Mzee Kikwete: CCM ya sasa ukimtambulisha kiongozi wa Upinzani anaonekana Adui, nilimpigia kampeni Dr Ndugulile WHO, Ummy naye alifanya Kazi Kubwa!

Mzee Kikwete: CCM ya sasa ukimtambulisha kiongozi wa Upinzani anaonekana Adui, nilimpigia kampeni Dr Ndugulile WHO, Ummy naye alifanya Kazi Kubwa!

Akiwa msibani kwa Faustine Ndugulile Rais mstaafu Dr Kikwete amesema kwa CCM ya sasa kumtambulisha kiongozi wa Upinzani hadharani unaonekana Adui yaani Kirusi.

Kikwete amesema hayo wakati akimtambulisha mbunge wa Viti Maalum Halima Mdee (Chadema)

Aidha Kikwete amesema baba yake Faustine yaani hayati Mzee Ndugulile alikuwa ni Rafiki yake na wamefanya Kazi pamoja Wizara ya Mambo ya nje.

Kikwete amesema alishiriki kumfanyia kampeni za WHO marehemu Faustine kwa kuongea na Viongozi mbalimbali wa Africa nao walikubali kutuunga mkono hata Senegal alipiga Simu kwa Waziri Mkuu naye akakubali Moja kwa Moja kuunga mkono Tanzania.

Pia Ummy Mwalimu alifanya Kazi Kubwa sana kuhakikisha Faustine anashinda.

Nawatakieni Dominica NJEMA 🌹


JK kasema ukweli, ila naona kuna mtu specifically anamtumia ujumbe
 
Magufuli alikua nguvu ya wazee kwenye maamuzi ya chama. Nguvu ya wazee iliasisiwa na Nyerere. Kwankulitambua Hilo Magufuli akaamua kuwapunguza nguvu na kuwato katika sehemu ya maamuzi magumu ya chama. Akàanzisha kilichoitwa Baraza la ushauri ambalo halina meno. Kama mnavyojua ushauri ni ama ukubaliwe au ukataliwe. Baada ya kuwanyima nguvu akaanza kuwang'ong'a hadharani wazi wazi akijua hakuna WA kumfanya chilochote. Akaingiza kundi la wajinga na watumia nguvu kwenye chama kuliko hoja huku wakiimarisha ndoa Yao na vyombo vya Dola sambamba na mabadiliko lukuki ya Sheria za usalama na ulinzi!
Uadui miongoni mwa watanzania kwa misingi ya chama iliasisiwa na huyo na Wala hakiwezekani kupingwa. Kikwete alipeleka maendeleo kwa maeneo yalichagua upinzani kama njia ya wlkwashawishi wananchi wakuunge mkono na chama chake. Magufuli aliweka bayana kwamba hawezi na hatopeleka maendeleo Kwa watu wenye itikadi tofauti na chama chake. Alienda mbali kuwafananisha na magunzi na kutaka hadharani. Hii ilichochea na kurasimisha ukatili na uadui dhidi ya upinzani.
Yani huyu Mzee nlikua simpendi Bora Mungu alituondooea hili Baa 21/3/2021 maana lilikua baya zaidi ya Sodoma na Gomora Muasisi wa yote haya matukio ya Umwagaji damu
 
Back
Top Bottom