Uwezi kumlinganisha Kikwete na Magufuli, Kikwete aliwekeza kwenye anasa, watu waliokuwa hawafanyi kazi, rushwa, nk, mpaka Magufuri anaingia madarakani kwenye azina pamekauka, Magufuri kukusanyika amewekeza kwenye miundo mbinu imara, kafufua mashirika yaliokuwa maututi, pamoja nahayo bado ameipaisha nchi mpaka kwenye uchumi wa kati. Kikwete alikuta azina kumejaa Yeye kaanza kula bata,. Kikwete Rais mbovu kutokea Tanzania
Tunavyodanganyana hivyo... eti hazina palikuwa pamekauka!! Kama hazina palikuwa pamekauka, unataka kusema wafanyakazi walikuwa hawalipwi mishahara?!
Kama hazina palikuwa pamekauka, unataka kusema wanafunzi vyuo vikuu walikuwa hawapati mikopo na grants zingine?
Kama hazina palikuwa pamekauka, unataka kusema shughuli za serikali zilisimama?
All in all, wakati nafahamu Wafuasi wa JPM hamna utamaduni wa kutafuta taarifa wenyewe na ndio maana inakuwa rahisi kudanganywa, ningekushauri spend few minutes na ku-Google the following Keyword " BOT Economic Overview 2015/2016" ambako utapata BoT's Annual Report, na sehemu ya ripoti inasema:-
Sasa how come unadai Hazina ilikauka wakati as of June 30, 2015 kulikuwa na Foreign Reserve ya USD 4.402 Million wakati hiyo ni zaidi ya TSh. TRILLION 9?! Yaani Hazina yenye zaidi ya shilingi Trilioni 9 ndo ilikuwa imekauka?!
Na wakati unadai JK kaacha hazina pamekauka wakati alikuta PAMEJAA,
Global Economy wanatueleza Mkapa aliacha nini pale Hazina:-
Kama ulisoma Statistics na Histogram angalau O-Level, utaona hapo wanaonesha 2005 ambayo Mkapa kaondoka madarakani, aliacha reserve ya roughly USD 2 Billion!!!
Sasa how come unadai JK alikausha Hazina wakati alikuta IMEJAA, and at the same time, data zinaonesha JK alipandisha Hazina from roughly USD 2 Billion to USD 4.4 Billion?!
That's one, but second, what did you just say?! JPM ndie kaipaisha nchi kwenye uchumi wa kati?! Kaipaisha kutoka hatua ipi na yeye kaipaisha kwa kiasi kipi?!
Tuangalie huo Uchumi wa Kati ambao World Bank walitangaza takwimu zake, tunaona mtu ambae unadai aliacha Hazina ZERO, huku akiwekeza kwenye ANASA, alipandisha GNI per capita from USD 720 in 2010 hadi USD 980 in 2015... yaani ongezeko la USD 260!!
Lakini hadi ripoti inatolewa, mwezi July under JPM, ndo kwanza kwa muda wote huo JPM alikuwa ameitoa Tz from USD 980 to USD 1080... yaani ongezeko la USD 100 TU kwa muda wote aliokaa madarakani!!!
Na kwa kuangalia GNI Growth kuanzia kipindi cha Mkapa hadi sasa, World Bank wanakupa takwimu zao hapa chini:-
Sasa huo ubora wa JPM kumlilinganisha na waliomtangulia unaupima kwa kutumia vigezo gani wakati takwimu ndo hizo hapo zinaonesha kapandisha for only USD 100 kwa muda wote aliokaa madarakani?!
Kwa upande mwingine, unadai eti JPM kafufua mashirika ambayo yalikufa!!!!
Shirika gani kwa mfano?! Loss Making
ATCL aliyoinunulia ndege za over TZS 1 Trillion, and later:-
Yaani ndo ufufuaji wa mashirika unaousema huu?! Yaani una-invest millions of dollars without a comprehensive business plan ndo unaita kafufua mashirika yaliyokua maututi wakati kaiingizia nchi hasara zisizo na maana, matokeo yake, anaamua kuihamishia Ofisi ya Rais ili CAG asitie mkono:-
Na taarifa hiyo inaendelea kusema kwamba:-
Mr Kabwe argues that over Sh1 trillion has been spent on the purchase of the aircraft but was yet to be audited by the Controller and Auditor General. “This year the government is asking Parliament to approve another Sh500 billion for
the purchase of more aircraft but it is surprising now that they are moving the flight agency to the office of the president where no one will query the expenditure. What are you out to hide,?” queried the MP
Yaani JPM katumia zaidi ya Sh Trillion 1 kununua ndege, na hadi habari hiyo inatolewa April 2019 shirika lilikuwa halijakaguliwa, na hapo hapo bado JPM anaomba more TZS 500 Billion, halafu unakuja hapa kudai eti "kafufua mashirika yaliyokuwa maututi"!
Kwanini Agency ambayo ndiyo mmiliki wa ndege za ATCL ameihamishia Ikulu?! Kwanini haijakaguliwa?!
Again unadai Magufuli kwenye miundombinu!! Miundombinu ipi wakati kama suala ni barabara nyingi ni za tangu awamu zilizopita, na hata alizozindua yeye kwa mara nyingine zilikuwa zimeanza kujengwa tangu awamu iliyopita?!
Flyovers ingawaje ni kitu kidogo sana lakini Wafuasi wa JPM mmekuwa mkitumia suala la flyover kama moja ya success ya JPM wakati ukweli ni kwamba, mpango wa Flyover ulianza way back in 2007 serikali walipoiomba Japan kujenga Flyover TAZARA na Ubungo!!
Baada ya hapo, Japan, kupitia JICA wakafanya pre-feasibility study kujiridhisha ikiwa kuna uhitaji wa Flyover lakini wakafikia conclusion kwamba, by the time ilikuwa inahitajika zaidi BRT lakini in the near future, from 2015, suala la Flyover litakuwa halikwepeki:-
From pre-feasilibility, zikaja feasibility studies nyingine, na hadi JK anaondoka madarakani, Serikali ya Japan tayari ikawa imeshatoa fedha za ujenzi, na JPM akaja tu kuifanya kazi anayoiweza zaidi:- UNYAPARA wa kusimamia ujenzi wa Flyovers!
Tanzania National Roads Agency (TANROADS) and Sumitomo Mitsui Construction Co.,Ltd. (SMCC) signed a contract on 15th October, 2015 concerning the project for Improvement of Tazara Intersection which will mark the construction of the first Flyover in Tanzania under the framework of the grant aid project supported by JICA.
Source:
JICA
So, endeleeni kudanganyana wenyewe kwa wenyewe na habari zenu za kuokoteza vichochoroni, huku source zenu zingine, zikiwa ni wanasiasa wakati mnatembea na libraries mikononi mwenu!!!