Nimesikiliza kipande kifupi cha hotuba ya JK ya leo, ama hakika Kikwete anazidi kuthibitisha umwamba wake kwenye fasihi.
Anakuwa shupavu wa muda wote, leo amepiga madongo makali sana kwa maneno mepesi. Nahisi upinzani pia uibe huu ufundi wa JK.
Nimefurahishwa sana pale alivosema target yake yeye na Mkapa ni uchumi wa kati wa per capita ya USD 3,000
Ameweka mzaa kidogo kwamba 'Kama Magufuli akichaguliwa tena, basi ifikapo 2025 basi pato litakuwa limefika USD 3000 kwa kichwa.
Kwa mahesabu yangu ya kiuchumi, ya haraka haraka, ili Tanzania ifikie pato la USD 3000 mwaka 2025 itabidi wastani wa ukuaji wa uchumi na pato la taifa uwe wa zaidi ya asilimia 22 kwa mwaka, na iendelee kuwa hivo kwa miaka minne ijayo.
Hapo ndo naona kwamba Kikwete ameamua kumzabua mtu risasi za moyo kwa kumpa target ambayo kamwe hawezi kuifikia hata robo yake. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba leo kuna mtu kavuliwa nguo hadharani. Aisee yule mkwere ni hatari, amedhihirisha kwamba yeye alizaliwa mjini Daslamu na atabaki kuwa hivo
| Year | 2020 | 2021 | 2022 | 2023 | 2024 | 2025 |
| Per capital GDP and projected | 1,080.00 | 1,317.60 | 1,607.47 | 1,961.12 | 2,392.56 | 2,918.92 |
| | | | | | |
| Required GDP growth per capita | | 22% | 22% | 22% | 22% | 22% |