu kiakili..
Awamu hii kiufupi inampitisha kwenye Moto mkali sana Mbowe ni vile uelewa wa siasa za nchi hii kwa baadhi yetu ni mdogo.
mimi ni Chadema lakini kuna tatizo kwenye chama lazima viongozi wajitafakari ikiwemo mbowe