Watanzania wengi ni watu wenye uelewa mdogo sana wa mambo. Kwa kutumia mwanya huo ndio maana CCM inaendelea kutawala nchi hii wanavyotaka.
Unashangaa watu wengi wanamsifia sana Kikwete na kumuona mtu wa aina yake na aliefanya mambo makubwa nchi hii lakini ukweli ni kwamba Kikwete kaliingiza hili taifa kwenye matatizo makubwa kuliko mazuri machache aliyoyafanya.
1. Kikwete ndio sababu nchi hii haina katiba mpya. Kumbuka alianzisha mchakato wa katiba mpya kinafiki halafu siku ya ufunguzi wa bunge la katiba akaponda maoni yaliyotolewa na wananchi kwa maslahi ya chama chake.
Hili tu lilipasa kufuta jambo zuri lolote alilolifanya Kikwete nchi hii. Watu wanalalamika Kwamba Magufuli alikua mbaya, kama tungepata katiba mpya labda Magufuli alingechaguliwa ama asingeongoza nchi anavyotaka.
2. Kikwete ndio alikuwa anasaini mikataba ya hovyo kama Dowans, Symbion nk ambayo haina exit clause. Nasikia hao jamaa wamelipwa zaidi ya Bilioni 500 za walipakodi masikini wa nchi hii.
4. Leo namuona Kikwete kama kiongozi wa waangalizi wa uchaguzi wa Afrika Mashariki huko Kenya anashauri ambae hatakubaliana na matokeo aende mahakamani huku yeye alishindwa kututengenezea hayo mazingira kwa maslahi ya chama chake.
Binafsi sioni kwa nini Kikwete anasifiwa, hastahili hata chembe ya sifa moja.
Yapo MAZURI alifanya, upinzani ulishamiri , alisaidia kutatua Mgogoro wa KISIASA KENYA, pesa mtaani ilipatikana chafu na safi. nk,nk.
Bt sitomsahau Kwa haya;
1. Kuuvuruga mchakato wa KATIBA.
2. Kupromote wanawake ktk uongozi wake, Hadi akasaidia sa100 Jina lake kuchomekwa kiaina.
3. Nchi ikifika mahala ikawa ghala la kutunza na kusambaza mambo ya USINGIZI Kwa vijana. Walilala sana sana.
4. Gasi iliuzwa mara mbili Kwa WATEJA tofauti, na mikataba mibovu kibao, ufisadi ulitamalaki. Richmond nk.
5. Mikopo ya wanafunzi vyuo vikuu iliongezeka, degree zilijaa mtaani, bila kisahau vyeti feki.
6. Mabomu yalilipuka mbagala na yalijirudia tena.
7. Awamu yake ya pili, chama kilichukiwa kiasi kwamba viongozi waliogopa kuvaa sare za Chama Kwa kuhofia kuzomewa .
8. Udhaifu wa Serikali yake ulilazimika watuletee Dictator. Ni Yeye!!!!
Tunashukuru Kwa muda wake. Aje tu DICTATOR mwingine, maana Awamu ya 4 na 6 ni kama zinafanana.
Ameeen.