Mzee Jakaya Kikwete, rudisha hilo hekalu Serikalini lipigwe mnada pesa zisaidie wananchi

Subutu, anaanzia wapi rudisha hekalu Mzee wa msoga ? Nchi za kiafrika Zina Mambo ya ajabu Sana, kwamba leo mtumishi anaelipwa mhaara wa chini Sana hubatika kujenga kibanda Cha kujiegesha ila aliwai kua rais , anashindwa mpaka ajengewe na serikali ,tz top ten kwenye kwenye uongozi ata wanapostahafu ndo wanatafuna hii nchi asikwambie mtu , unalipwaje 80% ya mshahara wa Alie madarakani , na hii sio kwa rais bali Hata Wengine wanalipwa vizuri Sana ,
 
Ndio maana nikakuita taahira!

Usifikiri kuna mtu unamkomoa hapa! Wanaoumia kwenye huo ugawaji wa mijumba na magari ni babu, bibi na ukoo wako waliotopea kwenye umasikini kule kijijini.!

Kama KIKWETE na watangulizi wengine wa jiwe waliionea haya hiyo sheria badala ya kuifuta usifsnye wao wawe ndio wasafi kama unavyotaka kutuaminisha hapa.

Mnatetea hata mavi eti kisa jiwe!
 
Nyerere alijengewa, Mwinyi alijengewa, Mkapa alijengewa na Kikwete amejengewa. Hata JPM atajengewa.

Hayo ni marupurupu ya kazi ngumu ya urais waliyoifanya. Huwezi kujua mangapi magumu wamepitia kutupambania sie raia mpk wanatoka madarakani. Hata hiyo nyumba ni kitu kidogo sana kwa kazi ngumu waliyoifanyia TZ.
 
Mama maria nyerere anastahili kujengewa alikabidhiwa lini nyumba hapo Dar au gari?
 
Bado tena why Kikwete? Kwa nini humtaji Magufuli kwamba kwa nini yeye hakuifuta na bado akaitekeleza? Na yeye atajengewa.

Pili, kujadili angekataa bado pia narudia tena Why Kikwete? Mzee Mkapa alikuwa na nyumba Lushoto na eneo kubwa tu. Dar pia anayo! Why Kikwete? Mzee Mwinyi pia ana eneo zuri Zanzibar na Dar pia! Why Kikwete?

Nimetoa mfano wa Wazee wangu Marais hao wastaafu si kwamba napenda, la hasha! Ni kuhoji huu msukumo wa kwa nini Kikwete nyumba aliyojengewa kisheria iwe nongwa? Pesa na mali zipi zenye ushahidi ambazo JK anazo? Hiyo pensheni ya asilimia 80 ya mshahara wengine pia wanalipwa, why Kikwete?

Jukwaa hili kama ni la great thinkers tujadili issues. Narudia tena, tujadili sheria.

SISI NI TAIFA.
 
Ulitaka nimuandikie Mkapa na Magufuli barua ya wazi, wataisoma?, wataweza kufanya ninachoomba kifanywe ndani ya hii barua ya wazi?
 
Nyumba hii nadhani ni stahiki kwake JK kama zilivyo stahiki za watu wengine ambazo huwa wanalipwa baada ya kuwa wamestaafu kazi. Unapomshauri apige mnada nyumba hii, ni kama kunishauri mimi nitoe maslahi yangu kwa umma baada ya kuwa nimestaafu. Unachomshauri JK kinaondoa maana halisi ya mtanzania kustaafu akiwa Rais, na vile vile kinapelekea kupotea kwa mantiki ya mtanzania kuitumikia nchi yake katika ngazi hiyo ya urais
 
Acheni roho za korosho kapewa kwa mujibu wa sheria unataka nendeni mkabadili na JPM anapewa. wakati marehemu Mkapa anapewa ulikuwa wapi kumwambia haya?
 
