Mzee Kikwete aweka rekodi sawa, Uchumi wa Kati waliopanga na Mkapa ni wastani wa dola 3,000 kila Mtanzania

Mzee Kikwete aweka rekodi sawa, Uchumi wa Kati waliopanga na Mkapa ni wastani wa dola 3,000 kila Mtanzania

Yani ulitaka barabara zisiwe na matuta?
Na kwamba hicho ndio kipimo cha ukilaza?
Mkuu Kuna nchi nyingine hapa duniani unaijua ambayo barabara zake zimejaa matuta Kama Tanzania?
 
Ungeangalia ile hotuba ya Dr. Mpango wakati anatoa hii habari ya kuingia uchumi wa kati ungejua sisi tunasema nini. Sasa kwa kuwa umekaa kusifia kuabudu kusujudu kutamka neno juhudi kama dozi ya TB basi na akili yako umeiweka mfukoni unatembea nayo!
Dr. Mpango alisema walipanga kufikia uchumi wa kati by 2025.

Kikwete anasema Mkapa aliweka lengo kwamba hadi kufikia 2025 tutangazwe uchumi wa kati tukiwa na dola elf 3 kama pato kwa kila mtanzania

Bank ya dunia imeitangaza tanznia kama nchi ya uchumi wa kati kabla ya 2025 kwa kutumia vigezo vyao.

Malengo ya kufikia pato la dola elf 3 kwa kila mwananchi bado yako pale pale na hakuna kiongozi yeyote wa selikali alishawahi kusema tumeshafikia lengo waliweka la pato la dola elf 3 kama yupo weka crip yake hapa.
 
Anajitapa kutufikisha uchumi wa kati kabla ya muda,yaani kabla ya 2025
Uchumi wa kati anatangaza Magufuli au bank ya dunia?

Kama wao walipanga kufikia uchumi wa kati kwa vigezo vya WB lakini wametangazwa kabla ya 2025 kwanini asijisifu?
 
Uchumi wa kati anatangaza Magufuli au bank ya dunia?

Kama wao walipanga kufikia uchumi wa kati kwa vigezo vya WB lakini wametangazwa kabla ya 2025 kwanini asijisifu?
Mimi nimesema ametangaza au anajitapa? Au kiswahili hujui mkuu?
 
Kikwete naona kaweka sawa kuhusu hizi propaganda kuwa Magufuli kafikia uchumi wa Kati kabla ya muda uliopangwa.

Kikwete kaweka sawa kuwa Uchumi wa Kati uliopangwa ni dola 3,000 na sio hii 1080. Na kampa Magufuli challenge kuwa 2025 inatakiwa awe amefikia kipato hicho kwa kila mtanzania.

Pia kaweka rekodi nyingine sawa kuwa Uchumi kukua kwa asilimia 7 Ni Mkapa ndio aliweka na baada ya Mkapa haijawahi kushuka hiyo Kasi.

Hii ni tofauti na propaganda za Sasa hivi kuwa Magufuli ndio kapandisha Kasi ya ukuaji Uchumi.

Sio Magufuli aliyesema tuko uchumi wa kati ni World Bank, so kawaulize hao ndio mtajua
 
Kwani hatujafikia uchumi wa kati kwamba anaongopa?
Hiyo haikuwa target yetu mkuu and our indicator for that is USD 3000 by 2025 unless Kama anatekeleza plan na target zilizopo kichwani mwake
 
Unajua lengo la kuweka matuta kwa nchi kama tanzania hasa ni nini?
Watu ni vilaza,madereva can not observe roads signs na wafuka kwa miguu nao ni hivyo hivyo.so matuta ndo yanatusaidia kusimamia sheria kwa sababu sisi hatuwezi sababu ya ukilaza wetu
 
Acha ramli chonganishi rais Magufuli alielezea vizuri tangu siku anarudisha form ya urais kuwa kazi ya kuipeleka nchi uchumi wa kati ilianzishwa na wa tangulizi wake. Kwenye timu ya mpira sifa anapewa mfungaji bora anayepokea pasi ya mwisho.
Nilishaandika humu mara nyingi TATIZO SIO JPM BALI NI YALE MAFISI YALIYOMZUNGUKA NA "MASHANGILIZI". Ndio hayo hupotosha na kumpa Mkuu uongo ili maslahi yao yatimie kisha hujifanya wao ndio wazalendo kuliko watanzania wengine. Inaposemwa kinyume na mapenzi yao ndipo utasikia "wasaliti... wanatumiwa na mabeberu!" Ilhali wao ndio wameifikisha nchi hapa tulipo.
 
Viwango vya uchumi wa kati wa chini na juu vimewekwa na WB. Sasa kuna watu kweli na akili zao timamu walikuwa hawafahamu hili? Leo ndio wamefahamu kwamba JK na BWM ndio walipanga?

''The World Bank classifies the world's economies into four income groups — high, upper-middle, lower-middle, and low. We base this assignment on Gross National Income (GNI) per capita (current US$) calculated using the Atlas method.''

''(MIC) According to the World Bank, middle-income countries (MICs) are defined as economies with a Gross National Income (GNI) per capita between $1,026 and $12,475. MICs are one of the income categories that the World Bank uses to classify economies for operational and analytical purposes.''

Haya majungu sijui yataisha lini, Watanzania tuwe macho na wapotoshaji.
 
We hujaelewa
Ni kweli tumefikia Uchumi wa Kati, according to WB

Na kulikuwa na lengo limewekwa kuwa tukifika 2025 tuwe tumefikia Pato la 3000 kwa kila Mtz

Lakini ilivyokuwa inasemwa Ni kuwa Magufuli amelifikia lengo la Uchumi wa Kati kabla ya 2025,
lakini lengo lenyewe halikuwa just Uchumi wa kati Bali Uchumi wa Kati wa dola 3000 kwa Wastani
Wewe ndio huelewi na hii yote inasababishwa na hasira ulizonazo kwa Magufuli personal

Hakuna mahala popote Magufuli aliwahi kusema wameshafikia malengo yao ya dola elf 3 kabla ya 2025

Alichosema yeye ni furaha aliyonayo WB kuwatangaza uchumi wa kati kabla ya 2025 waliyoikadiria wao.

Hiyo ya lengo la dola elfu 3 bado liko palepale na Jk alimwambia Magufuli ajitahidi hadi 2025 aifikie ili kumuemzi Mkapa.
Sasa hapo usichoelewa ni nini?
 
MATAGA watamuona JK ni bonge la Snitch.

Amesema kazi ya Magu sasa ni kututoa hapa kwny kipato cha $1,080 na kufikia $3,000 by 2025 ili kufikia uchumi wa Kati.

Yaani kama tangu 2005 mpk 2020 wamepambana marais hatari ndio tumefikia $1080 sijui miujiza ya aina gani itafanyika ndani ya miaka 5 kufikisha $1,920 zingine.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti bonge la snitch
 
Watu ni vilaza,madereva can not observe roads signs na wafuka kwa miguu nao ni hivyo hivyo.so matuta ndo yanatusaidia kusimamia sheria kwa sababu sisi hatuwezi sababu ya ukilaza wetu
Sasa hapo kilaza nikiongozi wako au ni wewe usieelewa alama za barabarani unaenda tu kama nyumbu mpka kiongozi wako anaamua kukuwekea alama mbadala?
 
Sasa hapo kilaza nikiongozi wako au ni wewe usieelewa alama za barabarani unaenda tu kama nyumbu mpka kiongozi wako anaamua kukuwekea alama mbadala?
Kilaza ni yule aliyefikia uamuzi wa kutumia matuta kusimamia sheria
 
Back
Top Bottom