Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Huyu mzee bana! Mbona wakati rafu zinafanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa alipiga kimya kama haoni kinachoendelea, leo maslahi yake yameguswa anakuja na blah blah kibao! Never trust this politicians.
 
Huo ni msemo wa KISWAHILI tu,ni kama vile kusema nyani haoni kundule,sio tusi.Tafasiri na upotoshaji.
Unamaana nzuri tu na inayoeleweka.......alikuwa anazungumzia baada ya kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa taifa,then Mbowe kwa namna nilivyoelewa huo msemo sumu haionjwi kwa ulimi,it means alikuwa anawatisha........then mzee naona anazidi kujidhalilisha tu
 
Atulie sasa aendelee kula posho ya wastaafu.
 
Tatizo kwa Sasa ni vigumu kumjua mpinzani wa kweli... Hata yeye anaangalia kushoto na kulia,anakwama...

Kuna mtu aliyetegemea mwanasheria msomi Kama Mzee Masumbuko Lamwai angerudi CCM??
Aliyewahi kusisimua upinzani wa miaka hiyo, na kufikia kuuambia umati wa aliokuwa akiwahutubia kuwa,... "...Kuwa mfuasi wa CCM ni sawa na kumchinja baba yako,na kuila nyama yake wewe mwenyewe...!!"

Au nani angetegemea sijui Waitara Mwikwabe wa Segerea angeweza toka upinzani? Sasa ni Waziri. Au nani angetegemea huyu DC wa Tunduru, Wala usingeweza kuota kuwa angetoka upinzani.

Na masuala hayo usiyachanganye na Zitto, Zitto ni mtu tofauti sana na wanasiasa wengine wote. Yeye huwa anataka faida,umaarufu,na kila jema yeye binafsi... Yaani Yule anapenda u-mimi sana.

Ni sawa na Nyerere,alifikiria kwa miezi mingi tu anamwachia Nani urais, na awe mtu ambaye, hata Kama Yuko nje ya ikulu,ataendelea kumtii yeye.. na hata unakumbuka,aliamua kubaki kuwa mwenyekiti wa chama,ili aendelee kuwa na nguvu.

Sasa Zama hizi, ni tofauti zaidi, upinzani umebanwa,umeminyika haufai... Hakuna fikra changamfu zinazozalishwa vyuoni kutokana na utawala wa awamu ya 5 kuvibana vyama vya upinzani kufanya shughuli zake.

Zamani ukimsikia mtu haendi kupiga kura, na hana sababu ya maana, unamwangalia, unamchukulia Kama mwenye uelewa mdogo, au anayesema atakayepita yeyote ndiyo huyohuyo, tulikuwa tunamchukulia Kama punguani. Lakini Sasa,mtu anayeenda kupanga foleni , ndiyo tunamshangaa na kuhisi labda hayuko timamu kiakili..

Awamu hii kiufupi inampitisha kwenye Moto mkali sana Mbowe ni vile uelewa wa siasa za nchi hii kwa baadhi yetu ni mdogo.
mimi ni Chadema lakini kuna tatizo kwenye chama lazima viongozi wajitafakari ikiwemo mbowe
 
Hahaha alitafuta madaraka ili awe na influence ndani na aibomoe CHADEMA, kakosa madaraka na kashindwa kuibomoa, lengo halikutimia na hakuwa na cha kufanya zaidi hivyo kujitoa.

Ushauri kesha utoa, ataishauri nini tena CHADEMA .

Nafasi ya kuwashauri alikuwa nayo, kaikimbia sasa atawashauri vipi naye siyo mwanachama wao tena?
 
Katiba ya chadema ndiyo inasema hiki ulichokiandika?

Mnaoishi mjini kwa kulamba viatu vya Mbowe acheni ujinga.
We vipi,Nani kakwambia naishi mjini?,Nani kakwambia Mimi chadema?,
Pamoja na kwamba Mimi Niko ccm,it doesn't mean that am an idiot,
I see things,I hear things and I translate them into what they are,,,
I don't hallucinate like you,I don't depend on politics in case you are wondering
 
Maneno ya Mr O yamenifikirisha,kama mwenyewe kapigwa mkwara itakuwaje kwa hao vidampa?

Ben alikuwa hapatani na Mbowe miaka yote kisa mjuaji na haaminiki na alikuwa anaundiwa zengwe anakatwa kwenye nafasi yoyote anayogombea kwa maagizo kutoka juu,ghafla et akawa msaidizi wa Mbowe na hapohapo akapotea.

"Put your friends close and your enemies closer"

Itakuwa imetumika hapa!!

BTW:Historia itakuwa upande wa Dr Slaa aliyeambiwa,"time and tides wait for nobody"
 
bagamoyo,
Anadai kaambiwa sumu hailambwi....

Yaani nimecheka ile mbaya, kuambiwa sumu hailambwi kajitoa cdm, kwa hiyo na yeye angemwambia ataoionja sumu Mbowe angegoma kugombea? Mjinga sana huyo mzee.
 
Cheo ni sharti la lazima kwake!
Wamemmwaga anatapatapa!!
 
Nahisi walizoea vile vyeo vya kuteuliwa, mikiki ya kugombea hawawezi.

Hii inaonyesha hata uwaziri mkuu ungekuwa unagombewa asingeshinda.

Kaguswa kakimbia, angechubuliwa nadhani angekuwa ICU sasa hivi.
 
Haya semeni tena wajinga na manyumbu mnaeburuzwa na Mbowe! Tukiwaambia mbowe anahusika na zile risasi za Lisu mtabisha, sasa mmeona? Mbowe ndiye mmliki wa chadema hakuna wakumtoa pale yyte anaetishia nafasi yake anamng'oa mapema mfano mzuri ni tukio la Lissu, Chacha Wangwe na Zito ongezea na hili la Sumaye.

Nawahakikishia chadema inakufa kifo kibaya na muuaji wake ni Mbowe! Mwakani mkipata hata viti vitano vya ubunge utakuwa ni muujiza wa kugeuza maji kuwa diesel .
 
namtakia safari njema katika maisha yake anayo ya Anza nje ya CHADEMA.
 
Back
Top Bottom