Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Sina wivu ila natumia akili za kawaida kabisa. Sigomi ila nagomea kudharaulika, si dharau ila nachukia kisahauliwa, napingana na kupendelewa kusiko na tija.

NIHIVI;
Sitaki wote tule tembele ila sikubali pale tembele zinapotumika kufunika nyama ili iive vizuri na kisha tembele litupwe! Ndio namaana moja, huyu halali nje, hakai nyumba inayovuja, habanwi kutokana na udogo wa eneo lake kuwa Dogo.

Kwanini tumpe mtu Nyumba ambayo hataishi humu wakati kuna shule hazina vyoo, madawati, maabara, walimu, vitabu vya kiada na ziada. Kwani hii keki ya Taifa tusiigawane wote hata kama sio nusu kwa nusu basi walau robo nasi tujilambe lambe...
 
Toka lini "Wanasiasa" wakawa na roho za huruma na upendo?
Kitu cha kwanza unapaswa kuwaelewa Wanasiasa, wote ni waongo, ni wanafiki na wamejaa tamaa na ubinafsi. Kikwete siyo wa tofauti hao.
Politicians are devils in sheep's skin. Hakuna hata mmoja wao mwenye utakatifu, even the late JKN was a devil too.
 
Sikiliza wewe tahira!

Sheria mbovu inafutwa siyo kuonewa aibu!

Kwa hiyo hao watangulizi wa jiwe walipaswa kuifuta siyo kuionea aibu.
Kwamba watangulizi wa Jiwe ndio walipaswa kuifuta ila Jiwe hakupaswa kuifuta?
Ni bora walioifumbia macho au aliyedemka kuwajengea Kwa kasi mpaka JK akaomba ijengwe taratibu?
Hili ni jambo la kikatiba sio sheria za kawaida za kumpelekea Ndugai abadilishe.

JK alianzisha mchakato wa mabadiliko ya katiba,bahati mbaya ukaishia Njiani, Jiwe alivyoingia badala ya kumalizia akasema iliyopo haina Shida na katiba mpya sio kiapaombele

Majuha Kama wewe ndio mlikuwa mnashangilia kila alichofanya Jiwe,akijamba mnapiga makofi,akitukana makofi,akiwaita wanyonge ndio kabisa mnanengua Kwa kubinjua makalio.
 
Kumbuka kuna nyumba za serikali pia waliuziwa. Nakumbuka JK yeye aliuziwa ile ya pale Migombani street kama unaenda kwa Kariuki hosp kwa kutokea ubalozi wa Marekani ( mikocheni) hiyo nyumba iko ndani ya viwanja viwili vya low density ambavyo zilikuwa nyumba mbili wakiishi familia mbili lakini ziligeuzwa plot moja , ndipo alipojenga nyumba mpya baada ya kuvunja zile zilizokuwepo. Kwa Dsm hapo ndipo anapoisbi kabla ya kujengewa hii ya sasa.
 
Sheria ngapi alizivunja wazi wazi zenye maslahi Kwa umma,hiyo ya hovyo ndio akaona atekeleze?huo ndio unafiki wake, anajifanya Kiongozi wa wanyonge Kumbe anawanyonga ili marajiri wapate mahekalu zaidi
I agree Mkuu,wanatukosea sana watu hawana ajira,mishahara midogo lakini vyote si kipaumbele,nilichokisikia nikacheka ni kujengewa nyumba yenye hadhi ya raisi,kumbe nyumba zinatofautiana hadhi,Lakini I stand to my point Sheria ifutwee.
 
Sasa mbona hawa mataga wanamlaumu Samia?
Hapa hatulinganishi watawala, tunazungumzia kuhusu matendo yao yote yasiyo na aibu ya Ulafi.

Kikwete ana Lijumba Msoga na hapa Dar es salaam maeneo ya Mikocheni ana Jumba, Halafu eti akajengewe Lihekalu Likubwa namna hii kwa kodi za wananchi, naye haoni aibu kulipokea huo ni Ulafi, Ubinafsi na Tamaa kupitiliza!.
 
