Mzee Kikwete: Manji alinambia wanamuonea, nikamshauri akae kimya kwani yatapita tu

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Jana ilifanyika dua ya kumuombea mfanyabiashara hayati Yusuph Manji katika viwanja vya Karimjee na mmoja wapo ya watu mashuhuri waliokuwepo ni Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne.

Katika hadhara hiyo, JK akapata wasaa kuongea, anasema kwake yeye Manji alikuwa kama mwanae na alimlea kwani aliachiwa usia na baba yake Manji la jukumu la malezi ya Yusuph.

JK akaongeza zaidi, kuna wakati Yusuph alinipigia(kipindi hiko nimeshatoka madarakani) akawa analalamika kuwa wanamuonea wanambambikia makesi na mambo mengineyo.

Nikamshauri akae kimya kwani nilijua siku moja yatapita tu, Yusuph alikuwa ana urafiki mkubwa sana na mwanangu Miraji.

PIA SOMA
- TANZIA - Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani
 
Jana ilifanyika dua ya kumuombea mfanyabiashara hayati Yusuph Manji katika viwanja vya Karimjee na mmoja wapo ya watu mashuhuri waliokuwepo ni Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne.

Katika hadhara hiyo, JK akapata wasaa kuongea, anasema kwake yeye Manji alikuwa kama mwanae na alimlea kwani aliachiwa usia na baba yake Manji la jukumu la malezi ya Yusuph.

JK akaongeza zaidi, kuna wakati Yusuph alinipigia(kipindi hiko nimeshatoka madarakani) akawa analalamika kuwa wanamuonea wanambambikia makesi na mambo mengineyo.

Nikamshauri akae kimya kwani nilijua siku moja yatapita tu, Yusuph alikuwa ana urafiki mkubwa sana na mwanangu Miraji.
Sema JK ni mwanadamu wa kipekee sana. Watu wa aina yake huwa wanaishi maisha marefu sana.

Jamaa hajawahi kujali maneno ya watu no matter how serious the issues are.
 
Back
Top Bottom