Mzee Kilomoni: Simba haiwezi kuchukuliwa na mtu mmoja, narudia tena haiwezekani

Mzee Kilomoni: Simba haiwezi kuchukuliwa na mtu mmoja, narudia tena haiwezekani

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kimenuka huko mtaa wa pili wa Kinywaji maarufu kijulikanacho 7UP.

Mmoja wa viongozi wa bodi ya wadhamini kwa muda mrefu sana pale SABASABA FC leo ametanabaisha wazi kuwa uongozi wa klabu hiyo unafanya mambo ya kiofisi kihuni, na kuhusu mpango wa kumpa "MO'' timu amesema hautokuja wezekana kamwe.

Na kwamba kama wanaSABASABA FC wanataka mabadiliko, basi wataendelea kuyapata bila kuiweka rehani klabu hiyo....''Kwani kama mabadiliko Simba tumefanya mengi, tulikuwa hatuna majengo sasa tunayo, hatukuwa na kiwanja sasa tutajenga karibuni," Alinukuliwa akisema

Mzee huyo anayeheshimika kwenye klabu hiyo alitanabaisha hayo yote wazi akiongea na vyombo vya Habari alasiri hii.


4.PNG
1.PNG
2.PNG
3.PNG
 
Mfumo wa hisa hauepukiki tukutane kwenye mikutano yetu ya clab ya simba na wao wawepo tuwasikie kama wana hoja
 
Anajitekenya tu, mahakama ilishawatimua saizi wanahaha tu! Ingekuwa utawala wa JK kweli mabadiliko yangeshindikana sababu ya figisu. Ila sasa hivi wanajua hawana chao msajili ameshaelekeza cha kufanya kwenye marekebisho ya katiba. Hata debe hutoa sauti linapokuwa tupu. Wapige kelele ila pia wajiandae kisaikolojia kwa mabadiliko. Watu gani kazi yao kuleta vurugu tu? Timu ikiwa na matatizo hawaonekani! Wapumzike wale ugali wa muhogo na vipande vya papa waliyozoea! Wanakera sana hawa vigagula!! Vyura fc nako akilimali katulia baada ya kuona njaa kuu na ya kutukuka imeingia, na hawa vigagula ndio wanachotaka kitokee na kwa upande wa mnyama! Wamefeli.

Arage Jekundu.
 
Ivi huyu Kilomoni anajua maana ya hisa?
Anajua jinsi biashara ya hisa inavyoendesha timu za
Ulaya ?
Anahitaji kuelimishwa tu huyo mzee Kilomolomo.
 
Ushauri wa bure kwa hawa wazee. hivi vilabu viwili (simba na yanga) haviwezi kuendeshwa kama zamani tena. Kwa sasa japo haijawa rasmi lakini Tanzania mpira umeshakuwa wa kulipwa. siku zote mabadiliko yoyote lazima yapate upinzani kwani hulka ya binadamu ni kiumbe mwenye hofu kwa kupokea kitu kipya. Kama vurugu zitaendelea namshauri Mo akae pembeni halafu mzee Kilomoni na Bi Hindu wapewe timu waigharamie kambi walau kwa siku moja tu. Au walipe mshahara wa mwezi mmoja tu wa mchezaji Jamal Mnyate achilia mbali wa Okwi.
 
Back
Top Bottom