Lile katu hawezi kurudisha. Uzuri wote ule, kaleni nyasi lazima Hekalu lijengwe na amepewa.
Watu waroho! Utajiri wote bado Hana huruma ya kukwapua majumba....

Ninachosema ni kuwa, Kama uko kwenye nafasi ya kuiibia serikali, Iba Sana na wewe, maana Hawa wamejihalalishia wizi kwa kuzitungia Sheria za kuhalalisha kuiba Mali za umma.
 
Hana watoto na ndugu wengine? Je nyumba hairuhusiwi kupangishwa au kuwa hotel nk? Ni mali ya umma au yake binafsi?
 
Magu aliwajengea hayo mahekalu kuwazima midomo kwa hekalu kuu alilojenga kijijini kwake Chato,haihitaji akili kubwa kujua hili
 
Why Kikwete? Mzee Mkapa alikuwa hana nyumba? Mzee Mwinyi hakuwa na nyumba na uwezo? Bottom line ya uamuzi huu ni sheria. Nilitegemea mleta hoja ajadili sheria siyo nyumba ya Mzee Kikwete. Kikwete hakuamua wala kuomba Serikali imjengee nyumba.

Guys let's be fair! Huyu mzee wa watu ana kosa gani? Kama great thinkers tuchambue sheria siyo kumjadili Kikwete na nyumba ambayo kajengewa enzi za Rais wetu aliyetutoka JPM. TUACHE KUENEZA CHUKI, SISI NI TAIFA
 
Mkuu, mimi nashangaa sana watu kusupport sheria hizi za hovyo ambazo watu wanajitungia ili kujinufsisha wao binafsi. Kikwete bila aibu anadai ni kwa mujibu wa sheria. Sasa kama ndivyo hivyo mbona hskuwajengea Mkapa na Mwinyi....!!?

Hizi sheria mbovu walizojitungia ni muda Sasa inabidi zibadilishwe. Imajine mama kila siku alikuwa ikijitapa na bunge la katiba lilivyompsidha.... Kaingia kwenye kiti kikuu kasahau anaanza kutwa bia katiba mpya tusubiri kwanza as if kuna kubwa analolifanya litakalozuia katiba mpya kwa Sasa.
 
Why Kikwete? Mzee Mkapa alikuwa hana nyumba? Mzee Mwinyi hakuwa na nyumba na uwezo? Bottom line ya uamuzi huu ni sheria. Nilitegemea mleta hoja ajadili sheria siyo nyumba ya Mzee Kikwete. Kikwete hakuamua wala kuomba Serikali imjengee nyumba.

Guys let's be fair! Huyu mzee wa watu ana kosa gani? Kama great thinkers tuchambue sheria siyo kumjadili Kikwete na nyumba ambayo kajengewa enzi za Rais wetu aliyetutoka JPM. TUACHE KUENEZA CHUKI, SISI NI TAIFA
 
Kosa la Kikwete.

1. Kukubali kujengewa hiyo nyumba wakati hana uhitaji wa Nyumba, anayo majumba mengi tu tunayoyajua, bado anayo marupurupu mengi tu ambayo bado ananufaika kutokana na jasho letu wananchi ikiwemo kulipwa asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani

2. Alipokuwa rais hajawahi kuifuta au kuirekebisha hiyo sheria.

3. Kuipokea nyumba ya Mabilioni ya fedha na kuifanya yake binafsi , huku akijua nchi hii ni masikini vya kutisha, hospitali zinapungukiwa dawa, watu wana shida ya maji, shule hazina madawati, hilo lijumba lingesaidia kupunguza adha hizo za wananchi.

Tunajua kuwa hata marais wenzie wastaafu walijengewa mikasri wakati hawana uhitaji nayo nayo ni makosa pia, ni unyonyaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…