Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Unfortunately kwa katiba yetu ilivyo, DPP hashinikizwi. Ukiona DPP anashinikizwa huo ni uvunjwaji wa katiba mwingine tunaoukataa.Ukiondoa wanao mshikilia sidhani kama kuna mtu ambae hataki Mbowe atoke. Tofauti ni namna atakavyotoka. Chama chake kinasema kwa sababu hajafanya kosa lolote basi DPP atangaze tu kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hivyo ataachiwa. Wengine wanasema kuwa aombe msamaha tu hata kama anajua kuwa hajafanya kosa ili atoke. Shida ya kuomba msamaha ni inamaanisha umekiri kuwa umetenda kosa uliloshitakiwa. Kwa sababu hiyo Mbowe atajulikana kuwa ni gaidi kwa kwenda mbele. Sidhani kama kuna watu wanakataa watu kufanya wanaloweza ili Mbowe aachiwe mradi tuu hawamlishi maneno kuwa ameomba msamaha. Ingekuwa hawataki atoke wasingefanya jitihada kubwa kuomba mataifa ya nje kuishinikiza serikali imuachie Mbowe. Au wasingeendelea kupaza sauti kuwa " Mbowe sio Gaidi".
Amandla...
Kwa nini tusiache mahakama ifanye kazi yake na kama hana hatia mahakama itamuachia tu. Au hatuna imani na mahakama?