Mzee Kikwete pokea maua yako kwa hizi shule za kata. Kuna Wana-CCM baadhi watapinga

Mzee Kikwete pokea maua yako kwa hizi shule za kata. Kuna Wana-CCM baadhi watapinga

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
15,331
Reaction score
22,307
Mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni, baada ya kumaliza shule ya msingi mwaka 1986, Sikuchaguliwa kujiunga na secondary ya serikali kwa maana nafasi zilikuwa chache na hata waliochaguliwa pia walikuwa wachache na wakati mwingine shule haitoi hata mwanafunzi mmoja wa kujiunga na kidato Cha kwanza!

Kwa sisi tuliosomea Kwa kina Babu na Bibi wengi wa waliofaulu walikuwa ni watu waliomaliza kitambo na kurudia Tena shule madarasa ya la 5,6,7 hivyo kufanya watu Hawa kufaulu.

Baada ya kuingia madarakani Raisi mstaafu na timu yake,wakaanzisha shule za kata, hapa CCm Ndio pa kujifunza Hapa: Watoto wakasoma hadi wengine Kwenda shule za vipaji!

Wakaelimika na kutoka vijijini kwenda mjini hadi Amerika na Ulaya!Wakajifunza mambo mbalimbali na kuona dunia inavyokwenda!
Zikazidi kuongezeka na wahitimu wakazidi kuongezeka! Kipengele kimekuwa ajira. Kwa Sasa wahitimu wa vyuo vikuu wamejazana vijijini hadi Mijini.

Mambo yamechangamka, uelewa umekuwa mpana, hakuna mtu wa kumdanganya. Sisi wengine tulilipiwa secondary na Wazazi wetu, wenye uelewa na Dunia tulikuwa wachache ña simu za Kisasa hazikuwepo,Tv nk.

Sasa hivi Dunia ni kama Kijiji, watu wameelimika pakubwa Hivyo basi, kulazimisha mambo ambayo mengine yanaonekana Kwa macho ni kuikosea Akili,ambayo kila mtu amepewa na Mwenyezi Mungu na kuongezeka maarifa Kwa Hizi Shule Za Kata!

Mithali 4:13(Mkamate sana Elimu,Usimuache aende zake;mshike, Maana yeye ni Uzima wako).

Tuna Cha kujifunza kama Watanzania hivi Sasa hutuna haja ya kutumia nguvu kubwa kulazimisha mambo ni kucheza na upepo na jinsi watu wanavyotaka Kwa kusaka maarifa popote.

Mwashambwa na Tlaahtlaah Mpo?

Yangu ni hayo Namshukuru Mungu na Nampa maua yake Dr Kikwete Kwa jambo hili Jema. Kazi na na utu ndio msingi wa Amani na Haki na Ustawi wa nchi.
 
Back
Top Bottom