Mzee Kikwete aweka rekodi sawa, Uchumi wa Kati waliopanga na Mkapa ni wastani wa dola 3,000 kila Mtanzania

Wacha wee! Leo hii hatimae imekuwa ni Zitto na gazeti la The Economist?! Na sio Eric Kabendera? Btw, kwani ni kipi kipya alichoongea JK ambacho huyo Zitto hakifahamu, hadi ionekane sasa Zitto ndo atatumia hiyo hoja kwa The Economist?!
Goodbye
 
Kwani hatujaingia tu uchumi wa Kati? Record ipi sawa alihoweka na akili zako hizo?
 
Hasa hasa anayefuata anapokuwa kilaza zaidi ya aliyepita,yaani wanaona Kama wameruka mkojo na kukanyaga kinyesi
 
Na hasa miongoni mwa hawa wawili, mmoja akiwa ni Makonda tutaufikia uchumi wa juu mapema zaidi.
Hapo tunahitaji marais wengine wawili kwa maana ya 20 yrs, hao kama wanatokea ccm
 
Mada inalenga kukebehi Serikali ya sasa kwa kumkariri Kikwete kana kwamba amekanusha yanayosemwa na Serikali. Mada inapotosha aliyoyasema Kikwete kuhusu mafanikio ya Serikali ya sasa ambayo wewe unayaita 'propaganda', kwa kumsingizia kwamba amekanusha yanayosemwa na Serikali. Ukweli wa mambo ni kama ifuatavyo.

Pato la wastani wa chini ya USD 1,000 huhesabiwa kuwa Low Income. Kuanzia USD 1,000 hadi USD 3,000 ni Middle Income; na juu ya hapo ni High Income. Ukiisha vuka USD 1,000 unaingia Lower Middle Income na ukikaribia kiwango cha juu cha USD 3,000 unahesabiwa kuwa kwenye Upper Middle Income. Malengo ya Serikali, tangu wakati wa Kikwete, yalikuwa kwamba ifikapo mwaka 2025 mosi, Tanzania iingie uchumi wa kati, yaani kuwe na pato la wastani wa zaidi ya USD 1,000; na pili, kipato cha wastani kiwe takriban USD 3,000.

Serikali ya Magufuli imefikia lengo la kwanza mwaka huu, ikiwa ni miaka mitano kabla ya tarehe iliyopangwa. Hatua hii ilitangazwa na World Bank yenyewe. Ni dhahiri kwamba mada yako inapotosha ukweli kwa kusema Kikwete amekanusha 'propaganda' za Serikali. Hakuna lo lote alilokanusha Kikwete. Yeye ameishia kutaja lengo la tangu Serikali yake ya kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. Serikali ya Magufuli imefanikisha hilo miaka mitano mbele na hilo likatangazwa na World Bank yenyewe. Hakuna cha propaganda hapo. Serikali iliendelea kusema kwamba kipato cha wastani, kufuatana na World Bank, ni USD 1,038. Wewe unamkariri Kikwete kwamba amesema Serikali inadanganya kwa kusema kiwango cha wastani ni USD 3,000. Serikali haijtamka hivyo. Mtu ambaye hakusikiliza hotuba ya Kikwete ataamini kwamba uyasemayo ni ukweli, ambapo si kweli. Tusubiri tuone kama lengo la pili la wastani wa mapato litafikiwa hapo mwaka 2025. Kwa kuangalia kasi iliyofikiwa katika miaka mitano tunayoimalizia, bila shaka lengo hilo litafikiwa pia. Mungu ibariki Tanzania na utulinde na habari potofu zinazoweza kuwaghafirisha wananchi.
 
Ukiona vyombo huru vya habari vinafungiwa ujue wanataka kutulisha matango pori kupitia Uhuru na tbc
 
We kichaa ni wakumfundisha JK kipi Cha kuzungumzia?
 
Mkuu ujenzi wa barabara ya morogoro hasa eneo la mbezi mwisho,Barabara zetu kujaa matuta,sheria za ajabu Kama matokeo ya urais kutopingwa popote nk ni moja ya indicators za ukilaza huo
Yani ulitaka barabara zisiwe na matuta?
Na kwamba hicho ndio kipimo cha ukilaza?
 
Mkuu 2025 development strategy ipo mtandaoni kwa nini usiisome ukajiridhisha?lengo mdogo wangu haikuwa kuingia uchumi wa kati tu bali kipato Cha USD 3000.00 Sasa tupo 1028.00 bado sana,na JK kamwambia bado sana shehe
Kwani Magufuli alisema anajivuna kwa kufikia malengo hayo ya dola elf 3 kabla ya 2025?
 
Usemi wake ni sahihi. Issue iliyoko sasa ni kuvuka/kuingia kwenye uchumi wa kati as a starting point. 2025 ni hatua ndani ya uchumi wa kati. Tupunguze viherere here. Pamoja
 
We hujaelewa
Ni kweli tumefikia Uchumi wa Kati, according to WB

Na kulikuwa na lengo limewekwa kuwa tukifika 2025 tuwe tumefikia Pato la 3000 kwa kila Mtz

Lakini ilivyokuwa inasemwa Ni kuwa Magufuli amelifikia lengo la Uchumi wa Kati kabla ya 2025,
lakini lengo lenyewe halikuwa just Uchumi wa kati Bali Uchumi wa Kati wa dola 3000 kwa Wastani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…