Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ameyasema hayo kwenye kongamano la viongozi wa Africa katika kuadhimisha miaka 20 ya Kamisheni ya Amani ya AU Mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Sitaki kuongeza maneno, mwenyewe huyu hapa
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema miongoni mwa sababu za kuwepo kwa migogoro kwa nchi za Afrika ni kutozingatiwa kwa miongozo ya uwepo wa uchaguzi ulio huru na wa haki.
Kikwete ameyasema hayo leo Mei 25, 2024 jijini Dar es Salaam katika mjadala uliokuwa sehemu ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 20 ya Baraza la Aamani na Usalama la Umoja wa Afrika (PSC).
Amesema migogoro mingi ya ndani ya nchi za Afrika inahusiana na upungufu wa kiutawala.
“Inaweza kuwa demokrasia, ambapo inafikia watu wanakosa imani na demokrasia, kunakuwa na chaguzi ambazo hazijaratibiwa vizuri.”
“Aliyeshinda hatangazwi na aliyeshindwa anatangazwa kuwa mshindi. Yote ni kwa sababu ni upungufu wa kiongozi, kukosekana usawa, ubaguzi, ukabila na upendeleo,” amesema Kikwete.
Amesema watu wanapokosa haki zao huamua kuzipambania na ndipo inapozuka migogoro.
Mwananchi
Toa maoni yako