Vipi Mwinyi na yeye hawezi kusoma?
Mwinyi anaweza kusoma, lakini kabla hajajibu anaweza kusahau niliuliza nini, kwa hiyo nimemwandikia Jakaya ujumbe mpana ufike kwa wastaafu wote waliohai, wale ambao wako madarakani kwa sasa na watakaofuata huko mbeleni.
 
Ulitaka nimuandikie Mkapa na Magufuli barua ya wazi, wataisoma?, wataweza kufanya ninachoomba kifanywe ndani ya hii barua ya wazi?
Kwani hiyo nyumba imeanza kujengwa mwezi huu? Mkapa kakabidhiwa baada ya kufariki au kabla? Why hukumuandikia hii barua akiwa hai? Why hukuandika hii barua pale Hayati mpendwa JPM alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa hii nyumba ya JK na kuagiza ijengwe haraka?

Ada ya mja hunena muungwana ni vitendo, kubali presentation ya hoja yako imemiss point kuu ambayo ni sheria. Jadili sheria. Muache Mzee Kikwete.
 
Mzee JK kama utapitia huu uzi wala usiumize kichwa kuna binadamu tumeumbwa na roho mbaya na uhasidi tu ingekuwa yeye kapewa angepiga mnada? watu wanaongea kwa sababu hawajapata hiyo nafasi lakini hakuna mtu hata mmoja Tanzania hii apewe nyumba tena kisheria halafu aseme hapana naiuza mnada isaidie watu maskini. labda Mama Thereza. tuache roho mbaya na unafiki. Mzee haijaiba iba kapewa ni haki yake.
 
Acheni roho za korosho kapewa kwa mujibu wa sheria unataka nendeni mkabadili na JPM anapewa. wakati marehemu Mkapa anapewa ulikuwa wapi kumwambia haya?
Mkapa ni marehemu, angekuwa hai huku ana afya njema naye tungemueleza.

Mzee Mwinyi sikumueleza ujumbe huu kwa sababu ana ugonjwa wa kusahau, huenda keshasahau kama hata naye alipewa kasri.

Halafu usilete habari za sijui roho ya korosho au kitu gani. Sisi tunamaindi kuona kodi zetu zinatumika Kiulafi

Hawa watu wana everything including hiyo mijumba, wanahitaji nini cha ziada zaidi ya kututwisha zigo sisi wananchi kugharamia mihekalu kama hiyo wakati tuna shida kibao za mambo ya msingi including upungufu wa madawati, dawa, shule, maji safi na salama etc!
 
Mwinyi anaweza kusoma, lakini kabla hajajibu anaweza kusahau niliuliza nini, kwa hiyo nimemwandikia Jakaya ujumbe mpana ufike kwa wastaafu wote waliohai, wale ambao wako madarakani kwa sasa na watakaofuata huko mbeleni.
Unapoteza uhalali wa madai yako, kwasababu hata JK siyo mwenyekiti wa marais wastafuu. Vile vile kama ambavyo wewe unadai Mwinyi hawezi kukuelewa, atamwelewaje JK?
 
Mkapa ni marehemu, angekuwa hai huku ana afya njema naye tungemueleza.

Mzee Mwinyi sikumueleza ujumbe huu kwa sababu ana ugonjwa wa kusahau, huenda keshasahau kama hata naye alipewa kasri
Kwani Mkapa alipewa yuko kaburini? si alipewa hai mlikuwa wapi. Jiulize ingekuwa wewe umepewa stahiki yako ungeipiga mnada au kuikataa? Jiulize kwanza wewe, sisi ni rahisi kusema lakini hakuna hata mtanzania mmoja akataa stahiki yake na wengine hata kama sio stahiki yake atachukuwa. wangapi Tanzania hii watafanya unayoyataka wewe JK afanye.
 
wakati mwingine tunatafuta vidonda vya tumbo bila sababu hili swala lipo kikatiba na wabunge wetu tuliowachagua sisi sasa tabu iko wapi?
hata hivyo turudi nyuma kazi ya urais sio kazi ndogo hailingani na nyumba walizojengew very risk kuwawa njenje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…