Pre GE2025 Mzee Kikwete asikitishwa na Migogoro ya Uchaguzi adai aliyeshinda hatangazwi aliyeshindwa anatangazwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kikwete ana la kujitetea. Aliharibu mchakato wa katiba mpya kwa hotuba yake ya upande mmoja kwenye bunge la katika. Yeye angewaachia wajumbe waamue na sio kuonesha msimamo wake. Pia kitendo chake Cha kutuma jeshi Zanzibar kwenye uchaguzi wa 2015 ilikuwa ujinga wa Hali ya juu. Vuai na CCM yake walikuwa wameitisha conference na kupinga matokeo ya kushindwa, ghafla jeshi likaongezwa Zanzibar na Jecha akazungukwa na wanajeshi na kushindwa kumtangaza Maalim Seif kuwa Rais. Mwisho wa siku wakatafuta sababu za kijinga eti wajumbe hawaelewani na maalim kajitangaza mapema.
 
Ni kipindi cha JK ndipo tumeshuhudia idadi kubwa ya wabunge wa upinzani bungeni (Kambi imara ya Upinzani)........kwenye hili hongera, kwa kiasi kikubwa JK ni mwanademokrasia

japo kwa Zanzibar ilikuwa tofauti labda kwa kuwa miaka nenda rudi Zanzibar ni koloni la Tanganyika uchaguzi wa 2015 angetangazwa alieshinda Maalim Seif ingeleta shida kwenye issue ya muungano
 
Wapi kasema uongo? Yeye alikuwa Rais wa nchi kwa miaka 10 mfululizo kwahiyo anajua yote haya aidha alipokuwa mamlakani ama hata baada ya kutoka maana ana vyanzo vingi na vya kuaminika vya kumpa taarifa.
Ni mnafiki tu. Katuma jeshi Zanzibar 2015 kuzuia Maalim asitangazwe. Na kweli hakutangzwa.
 
Kwanini iwe shida?. Ule ulikuwa uhuni.
 
Kikwete alivyo mnafiki ataandika kitabu akiomba Radhi kuzuia Maalim Seif Kutangazwa Rais wa Zanzibar 2015.
 
HUYU NINACHOCHUKIA NI KUWA NI MNAFIQ NA HANA AIBU KABISA.YAANI UNAFIQ UPO DAMUNI.NI SEHEMU YA MAISHA YAKE
 
Kosa lake lipi hapo kwa kauli hiyo hadi mumtukane?
Jamani jifunzeni kutafakari kilichosemwa siyo chuki dhidi ya mtu.
Huu ni nwanzo mzuri hata kana huko nyuma hakuyazingatia hayo.
Kikwete ni sehemu ya mifano hai ya chaguzi za kishenzi hapa barani Africa. Kama anachokisema anamaanisha angekuwa anajitokeza kutaka tume huru ya uchaguzi dhidi ya chama chake. Kinyume na hapo ni kutaka sifa zisizo na tija kwa kufurahisha genge.

Mikutano ya aina hiyo huwa naiona haina tija, maana watu hushiriki kuongea mambo wasiyoyatekelaza Wala kuyaamini.
 
Huyu Mzee ni snitch ndio maana aliwahi kukimbia kule Monduli kwenye chuo Cha kijeshi sababu ya unafiki.
Huyu angalau alijitahidi tulikuwa na bunge imara lenye kuibua hoja nzito. Katika miaka yake kumi zaidi ya asilimia 60 ya watumishi wa umma wa sasa waliajiriwa. Ukimuona mtoto wa maskini ameajiriwa serikalini basi wengi wao ni kipindi chake.
 
Rais bila watu hakalii kiti hata kwa siku moja, atafurushwa tu.
Rais hutegemea kundi lililomzunguka na kumlinda (likiwa ovu, uovu utatamalaki na kinyume chake ni sawa).
Kwa hiyo, ni muhimu kujenga watu, jamii na taifa katika maadili kuanzia watoto badala ya kusubiri kutegemea mtu mmoja ambaye aweza kugeukwa na kufukuzwa na waovu wakiwa wengi.
Zipo (atake asitake za kimya kimya nyingi kuliko za wazi kama enzi za Magufuli) na Viongozi hukubaliana nazo vivyo hivyo kulingana na zilivyokuja.
 
Tusimubeze anao ushahidi, ameshiriki hili, walio nyanganywa ushindi wengine walikuwa marafiki zake, amewazika, watamzika waliobaki hai kama atawatangulia. Ni ujumbe kwa wasimamia uchaguzi wa leo/kesho kujisahihisha. Wezi wa jana kukemea wezi wa leo/kesho siyo vibaya.
 
Aiseeee
 
😆😆😆😆😆
 
Kwahiyo we mzee ndio unataka umuunge mkono mkojani ili akishindwa atangazwe mpinzani wake au!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…