Mzee Frederick Tluway Sumaye ajiondoa CHADEMA. Asema mambo yamembadilikia CHADEMA baada ya kuchukua fomu kugombea Uenyekiti Taifa

Haahhhahah. Mimi siogopi matusi. Huwa natukanwa sana humu. Kasema atakuwa mshauri wa chama chochote including Chadema. Tanzania hakuna upinzani. Yaani waruhusu mgombea binafsi na sisi tugombee.
Nani aruhusu mgombea binafsi?
 
Aisee - umemaliza kila kitu ni kweli kabisa - CHADEMA HAKUNA DEMOKRASIA WALA MAENDELEO. Nimeongeza sauti. Inasemekana Lowassa alitoa "Mlungula" kwa "MMILIKI" wa CHADEMA.
Umeona eeeh. Hivi vyama vyote ni upuuzi tu. Waruhusu wagombea binafsi. Mtanzania awe na haki ya kugombea bila kupitia chama chochote. Tuwe huru. Kugombea na kuchagua. Hii ndo demokrasia ya kweli.
 
Alipogusia Mashamba yangu yamenyang'anywa ndipo paliponifurahisha
 
Chadema mmetuvuruga sana!! Tulikuwa tunawaamini sana!! Sasa ni bora kulima kuliko kushabikia siasa!!!
Nashukukuru kwa kunihakikishia kutopiga kura tena maishani.
 
Bora amejiuzulu wenzie walifukuzwa Kama mbwa.. na wengine kufa kwa utata... Kumbuka mwenyekiti anasimamia mamilions ya ruzuku achilia mbali pesa za wabunge, misaada na michango ya wahisani. Pale Kuna Vita ya masilahi ndugu zangu... Ni Vita ya kifo
Kama hao wanaokufa kwa utata unadhani kwa nini polisi hawafanyi uchunguzi kwa mbowe na CDM ili kuupata ukweli na kumfunga mbowe ambaye anaonekana kutonunulika na ccm?Polisi jinsi wanavyochukia upinzani wangeacha kufuatilia hao unaoita wenye vifo tata?Na je vipi Mzee mtikila,Akwilina,Ben saa nane,Mawazo,Lissu,Karume,sokoine,mwakyembe,Magufuli,na wengine wengi nao ni mbowe alitaka kukatisha uhai wao kwa kuwa wanaitisha nafasi yake?Kama ni hivyo huoni wajibu wa polisi wa kulinda raia na mali zao wameshindwa?polisi kama wameshindwa wewe unakuja unatokwa na utoko hapa wa kipuuzi?
 
Maneno ya mkosaji.
 
Hata hivyo CHADEMA ilikuwa MOVEMENT ya vijana, raia wanaoamini katika mbadala wa CCM sio bendera na/au mabwanyenye waliokataliwa katika chaguzi na figusi za MaCCM… Chama lazima kirudi huko.

Hata Rais Magufuli alisema anaogopa kukutana na viongozi wa upinzani kwasababu wamesema wakikutana naye watamnyonga wamtumbukize baharini, kama unaamini ya Sumaye unashindwaje kumuamini Mh. Rais.

Kwenye Siasa Ukikubali Mshindani Ama Hasimu Wako Akupangie Safu Ya Uongozi Basi Ndiyo Mwanzo Wa Kuondoka Katika Siasa Za Ushindani, Kwani Hakuna Mshindani Anayetaka Kushindana Na Mtu Ama Taasisi Thabiti Na Imara.

Kuna vitu vinafikirisha sana hasa kwa sisi watu wazima ambao tunajua haya mambo,watu wanadhani suala la uongozi ni kukurupuka tu na unakuwa kwenye nafasi kwa kuwa tu ulipotoka ulikuwa na cheo,hapana amekosea na ameoneshwa hali halisi ya maisha.Angetulia tu dawa imuingie vizuri.

Kwamba unaweza kutoka CCM mwaka 2015 na kujiunga Chadema, halafu baada ya miaka minne ukatosha kuwa Mwenyekiti wa Chadema iliyoanzishwa mwaka 1992? Mbona ni utani sasa!

Kwasasa interejensia ya chadema ni kubwa sana.

Nimependa na ndio chama kinapaswa kuwa hivyo.

Chama kinatakiwa kijitathimin San pamoja na kua na mamluki wanatakiwa wakirudishe chama kwa watu sio kujifanya chama chao.

Kwasasa CHADEMA wamejifunza makosa waloyafanya kwa Lowassa?

Kwa Hiyo Tunakubaliana Kuwa Chama cha Upinzani Tanzania ni CHADEMA, Angalia Namna Kinavyotafutwa Kushughulikiwa Kutoka Kila Kona, Ushawi Sikia Uchaguzi wa Jahazi Asilia, PPT-Maendeleo, CHAUSTA au Demokrasia Makini? Msajili Ashawahi Japo Kuvitaja?

Hongera Sana Chadema mmefika hatua nzuri keeping moving.

Mr yamoto mtoto wa Mr mkiki.
 
Wachache sana wanye uelewa wako tatizo la wengi wako kimuhemuko zaidi humu kwasababu ya mtu fulani Elungata,
 
Mzee Sumaye ulipigiwa kura, kushinda na kushindwa ni harakati za uchaguzi. Unadai wajumbe waliwekwa hotelini na walipewa rushwa. Kwa mwanasiasa mkomavu kama wewe haya yalikuwa ya kuzungumzwa kwenye kikao cha kamati kuu na hoja yako isikilizwe.

Heche na Mwambe ni wana chama wa muda mrefu kuliko wewe. Kwanini hawajajivua u wanachama baada ya kukosa kiti cha kanda. Mzee unatufundisha nini sisi wachanga kwenye siasa? Kuwa ukishindwawuchaguzi unajivua u wanachama.
 
Chadema ulikuwa enzi za Dr Slaa. Kwa sasa wamebaki nyoka wa kibisa tu.

Ccm ilikuwa enzi hizo za Nyerere. Kwa sasa limebaki genge la mafisadi na wahuni tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…