Jana ilifanyika dua ya kumuombea mfanyabiashara hayati Yusuph Manji katika viwanja vya Karimjee na mmoja wapo ya watu mashuhuri waliokuwepo ni Jakaya Kikwete, Rais mstaafu wa awamu ya nne.
Katika hadhara hiyo, JK akapata wasaa kuongea, anasema kwake yeye Manji alikuwa kama mwanae na alimlea kwani aliachiwa usia na baba yake Manji la jukumu la malezi ya Yusuph.
JK akaongeza zaidi, kuna wakati Yusuph alinipigia(kipindi hiko nimeshatoka madarakani) akawa analalamika kuwa wanamuonea wanambambikia makesi na mambo mengineyo.
Nikamshauri akae kimya kwani nilijua siku moja yatapita tu, Yusuph alikuwa ana urafiki mkubwa sana na mwanangu Miraji.